Sarafina - Mtunzi Nyemo Chilongani

Sarafina - Mtunzi Nyemo Chilongani

SEHEMU YA 38...

Uzuri wa Gloria ulikuwa balaa, David alikuwa na mawazo tele, kila alipokaa alimfikiria msichana huyo mrembo. Alikuwa mtoto wa kishua, baba yake, Mzee Mpobela alikuwa mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania, alikuwa na makampuni mengi, maduka makubwa, migodi ya dhahabu na vitu vingine vingi.

David alilijua hilo, alihakikisha kwamba anamchukua msichana huyo ili maisha yake yawe laini, apate afueni ya maisha kwani kama kuchunwa na wanawake, alichunwa vilivyo na aliona huo ndiyo muda wa yeye kula pesa za msichana.
Walikuwa wakiwasiliana kama marafiki, David hakutaka kukaa sana kwenye mawasiliano ya kirafiki kitu kilichomfanya kuanza kumchombeza msichana huyo kwa maneno matamu, kwamba alikuwa mzuri kiasi kwamba hata Mungu alikuwa akijivunia kumuumba msichana mzuri kama yeye.

“Hukutakiwa kuwa binadamu, wewe ulitakiwa kuwa malaika,” alisema David, alikuwa akizungumza na msichana huyo ana kwa ana.
“Kweli?”
“Ndiyo! Gloria, nimeona warembo wengi, weupe, weusi, warefu na wafupi, ila kwako! Huna kasoro, wewe ni mrembo uliyekamilika,” alisema David huku akimwangalia Gloria machoni.

Alizaliwa kwenye familia ya kitajiri, alipata kila kitu alichokihitaji ila katika maisha yake alikosa kitu kimoja tu, kusifiwa na mwanaume. Kila mtu aliyemtaka, hasa watoto wa mabilionea wengine, walimfuata, walimpeleka klabu na baada ya kutoka huko wakawa wanafanya mapenzi bila kutongozwa.

Hayo yalikuwa maisha yake, hakuwahi kuambiwa kwamba alikuwa mrembo, hakuwahi kuambiwa kwamba alikuwa na tabasamu pana. Maneno yote hayo aliambiwa na David, ndiyo maneno yaliyomfanya kujisikia kwamba alikuwa mwanamke mrembo, mwenye sifa za kimalaika.

Gloria akajiweka mikononi mwa David, akatokea kumpenda mwanaume huyo kiasi kwamba kwake alikuwa haoni hasikii, haambiwi chochote kile. Hakutaka kujificha, kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia David alionekana kuwa kijana muoaji hivyo kumwambia baba yake na ndugu zake kwamba alipata mwanaume ambaye alistahili kuwa mume wake wa ndoa.

“Una uhakika anakupenda kweli?” aliuliza Mzee Mpobela huku akimwangalia Gloria.
“Ndiyo baba!”
“Narudia tena! Una uhakika anakupenda kweli?” aliuliza mzee huyo.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 39...

“Ndiyo baba!”
“Tunahitaji kumuona!”
Hilo halikuwa tatizo, haraka sana Gloria akawasiliana na David na kumwambia kwamba baba yake alitaka kumuona. Alilitegemea hilo, hakutaka kumdanganya Gloria kwani aliamini kupitia msichana huyo angepata kiasi kikubwa cha pesa na maisha yake kubadilika kabisa.

Akamwambia kwamba hilo lingewezekana na hivyo siku iliyofika kwenda nyumbani kwa kina Gloria. Mzee Mpobela alipomuona, akafurahi, alitamani sana kumuona binti yake akiwa na furaha kwani ndiye alikuwa mtoto pekee wa kike mbali na watoto wawili wa kiume aliokuwa nao.

Akakaribishwa ndani ya nyumba hiyo, akaambiwa chochote ambacho angekihitaji angepewa ila alitakiwa kumuheshimu sana Gloria kwani ndiye alikuwa mwanamke aliyemfanya kuwa pale alipokuwa.

“Haina shida baba. Lengo langu ni kumuoa Gloria! Hakuna kingine,” alisema David.
“Tunatoa baraka zote!” alisema mama yake Gloria.
Uhusiano ukawa wazi, David alifurahi kwani kile alichokuwa akikihitaji kilikuwa kimetimia. Kwa kuwa alimaliza chuo na hakuwa na kazi, akapewa kiasi cha fedha cha milioni kumi na kuambiwa kuanza kufanya biashara na kiasi kingine angepewa ndani ya siku chache.

