Niaje wakuu, Nimetumia A50 4gb/128gb kwa takribani wiki ya tatu sasa. Nilinunua kenya.
Mazuri
1. Design nzuri
2. Kioo cha kisasa cha super amoled
3. Ina mambo mengi kama flagship brands ukizingatia bei yake. Kiufupi samsung linapokuja ishu ya software wako vizuri sana
4. inachaji kwa haraka sana. ndani ya dk 40-45 inakuwa imejaa
5. Storage kubwa ya 128gb
Mapungufu
1. Haikai sana chaji hasa ukiwa unatumia internet(light browsing mf twitter, whatsapp, ). Inashangaza ukizangatia ina battery kubwa ya 4000mah
2. Iko very delicate sana hasa kioo, inahitaji uangalifu mkubwa sana
3. Ubora wa camera uko chini sana. ila watu wengi wanashauri kuinstall GCAM ila sijaribu
Kwa mtumiaji wa simu ya kawaida ni sawa, ila ukiondoa swala la battery na camera ni simu nzuri sana kulingana na bei yake