PostGE2025 Samia anasema wapiga kura wa CHADEMA walimpigia yeye

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sikusikiliza hotuba nzima ya jana kwa hiyo kila ninapopata vipande vipya napata mshangao mpya.

Katika hotuba yake ya jana, Samia aliwakosoa watu wanaoshangaa na wanaosema 98% alizopata hawezi kuwa amezipata kwa sababu mwitikio wa wapiga kura ulikuwa mdogo sana. Akasema 98% ni ya kura zilizopigwa.

Kuna mfululizo wa sentensi alioutoa katika hoja hii, moja ni kweli ila zilizofuata mmmmh...embu tupitie hoja moja baada ya nyingine.

1. Alisema 98% alizopata si za wapiga kura wote waliojiandikisha bali ni za kura zote zilizopigwa. Embu tuchukulie labda hii ni kweli maana wachache waliopiga kura wengi ni CCM. Kwa hiyo hata kama kura zilizopigwa nchi nzima ni 2300, 98% walimpa Samia. Embu tumpe hii point ingawa Tume wakazingua kwa kutuambia actually zimepigwa kura milioni 31. Tuendelee....

2. Alisema alishinda kwa kishindo kwa kuwa hakuwa na wapinzani imara na akawataja kabisa kwamba CHADEMA na ACT hawakuwepo ulingoni. Kitendo cha kukiri hivi kilinishangaza sana maana yeye anahusishwa moja kwa moja na kutokuwepo kwao katika uchaguzi. Hapa IQ inahusika.

3. Alisema wapiga kura walipiga kura asubuhi na hao walioanzisha vibe lao la maandamano saa 5 walikuta kura zimeshapigwa. Mmmhhh. Ukiacha vituo kuwa vitupu ila kuna idadi ya kutosha ya vituo vilivyoharibiwa na kura kutupwa na kuchomwa moto. Hesabu za Tume ya Uchaguzi zinaanza kuharibika.

4. Akamaliza hoja yake kwa kusema kuwa kwa sababu wapinzani wake wakubwa hawakuwepo katika uchaguzi, basi wapiga kura ambao labda wangewapigia wapinzani kina Lissu wamempigia yeye. Nilivyosikia vile nikajisemea ile video inabidi niihakiki, inaweza kuwa ni AI.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kwa takwimu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi, Samia alishinda kwa 84.8% ya kura zote kama wapiga kura wote waliojiandikisha wangepiga kura. Hii asilimia bado ni kubwa sana kwa mwitikio ule tuliouona. Hii figure ndiyo inakosa kabisa uhalisia kuliko hata ile ya 98% ya kura zilizopigwa.

Mchana mwema.
Kama CHADEMA wanasafiri na SGR, ATC, wanatumia umeme wa bwawa la Nyerere, wanatembeza magari yao katika barabara alizojenga Samia n.k ninaamini hao wanachadema ndio waliomchagua Samia.
Ni kukweli usiopingika kuwa hata katika No Reforms no election... si wanachadema wote walikubaliana na hilo.
Swali: walitekelezaje dhamira yao binafsi wakifikiri nje ya box au maarufu kama "za kuambiwa changanya na za kwako".
 
Ubongo wa bata
 
Unawatania walionuna?
 
Sikusikiliza hotuba nzima ya jana kwa hiyo kila ninapopata vipande vipya napata mshangao mpya.

Katika hotuba yake ya jana, Samia aliwakosoa watu wanaoshangaa na wanaosema 98% alizopata hawezi kuwa amezipata kwa sababu mwitikio wa wapiga kura ulikuwa mdogo sana. Akasema 98% ni ya kura zilizopigwa.

Kuna mfululizo wa sentensi alioutoa katika hoja hii, moja ni kweli ila zilizofuata mmmmh...embu tupitie hoja moja baada ya nyingine.

1. Alisema 98% alizopata si za wapiga kura wote waliojiandikisha bali ni za kura zote zilizopigwa. Embu tuchukulie labda hii ni kweli maana wachache waliopiga kura wengi ni CCM. Kwa hiyo hata kama kura zilizopigwa nchi nzima ni 2300, 98% walimpa Samia. Embu tumpe hii point ingawa Tume wakazingua kwa kutuambia actually zimepigwa kura milioni 31. Tuendelee....

2. Alisema alishinda kwa kishindo kwa kuwa hakuwa na wapinzani imara na akawataja kabisa kwamba CHADEMA na ACT hawakuwepo ulingoni. Kitendo cha kukiri hivi kilinishangaza sana maana yeye anahusishwa moja kwa moja na kutokuwepo kwao katika uchaguzi. Hapa IQ inahusika.

3. Alisema wapiga kura walipiga kura asubuhi na hao walioanzisha vibe lao la maandamano saa 5 walikuta kura zimeshapigwa. Mmmhhh. Ukiacha vituo kuwa vitupu ila kuna idadi ya kutosha ya vituo vilivyoharibiwa na kura kutupwa na kuchomwa moto. Hesabu za Tume ya Uchaguzi zinaanza kuharibika.

4. Akamaliza hoja yake kwa kusema kuwa kwa sababu wapinzani wake wakubwa hawakuwepo katika uchaguzi, basi wapiga kura ambao labda wangewapigia wapinzani kina Lissu wamempigia yeye. Nilivyosikia vile nikajisemea ile video inabidi niihakiki, inaweza kuwa ni AI.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kwa takwimu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi, Samia alishinda kwa 84.8% ya kura zote kama wapiga kura wote waliojiandikisha wangepiga kura. Hii asilimia bado ni kubwa sana kwa mwitikio ule tuliouona na joto la kisiasa lililokuwepo nchini. Hii figure ndiyo inakosa kabisa uhalisia kuliko hata ile ya 98% ya kura zilizopigwa.

Mchana mwema.
Anasema wapinzani wa kweli hawakushiriki, wapinzani dhaifu ndio walishiriki, wafuasi wa wapinzani strong (CHADEMA & ACT) walimpigia kura kupata hiyo 97.66%. Sasa unajiuliza kwa nini alikuwa anasomba watu kwenye maroli kuwaleta mikutanoni kama alijua hakukuwa na upinzani? Mmh! Watanzania tulipigwa parefu sana
 
laZima katiba mpya ipatikane
Uchaguzi urudiwe
Tupate tume huru ya uchaguzi
Wauaji wafike ICC
Katiba mpya inapatikana.
Uchaguzi urudiwe...Mmm mtasubiri sana:FLUSH::FLUSH: ... uchaguzi ni 2030.
Tupate tume huru- Itakuwepo ndani ya katiba mpya- tiki
Wauaji wafike ICC- ICC si chombo cha kuiimarisha Afrika, ni chombo maslahi kwa ulaya.
 
Back
Top Bottom