“Nashukuru sana! Nitafanya biashara nyingi kweli,” alisema David huku akikenua, kitendo cha kuwa na Gloria kilimuonyesha maisha mazuri, ila hakujua kitendo cha kuwa na Gloria, kwa upande wa pili kilimuonyesha mwanzo wa maisha yaliyojaa mateso makubwa.

**** Daktari akatoka ndani ya chumba kile, akamkuta nesi wake akilia na Sarafina. Hakujua ni kitu gani kilitokea mpaka wawili hao kulia namna hiyo. Hata kabla hajauliza kitu chochote kile, akachukua koti lake refu na kisha kumvisha Sarafina aliyekuwa na nguo ya ndani pamoja na sidiria.

Akamuuliza nesi kilichokuwa kikimliza na majibu yake ni kwamba aliumia sana jinsi mtoto Malaika alivyokuwa akiumwa. Hakutegemea kumuona mtoto aliyekuwa akiumwa namna ile na wakati mama yake hakuwa na uwezo wowote ule.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 40...

Moyo wake ulichoma kupita kawaida, hakuendelea kubaki mahali hapo, akaondoka kwenda nje huku akianza kulia kwa kilio cha kwikwi. Daktari akamchukua Sarafina na kuelekea naye katika ofisi yake, huko, akamwambia kilichokuwa kimetokea kwamba mtoto wake alikuwa kwenye hali mbaya japokuwa wao kama madaktari walikuwa wakipambana kumtibu kama kawaida.

“Anasumbuliwa na degedege na ndiyo maana hali yake imekuwa mbaya namna ile,” alisema daktari huku akimwangalia Sarafina.
“Atapona?” aliuliza kwa sauti ya chini.
“Atapona. Umetokea wapi?”
“Ilala! Nilikuwa mitaani tu!”
“Umetoka Ilala mpaka huku?”

“Ndiyo! Kwa miguu! Dokta! Naomba unisaidie mtoto wangu apone,” alisema “Mbona hukumpeleka hata Magomeni?” “Sipafahamu! Ninapafahamu hapa na Muhimbili tu! Sikukaa sana Dar es Salaam dokta. Naomba umsaidie binti wangu,” alisema Sarafina na kuanza kulia mahali hapo.

Moyo wake ulimuuma, ulichoma, alihisi kabisa kitu chenye ncha kali kikimchoma moyoni. Aliendelea kubaki hospitalini hapo, dokta yule aliendelea kumtibu Malaika. Hakukuwa na aliyelala, kila mmoja alikuwa macho.

Yule mwanaume aliyemsaidia hakutaka kuendelea kubaki hospitalini hapo, akaondoka huku akiahidi kumtembelea tena mapema siku inayofuata
Moyo wa Sarafina ulimwambia kabisa kwamba mtoto wake hakuwa na muda mwingi wa kuishi, ilikuwa ni lazima afariki dunia kitandani pale. Alimwambia daktari kwamba ingekuwa vizuri kama angepata nafasi ya kwenda kukaa na mtoto wake chumbani mule, pembeni ya kitanda chake kwa ajili ya kufuatilia kila hatua.
Hilo halikuwa tatizo, akaruhusiwa na kuingia ndani. Macho yake yalipotua kwa Malaika, moyo wake ukauma zaidi, kitandani pale alipokuwa amelala alionekana kama mfu, mashine ya kupumulia ilikuwa puani mwake huku dripu ikining’inia juu yake.

Sarafina alilia, aliendelea kuumia, usiku mzima hakuyaruhusu macho yake kufumba, alikesha huku akimwangalia Malaika tu. Alimuomba Mungu pembeni ya kitanda cha mtoto wake, aliamini kwamba angeweza kumpa nafasi nyingine ya kuishi.

Itaendelea.
 
01

“Jamani leo natangaza rasmi….” alisikika jamaa mmoja akiwaambia wenzake.
“Tangaza…” wenzake walisema huku wakicheka.

“Kuanzia leo kwa hapa chuo, hakuna demu mkali kama yule Msukuma…” alisema jamaa huyo.
“Msukuma gani?” aliuliza jamaa mmoja huku akimwangalia mwenzake huyo aliyeamua kutangaza.
“Sarafina Butati! Yaani hakunaga!”
“Hahaha!” watu wote wakajikuta wakicheka.

