Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 80...
Wakarudi barabarani, wakasimisha gari na kumwambia Ibrahim ateremke na Malaika huku mvua kubwa ikipiga nje. Ibrahim hakuwa na jinsi, akamchukua Malaika wake, akamshusha kutoka garini na kumuweka kwenye lami.
“Bro! Mbona mnataka kutuacha! Mbona mnanichia majanga?” aliuliza Ibrahim huku akilia, kila alipomwangalia mpenzi wake, Malaika moyo ulimuuma mno.
“Baki naye, utaomba msaada! Msaada pekee tuliowapa ni kuwaacheni hai!” alisema Jumanne na Fredi kuliondoa gari mahali hapo ambapo baadaye akampigia simu David na kumwambia kwamba tayari waliwaua watu hao kwa kuamini kwamba wasingeonana tena katika maisha yao.
Ibrahim akabaki na Malaika wake, aliangalia kila upande, hakukuwa na magari mengi yaliyokuwa yakipita na hata yale machache yaliyokuwa yakipita mahali hapo hayakuwa yakisimama hata kidogo.
Alishindwa kujua afanye nini, kila alipomwangalia Malaika, moyo wake ulimwambia kwamba hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho za uhai wa msichana huyo mdogo ambaye tangu kuzaliwa kwake, alikuwa mtu wa kuteseka tu.
“Malaika usiniache! Usiniache Malaika subiri niendelee kusimamisha magari,” alisema Ibrahim huku akiwa amemuinamia msichana huyo na mvua kali ikiendelea kunyesha.
Ibrahim hakutaka kuacha, bado alihitaji msaada mkubwa kutoka kwenye gari lolote lile, alimwangalia msichana Malaika, alionyesha kabisa kwamba alikuwa akienda kufa kwani kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa, alionekana kutokuwa na muda mwingi wa kuendelea kuishi.
Magari hayakusimama, yaliendelea kuwapita. Uamuzi wa mwisho kabisa alioufanya Ibrahim ni kumbeba Malaika na kumuweka katikati ya barabara na kusimama karibu yake, alitaka kuona gari lolote ambalo lingepita alisimamishe.
Wala hazikupita dakika nyingi, gari ndogo aina ya Spacio likaonekana mbele yake. Ibrahim akapunga mikono juu kama kulisimamisha gari hilo.
Alikuwa akipiga kelele ili aonekane kwani kama asingelisimamisha na gari hilo kupita, ilimaanisha lingemgonga yeye na msichana Malaika aliyelala chini.
Itaendelea.