“Jamani yule mtoto mkali! Jamani yule mtoto anaita! Jamani yule mtoto ana figa! Jamani! Jamani! Jamani! Nasema hivi! Kwa hapa chuo hakuna demu mkali kama Sarafina,” alisema jamaa huyo.
“Anamshinda Manka wa Kichaga?” aliuliza jamaa mwingine.

“Manka! Hivi yule demu anaingia kwa Sarafina? Hivi ushawahi kuvuta picha kichwani mwako ukamuona Sarafina akiwa mtupu? Yule mtoto jamani ni mkali sana, kuna kila haki ya sisi marijali kumpigia misele,” alisema jamaa huyo na wote kuanza kucheka.

Huyo ndiye msichana aliyekuwa gumzo katika Chuo cha Amazon kilichokuwa Temeke jijini Dar es Salaam. Kila mwanaume aliyekuwa katika chuo hicho cha ufundi alivutiwa na msichana huyo, uzuri wake uliwapagawisha wanaume wengi kiasi kwamba kila mmoja alimtolea macho.

Sarafina alikuwa msichana mrefu, mwenye mwendo wa maringo, alikuwa na hipsi pana ambazo kwa watoto wa mjini walipenda kuziita pisto, alikuwa na miguu iliyojazia kidogo huku akiwa na mapaja manene kiasi kwamba kila alipoyaruhusu yaonekane, kila mwanaume aliyamezea mate.

Usoni hakuwa wa kawaida, alikuwa na sura nyembamba, mdomo wake ulikuwa na lipsi pana, hata kama macho yake alikuwa akiyakaza, bado yalionekana kusinzia kwa mbali mithili ya mwanamke aliyekula kungu.

Mashavuni mwake alikuwa na vishimo viwili ambavyo viliufanya uzuri wake kuonekana kila alipokuwa akicheka hata kutabasamu. Hakuwa msichana wa kusuka, muda mwingi nywele zake alikuwa akizikata huku sura yake hiyo akiipendezesha na miwani meusi.
Sarafina hakujua kutembea kwa kasi, kila alipokuwa akitembea, alitembea kwa mwendo wa maringo kana kwamba hakuwa akikanyaga ardhi hiihii.

Aliwadatisha wanaume wote waliokuwa chuoni hapo, kila mmoja alimpenda, kila mmoja alitamani hata siku moja msichana huyo mrembo awe mpenzi wake.

Itaendelea
Na wewe umekuwa mtunga story!??? Ina maana boy wako kakushauri hivi???
 
SEHEMU YA 41...

“Mungu! Nakuomba umpe nafasi nyingine. Kama umempa nafasi ya kufika hospitali salama, kwa nini usimpe nafasi nyingine ya kuwa na afya tena?” aliuliza Sarafina huku akionekana kuwa na huzuni mno.

Mpaka asubuhi inaingia, bado Malaika alikuwa kwenye hali ileile. Sarafina hakuacha kumuomba Mungu, aliamini kwamba angeweza kumponya mtoto wake. Hali yake haikubadilika lakini ilipofika saa nne asubuhi, mwili wake ukaanza kurudi katika hali ya kawaida, joto la mwili wake likaanza kupungua na mwisho wa siku kuyafumbua macho yake.

Sarafina hakuamini alichokuwa akikiona, akatoka kitini na kupiga magoti chini, akainyanyua mikono yake juu na kumshukuru Mungu. Hakuamini kama alimpa nafasi tena mtoto wake ya kufumbua macho, kwa jinsi alivyokuwa akishukuru mpaka wagonjwa wengine walishangaa.

“Sina mwingine zaidi ya Malaika wangu. Najua nitakufa kwa kansa ya matiti lakini naomba huyu aendelee kuwa kwenye hali yake ya kawaida,” alisema Malaika huku akimwangalia mtoto wake.
Siku hiyo aliendelea kubaki hospitalini hapo, kila alipokuwa akiletewa chakula kwa ajili ya kula, alishindwa, hakuwa na hamu ya kula hata kidogo. Kitu alichokihitaji wakati huo si chakula bali ni afya ya mtoto wake tu.

Madaktari na manesi walimlazimisha kula lakini alikataa, aliwaambia dhahiri kwamba hawezi kula na wakati mtoto wake hakuwa akinywa uji, angejisikia vipi kama mzazi akashiba na mtoto wake kuwa na njaa?

Ilipofika saa moja usiku hali ya Malaika ikaanza kutengemaa kwa nguvu, akarudi katika hali yake ya kawaida, aliendelea kupata nafuu jambo lililomfanya Sarafina kufurahi kwani hakutegemea lile alilokuwa akiliona.

“Hali yake itaendelea kutengemaa, wala usijali!” alisema daktari huku akimwangalia Sarafina.

Sarafina na mtoto wake walikaa hospitalini kwa siku tatu ndipo akaruhusiwa kutoka. Hakuwa na pa kwenda, kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ndivyo ilivyokuwa kipindi hicho, akaanza kulala mitaani huku akiomba misaada katika magari yaliyokuwa yakipita.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 42...

Alikuwa kwenye kipindi kigumu mno, aliteseka lakini hakutaka kumuona mtoto wake akitoka mikononi mwake. Walizunguka sehemu kubwa, usiku wa saa nne ulipokuwa ukimkuta ndipo hapohapo alipokuwa akilala.

Maisha hayakubadilika! Alizurura kila kona jijini Dar es Salaam, hakuacha kuomba kwa kila mtu aliyekuwa akikutana naye njiani. Baada ya kupita miezi ndipo akabahatika kukutana na mtu ambaye alikuwa na hamu ya kukutana naye.

Siku hiyo, alinyeshewa sana na mvua, alikuwa amelowa, hakuwa na kitu, hakutaka kupumzika kwani tangu asubuhi mpaka muda huo ndiyo kwanza alipata shilingi elfu tano. Alijifunika khanga huku akiyafuata magari mbalimbali yaliyokuwa yamepanga foleni.

Wakati akiwa amelifuata gari moja la kifahari kwa lengo la kuomba, dirisha la gari likafunguliwa na msichana mmoja mrembo, aliyependeza kupita kawaida. Msichana huyo akamwangalia Sarafina, alimuonea huruma, alionekana kuteseka, mvua ilimpiga na alikuwa amemfunika Malaika kwa khanga yake ambayo haikuifanya kumzuia na maji ya mvua, aliendelea kulowa.

“Pole sana,” alisema msichana huyo huku akimwangalia Sarafina, dereva wa gari hilo alitulia, umakini wake ulikuwa mbele, alionekana kukasirika na foleni iliyokuwa ikimkabili.
“Nashukuru!”
“Mtoto wako mzuri! Anaitwa nani?” aliuliza msichana huyo.
“Malaika!”

“Ooh! Jina linaendana na yeye mwenyewe. Pole kwa mvua. Shika hii!” alisema msichana huyo huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa kaki uliokuwa na noti nyingi kisha kutoa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kumpa.

“Nashukuru! Nashukuru sana mama! Nashukuru sana,” alisema Sarafina huku akianza kupiga magoti, hakujali mahali alipokuwa, hakujali kama mvua ilikuwa ikinyesha sana, alichokuwa akikihitaji ni kumuonyeshea shukrani msichana huyo ambaye kwa msaada wake, na umri wake mdogo alimuita jina la mama kabisa.
“Usijali!”

Wakati wawili hao wakizungumza, macho ya Sarafina yakatua kwa mwanaume aliyekuwa akiendesha gari hilo. Alimwangalia vizuri, alikuwa David, mwanaume aliyewahi kutembea naye, akampa mimba na kisha kumuacha.

Itaendelea.
 
Kwendraaaa
Siendi popote nakaa hapa kushangaa maajabu ya ubongo mzembe duniani kama huu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
SEHEMU YA 43...

Hakutoa macho yake kwa David, aliendelea kumwangalia huku akiwa haamini kama kweli huyo alikuwa David au mwanaume mwingine aliyefanana naye kiasi kile.

“David…!” aliita Sarafina, David akashtuka, akamwangalia mtu aliyemuita, macho yake yakagongana na Sarafina, akasikia moyo wake ukipiga paaa!

Hakuamini alichokuwa akikiangalia, mbaya zaidi, alipoyapeleka macho yake kwa mtoto aliyebebwa na Sarafina, alifanana na yeye kwa kiasi kikubwa, alionekana mtoto mwenye njaa, alikuwa mwembamba mno kiasi kwamba unaweza kuhisi kwamba muda wowote ule angekufa.

“David…ni wewe?” aliuliza Sarafina lakini hata kabla mwanaume huyo hajajibu, foleni ziliruhusiwa, kwa haraka sana David akapiga gia, hakuzungumza kitu, akaliondoa gari mahali hapo na kumuacha Sarafina akiwa haamini alichokiona, akabaki akiwa amesimama, akitetemeka kwa baridi kali huku mvua ikiendelea kunyesha.

“Mungu wangu! David ameniacha, hakutaka hata kunisikiliza? Anakula maisha na mwanamke mwingine huku mtoto wake akiteseka?” alijiuliza Sarafina huku akilia, kile alichokiona, hakuamini kabisa.

**** David alichanganyikiwa, hakuamini kile alichokiona, picha ya msichana Sarafina ikaja kichwani mwake, hakuamini kama kweli yule msichana aliyechoka, aliyekongoroka, asiyekuwa na mvuto wowote alikuwa Sarafina, yule msichana aliyekuwa akimsifia kila siku, mwenye umbo mtata.

Alinyamaza ndani ya gari, hakutaka kuzungumza kitu, alikuwa na mawazo tele. Mtoto aliyekuwa amemshika alifanana sana na yeye. Moyo wake ukamwambia kwamba mtoto yule alikuwa wake, ila swali muhimu alilojiuliza ni kuhusu mtoto yule, ile mimba hakutoa? Na kama hakutoa, ni kitu gani kilitokea mpaka kuiacha.

Wakati yeye akifikiria hayo, naye Gloria aliyekuwa pembeni yake alikuwa akifikiria yake. Kichwa chake kilichanganyikiwa, alikuwa akijiuliza maswali mengi kuhusu msichana yule, ombaomba aliyekuwa mtaani ambaye alimsaidia kiasi cha fedha.

Ilikuwaje amjue David? Kwa nini David alivyoitwa alishindwa kusema kitu chochote kile zaidi ya kubaki akimwangalia mwanamke yule kwa macho yaliyojaa mshangao mkubwa? Je, walikuwa wakijuana au? Kila alilojiuliza, alikosa jibu kabisa.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 44...

“David! Tell me something,” (David! Niambie kitu) alisema Gloria huku akimwangalia mwanaume huyo.
“What do wanna know?” (unataka kufahamu kuhusu nini?) aliuliza David.
“Who was she?” (yule mwanamke ni nani?) aliuliza Gloria.

“My classmate?”(mwanadarasa mwenzangu)
“So, why didn’t you stop the car and listen to her? Is there something wrong?” (Kwa hiyo, kwa nini hukusimamisha gari umsikilize? Kuna tatizo lolote?) aliuliza Gloria.
“Nothing!” (hakuna kitu)

Hakujua ni kitu gani alitakiwa kumwambia Gloria, jinsi alivyoonekana, msichana huyo alijaza maswali mengi kichwani mwake. Alijua fika kwamba kama angemwambia ukweli huo ndiyo ungekuwa mwisho wa yeye kuwa naye hivyo ilikuwa ni lazima ampange rafiki yake, Paschal kwa ajili ya kulitatua tatizo lile.

“Hebu subiri kwanza. Yaani yule Sarafina kanichanganya,” alisema David, hapohapo akachukua simu yake na kupiga upande wa pili.
Gloria alikuwa akisikiliza tu, alitaka kujua ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Alimsikia David akizungumza na mwanaume kutoka upande wa pili, alikuwa Paschal ambaye pia alimfahamu kama rafiki yake mkubwa.

Akataka kuonana naye, hilo halikuwa tatizo na hata David alipokata simu, akamwambia kwamba walitakiwa kubadilisha safari na kwenda nyumbani kwa Paschal kwa ajili kuzungumza naye kuhusu yule msichana. Gloria hakukataa, alitamani kujua ukweli hivyo kwenda huko ambapo walitumia dakika thelathini, wakafika Kijitonyama Mabatini.

“Aisee nimekutana na Sarafina,” alisema David huku akimwangalia Paschal, yaani walitakiwa kuzungumza kikawaida na kwa sababu rafiki yake huyo alikuwa mzoefu wa kuunganisha stori, hakukuwa na tatizo lolote lile.

“Wacha weee! Sipati picha anavyoringa sasa hivi! Anafanya kazi wapi, kulekule uwanja wa ndege?” aliuliza Paschal.
“Daah! We acha tu! Yule demu amekuwa ombaomba mitaani!”
“Unasemaje? Sarafina huyuhuyu kawa ombaomba?”
“Ndiyo!”

“Pamoja na maringo yake yote yale? Pamoja na kukukataa kwa kukumwagia maji, leo kawa ombaomba?” aliuliza Paschal, alichokuwa akikizungumza ndicho alichokuwa akikitaka David.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 45...

“Ndiyo! Masikini weee! Sarafina amefikia hatua ile!” alisema David huku akiangalia chini, alijifanya kuumia sana.
“Duuh! Na Gloria kamuona?”
“Nimemuona. Kumbe mlisoma naye?”

“Ndiyo! Demu alikuwa ananata yule, anajua kuringa, alikuwa anapenda magari yule, mabosi ndiyo walikuwa wanamchukua tu!” alisema Paschal.
“Masikiniiiiii! Leo ndiyo amekuwa ombaomba!”

“Ni Mungu! Nadhani anamlipa kwa kile alichokifanya. Alijua kututukana wanaume,” alisema Paschal.
Kwa jinsi walivyokuwa wakizungumza, ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba kile alichokuwa akiambiwa Gloria kilikuwa ni uongo. Watu hao hawakupangana, hawakuzungumza kwa siri, kila kitu walichokuwa wakikizungumza kiliaminika kichwani mwa msichana Gloria na kuamini kwamba kweli Sarafina alikuwa msichana mbaya ambaye alikuwa na maringo mno.
Walipomaliza, wakaondoka, moyo wa David ukatulia, kidogo tabasamu likaanza kuonekana usoni mwake japokuwa bado alikuwa akijiuliza kuhusu Sarafina.

Maisha yaliendelea, mapenzi yaliendelea kwenda mbele, kila mmoja alimuonyeshea mwenzake jinsi alivyokuwa akimpenda. Sarafina hakutoka kichwani mwa David, moyo wake ulimuuma sana kwani alijua fika kwamba mtoto aliyekuwa na Sarafina alikuwa mtoto wake, alimuacha akiteseka mitaani na yeye akila raha na mwanamke mwingine kabisa.

“Ila sawa. Sina kosa, nilimwambia akatoe mimba, nikampa hela, kama hakutoa, hilo janga lake, mimi nilinawa mikono yangu! Sina hatia, naamini hata Mungu atanielewa,” alisema David huku akijaribu kuyatoa majonzi moyoni mwake, hakika akafanikiwa, moyo wake ukapoa, kaubaridi kakaingia, mawazo juu ya Sarafina na mtoto Malaika yakaanza kutoka, kwa kifupi ni kwamba alianza kurudi katika hali yake ya kawaida.

Itaendelea.
 
Siendi popote nakaa hapa kushangaa maajabu ya ubongo mzembe duniani kama huu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Shenzy zako kabisa mxxiuue
 
SEHEMU YA 46...

Sarafina aliendelea kusimama pale alipokuwa, hakuamini kama mwanaume aliyempa mimba, David ndiye alikuwa ndani ya gari lile, aliumia mno, akalia sana, akanyeshewa na mvua na hakutaka tena kuomba kwa siku hiyo, akaondoka kuelekea pembeni ya jengo moja kubwa, chini ya mti kisha kukaa na kuanza kulia.

Picha aliyoiona ilimuumiza mno, hakuamini kama kweli yeye ndiye aliyekuwa akipitia maisha yale huku mwanaume ambaye alisababisha kuwa hivyo hakuwa na habari naye na inawezekana hakuwa akifikiria kama alikuwa hai hapo kabla.
Alilowa hivyo hata machozi yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwake hayakuonekana. Alimkumbatia Malaika, alimuonea huruma, alikuwa mtoto mdogo ambaye hakutakiwa kabisa kupitia katika maisha aliyokuwa akipitia.

Ni kama Malaika hakuwa na baba kwani kila kitu alichokuwa akikifanya, alikifanya peke yake, yeye ndiye aliyekuwa kila kitu katika maisha ya mtoto huyo ambaye kwa kumwangalia tu ilikuwa ni rahisi kusema kwamba alikuwa akiumwa utapiamlo.

“Malaika mtoto wangu! Umemuona baba yako alivyoondoka? Hakujali, hataki kusikia chochote kuhusu wewe. Unapata tabu, angalia unavyonyeshewa na mvua, angalia jinsi mama yako ninavyoumwa kansa. Najua una njaa ila siwezi kukunyonyesha kutokana na ugonjwa ninaoumwa, jitahidi kunywa uji, ukishindwa hata juisi nitakununulia,” alisema Sarafina huku akimwangalia mtoto wake, ni kama alikuwa akisikia, naye alikuwa kimya akimwangalia mama yake.

“Mama yako ninateseka. Nilipanga mtoto wangu wa kwanza akasome shule za gharama, awe na kila kitu na baadaye aje kuwa rais wa nchi hii lakini kitu cha ajabu kabisa, nimekuwa ombaomba, hakuna shule tena, hakuna urais tena. Malaika, si mimi, katika maisha yako usinilaumu, ninafanya kila kitu kama mama, nipo tayari hata kufa ili uendelee kuishi, sitokuacha, utakapolia, nitalia, utakapohuzunika, nitahuzunika, utakapokufa, na mimi sitoona umuhimu wa kuishi,” alisema sarafina huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 47...

Maisha hayakubadilika, kila siku aliendelea kupata tabu zaidi na zaidi. Malaika akafikisha umri wa mwaka mmoja, hakuwa na afya njema lakini kila siku sarafina alipambana kwa ajili ya mtoto wake huyo.

Alikuwa na miaka ishirini na nne lakini muonekano wake ilikuwa ni rahisi kujua kwamba alikuwa na miaka arobaini na tatu, alizeeka, maziwa yake yalilala na kuisha kabisa, alikonda kiasi kwamba wengi wakahisi kuwa mwanamke huyo alikuwa akiumwa kifua kikuu.

Kutokana na kuzunguka kila kona jijini Dar es Salaam, Sarafina akalijua jiji, alijua mitaa yote, alijua sehemu ambazo zilikuwa na watu wenye pesa nyingi, kidogo na hata wale ambao hawakuwa na pesa za kutosha.

Kulala kwake kuliendelea kuwa kwa tabu sana, hakujali, hakutaka kuona akifa na kumuacha mtoto wake akiwa mdogo namna ile. Siku zilikatika na kukatika, alipigia kwa kiasi kikubwa na Malaika alipofikisha umri wa miaka mitano ndipo matatizo yakaanza kuonekana kwa Sarafina.

Kansa ya maziwa aliyokuwa akiumwa ikaanza kumletea madhara, akakonda zaidi, akawa mtu wa kukohoa kila wakati, maziwa yake yakaanza kutoa vidonda na alipokuwa akijaribu kuyakamua, yalitoa damu.

Alilia sana, usiku hakulala, alikuwa kwenye maumivu makali mno. Mtoto wake, Sarafina ndiye aliyekuwa akizunguka mitaani, ndiye aliyekuwa akimsaidia mama yake kuomba pesa kwa watu waliokuwa nazo.

Hakuwahi kujua elimu, hakuwahi kujua kama kulikuwa na maisha mazuri, alikulia mitaani na maisha yake yalikuwa mitaani tu. Wakati mwingine alipokuwa akienda kuomba mitaani na kupata pesa, watoto wenzake walimpiga na kumpokonya, wakati mwingine walimtishia kumuua kama tu asingewapa pesa walizokuwa wakizihitaji.

Alikua, aliutambua umuhimu wa mama yake, kwake, mwanamke huyo alikuwa kila kitu, ndiye aliyemlea, alijua kwamba alikuwa masikini, mama yake hakujiweza kutokana na kuumwa sana hivyo hata mitaani alipokuwa, aliomba pesa kwa nguvu huku picha ya mama yake akiwa mgonjwa, amelala chini ikimjia.
“Mama yangu anaumwa!” alisema Malaika.
“Anaumwa nini?”

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 48...

“Anatoka damu kwenye maziwa na ametoka vidonda. Naomba unisaidie hela ya kula, nataka nikamlishe mama!” alisema Malaika, alikuwa katika kioo cha mlango wa gari, alikuwa akiongea na mwanaume aliyekuwa ndani ya gari hilo.

Walimuonea huruma, aliongea huku machozi yalimtoka. Hakutaka pesa kwa ajili ya kutumia yeye mwenyewe, alihitaji pesa kwa ajili ya kumnunulia mama yake ambaye hakuwa akijiweza, alipokuwa akilala, hakuwa akiamka mpaka usiku.

Aliendelea kukusanya pesa na alipofika mahali ambapo mama yake alipokuwepo, alimpikia chakula kwenye vyombo vichafu na kuanza kula.
Malaika alikuwa mtoto mrembo, alichukua uzuri wa mama yake lakini ilikuwa ni vigumu kuuona uzuri wake kutokana na maisha magumu, yenye dhiki aliyokuwa akiyapitia na mama yake.

Alilia, kila alipokuwa akimwangalia, alijua kabisa kwamba alikuwa akienda kufa kitu kilichokuwa kikimletea majonzi makubwa moyoni mwake. Hakuacha kumuuliza kuhusu baba yake, kila siku alimuuliza lakini mama yake hakujibu zaidi ya kulia.
“Yupo wapi?” aliuliza Malaika.
“Alikufa!”
“Alikufa?”
“Ndiyo!”

Alitamani kumuona baba yake, alipoambiwa kwamba alikufa, moyo wake ulimuuma sana. Alilia kila siku, kila alipokuwa akimwangalia mama yake, alimuona akiwa mpweke na kitu ambacho alikiona ni kuwa alikuwa na mawazo ya kumfikiria marehemu baba yake.

Alitamani kusoma lakini hakujua angeanzia wapi. Hakujua kusoma wala kuandika, kitu pekee alichokijua maishani mwake ni kuamka asubuhi, kwenda barabarani kuomba na mchana kurudi nyumbani.

Hali ya Sarafina iliendelea kuwa mbaya, kila siku kwake yalikuwa mateso makubwa, alilia kwa maumivu makali na wakati mwingine alimuomba Mungu afe tu kwani kama kumlea Sarafina, alikuwa amekua kidogo kiasi kwamba angeweza kuyaendesha maisha yake kwa kuombaomba mitaani kama alivyokuwa akifanya.

Mitaani huko hakukuwa salama, kila mtu alimtamani Sarafina, alikuwa msichana mdogo mno, ila alipofikisha miaka sita na kifua chake kuanza kujaa, wanaume wakatokea kumtamani na kila mmoja akataka yeye awe wa kwanza.
“Ila kanavutia haka katoto!” alisema jamaa mmoja, alikuwa muuza mitumba wa Keko.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 49...

“Kweli kabisa. Kile kifua ukikipata, unakishikilia vilivyo! Ngoja tutumie hela tumpate, tukianza naye mdogomdogo, mwisho wa siku tunamvuta magetoni na tunapiga wote wawili! Au unaogopa?” aliuliza jamaa huyo.

“Wala siogopi. Ila mimi niwe wa kwanza!”
“Haina noma.”
Malaika hakujua kama wanaume walikuwa wakimvizia, kila siku aliamini kwamba watu wote walikuwa wakiwaonea huruma watu wa mitaani, hakujua kama kulikuwa na wanaume wengine walikuwa wakimtamani kwa sababu tu kifua chake kilianza kujaa.

Wanaume hao wakajifanya kama marafiki zake, kila siku alipokuwa akienda maeneo ya Keko kuomba pesa, walimgawia kiasi kikubwa kwake cha shilingi elfu mbili pasipo kujua kama wanaume hao walikuwa na malengo yao vichwani.

Alifurahia, alimwambia mama yake bahati aliyokuwa akiipata kila siku. Sarafina alikuwa na machale, alijua kabisa kwamba hao hawakuwa watu wazuri, alimzuia Malaika kwenda huko lakini hakusikia, hakuwa tayari kuziacha pesa hizo.

“Mungu naomba umlinde mtoto wangu. Ningekuwa na nguvu ningekwenda hukohuko. Ninashindwa hata kutembea, ninaoza huku nikijiona, Mungu! Naomba umlinde mtoto wangu,” alisema Sarafina huku akiwa amelala.

Maziwa yake yalioza kabisa, yalikuwa yakitoa harufu mbaya, kansa ilimtafuna kwa kiasi kikubwa, aliteseka mno na kila siku alimuomba Mungu amuue lakini kifo hakikumsogelea hata kidogo.

**** Ilikuwa ni hatari kwa Malaika lakini hakutaka kuacha, akatokea kuwazoea wanaume ambao kila siku alipokuwa akienda walimpa shilingi elfu mbili kiasi ambacho kwake kilionekana kuwa kikubwa mno.

Binti huyo mdogo alipokuwa akifika kijiweni kwao, walikuwa wakizungumza naye, walijenga mazoea lakini vichwa vyao vilikuwa vikifikiria kumbaka tu kwani pamoja na uzuri wake, kifua chake kiliwatamanisha mno na kuona kwamba kumuacha lilikuwa kosa la jinai.

“Leo umependeza,” alisema jamaa mmoja huku akimwangalia Malaika aliyekuwa akitabasamu.
“Ahsante!”

“Baadaye njoo uchukue hela nyingine, umesikia mtoto mzuri?” alisema jamaa huyo.
“Sawa. Nitakuja kaka!” Itaendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom