Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Basi washaurini Wamarekani nao waseme Baraka Obama sio Mmarekani.

Hapa hivi tunabishana nini? Tafuteni makosa mengine ya Salva, lakini yeye ni Mtanzania.

Ni mtanzania kwa sheria gani? Nadhani ndilo lilikuwa swali. Obama ni Mmarekani kwa sheria za Marekani sasa kwanini watu waseme si Mmarekani. Uraia hauambukizwa kwa osmosis.
 
Basi washaurini Wamarekani nao waseme Baraka Obama sio Mmarekani.

Hapa hivi tunabishana nini? Tafuteni makosa mengine ya Salva, lakini yeye ni Mtanzania.

OBama sio Mkenya ni Mmarekani. Ukizaliwa Marekani automatically ni raia wa marekani hata kama wazazi wako wanaishi Marekani kimakosa. Obama kazaliwa Hawaii.

Mzazi wako mmoja akiwa Mmarekan una haki ya kuwa raia wa Marekani. Mama yake Obama ni Mmarekani.

Tupeni sheria za Tanzania za uraia na jinsi Salva anavyo-qualify (period).
 
Wakati mada hii ya uTanzania na mTanzania inaendelea tuanze na kuulizana nani mZanzibari na nani mTanganyika, halafu tuanze nani mHaya na nani mZaramo na nani mChaga na kadhalika, tukimaliza hapo tuanze kujua ni nani mwenye haki zaidi katika nchi hii, MHaya, Mzaramo, Mkara, Mhutu, ..., halafu tukikosa jibu tutafute mapanga tuanze kuuwana, ataebaki ndio mwenye haki, si ndio maana ya kuanzisha mada kama hii?

Ndio hayo, mwenye kuelewa maana atajuwa kabisa nakusudia nini.
 
Ndio hayo, mwenye kuelewa maana atajuwa kabisa nakusudia nini.

wakati mwingine mtu anaweza kusema kitu akadhania amemaanisha kitu kumbe kile alichosema na kile alichomaanisha ni vitu viwili tofauti. Hivyo ni jukumu la mtu yule kumaaminisha anachosema na kusema anachomaanisha; vinginevyo watu wengine wasiojua alichomaanisha watasema kamaanisha asichosema.
 
Lets assume he is NOT Tanzanian by birth or whatever definition but one thing appears to me to be clear, he loves and is proud of being Tanzanian. If that is true then questioning his nationality for me is, as Mwalimu put it, "primitive nonsense". Baadhi yenu hapa mnamwona Jeetu Patel, Manji na Rostam watanzania zaidi eti kwa vile tu walizaliwa hapa au kupata uraia! Hii thread kweli sasa imeingiliwa!
 
Sasa kuna shida gani ya kusema background yako ukiwa unaipenda Tanzania.
 
wakati mwingine mtu anaweza kusema kitu akadhania amemaanisha kitu kumbe kile alichosema na kile alichomaanisha ni vitu viwili tofauti. Hivyo ni jukumu la mtu yule kumaaminisha anachosema na kusema anachomaanisha; vinginevyo watu wengine wasiojua alichomaanisha watasema kamaanisha asichosema.

Ndio maana mwenye kujuwa maana haambiwi maaana na asiyejuwa maana hata ukimwambia maana bado atakuwa hana maana kwa sababu hajui maana na ukizidi kumfunda maana kwa kuwa hajui maana anakuwa hana maana wala haelewi maana kwa hiyo haina maana kumjulisha maana inabidi umwache abaki bila maana kwa kuwa hana maana.
 
kuna maana gani katika ulichoandika hapa sasa! grrrrrrr
 
Ndio maana mwenye kujuwa maana haambiwi maaana na asiyejuwa maana hata ukimwambia maana bado atakuwa hana maana kwa sababu hajui maana na ukizidi kumfunda maana kwa kuwa hajui maana anakuwa hana maana wala haelewi maana kwa hiyo haina maana kumjulisha maana inabidi umwache abaki bila maana kwa kuwa hana maana.

Nimeikubali hii tamathali ya semi!!
 
hivi wewe unawajua hawa watu au unawasikia? si lengo langu kuwa mbaguzi lakini mie nimeishi nao i know them, mzazi wangu mmoja anatoka huko, wako troubled psychologicaly, wataleta matatizo sana ukiamua waunganishwe na tanzania.

Jamani jamani mama wa paroko, unakoenda siko. Hata akina Hitler na Musolin walianza hivi hivi! Jamani hizi chuki dhidi ya watusi sijui wahutu..zisitufikishe huku! Anyway the jury is still out.!

lakini jamani kwa nini kuna chuki sana dhidi ya watusi? hivi mnajua hakuna aliyechagua sura wala kabila? sasa mtu kama anatoka Kigoma, Ngara au Karagwe. anajina la kiburundi au kirwanda..anakuwa branded mtusi! Jamani tunakoenda ni kwingine. Hii mtu kazaliwa wapi...jamani wengine tumezaliwa vijijini, baba hakusoma, mama hakusoma..zahanati ni moja wilaya nzima!! and on and on.... hata Clinic wengine hatukwenda! sasa leo mnatudai vyeti vya kuzaliwa...haki ya nani..ukistaajabu ya Musa....Tutashikana masharti...

Mi personally mpaka leo natumia hati ya mahakama ya mwanzo...maana, Hicho cheti ningekipata wapi?..Anyway tuendelee kukataa issue..ipo siku kitaeleweka...
 
Watu wa mipakani wana mahusiano mwakubwa Sana.lugha..tamaduni, muingiliano wa Familia.. angalia nchi nyingi hali ndio ilivyo,ila muhimu kuwa na Taratibu au sheria zinazotambulika. Hivi Wamasai wa Kenya na Wamasai wa Tanzania utawatofautisha Vipi? Hivi wasegeju wa Kenya na wa Tanzania utawatofautisha Vipi?
Ndugu Chuma,
Tofauti ya Mmasai Msegeju Mujaluo nk. wa Kenya na Tanzania ipo penye vitambulisho vya uraia. Of course hao jirani zetu wakiingia Tanzania ni kama wanaingia bila hodi, kwani hata chooni inabidi kupiga hodi. Mjaluo/ Mmasai nk wa Tanzania hawezi kuingia Kenya akaishi na akapata nafasi na haki zote kama Mkenya. Nilikuwa Nairobi penye Kongamano la kidini miaka kadhaa iliyopita, wakati wa mapumziko ya mchana, nilitembea hatua chache toka ukumbini, nikiwa na makabrasha husika na name-tag kifuani pangu iliyoonyesha uhalali wa uwepo kwangu pale, bado, polisi walitokea na kuniuliza KIPANDE CHANGUtena kwa ukali kama vile nimetenda kosa.
Tunataka Vitambulisho vya Uraia. Hii haipaswi kutumia mamillioni/mabilioni ya pesa kama inavyoonekana. Hata ktk baadhi ya nchi zilizo endelea bado wanatumia vitambulisho vya kawaida na hasa kwa wazawa. Cha muhimu nikuweka viongozi waadilifu kusimamia hili. Kwa nini sisi tunaongelea kutumia modern technology ambazo hatutaweza kuzimudu! Serikali ingeweza kuomba ushauri kwa raia wema kuliko kuanza kutangaza tenda za watengenezaji vitambulisho. Modern technology siyo jibu bali uadilifu, mpaka sasa ni ngumu kwa Mtz wa kawaida kupata pasi kuliko mgeni asiye raia licha ya kuintroduce hizi pasi za kisasa. Sina uhakika na hili, lakini nilisikia tayari pana foggery penye hizi pasi mpya. Hivi watawala wetu wanajua ni kwa lini na mazingira gani yanayoambatana na utumiaji wa electronic cards. Hivi Tanzania tumefikia hatua hiyo. Haya mambo hata penye nchi zilizoendelea wenye umeme wa uhakika angalau kwa 99% bado wanaexperience matatizo, itakuwa sisi? Twendeni hatua kwa hatua. maana naona ni kama kusema elimu ya IT ifike vijijini wakati hao wanafunzi hata penseli hawamudu kukunua. Tupeni wananchi nafasi tutoe ushauri/maoni yao.
 
Ushauri wa bure kwa Moderators:
kuweni makini sana na aina za mijadala, mjadala huu ukiendelea mwisho wake si mzuri utainua hisia NDIZO AMBAZO SIZO wasiwangu ni kutugawa jamani!! mi naogopa kwani mke wangu ni Mkurya wa mpakani sina hakina kama wametokea Musoma kweli, kesho mkisema tuwafukuze si nitabaki mkiwa!!!
 
Hii tabia ya kubaguana ni mbaya sana...tuikemee; naona kama vile kuna watu wameishaanza "kula nyama za watu", tusipoangalia wataendelea kula tu na siku moja itakuwa zamu yetu kuliwa. Kwa mfano mimi nafikiri tufike mahali tuamue kama Taifa kwamba wale wote walio Waafrika na wapo Tanzania na wanaipenda Tanzania (vigezo viwekwe), wapewe tu urai, wananchi wote wawe na vitambulisho na huu ubishi uishe.
 
Nego:

Nadhani kuna vitu vinapindishwa hapa. Wengi tulio hapa sio wabaguzi kwa sababu tunaheshimu watu wa rangi nyingine, dini nyingine na makabila mengine.

Baada ya kusema hayo, ni lazima tukubali kuwe wengi wetu tunaona kuwa njia ya kuliongoza taifa letu na jamii yetu ni misingi ya sheria.

Miaka iliyopita tulikubali Azimio la Arusha, la Zanzibar na mengine kuongoza nchi. Vilevile tulikubali siasa kuwa ndio mtindo wa maisha ya kila siku.

Tunaona hasara inayotupata ni kubwa na kilichobaki ni kujenga taifa lenye kufuata misingi ya sheria. Na moja ya sheria hizo ni sheria za uraia. Hivyo basi Mchina, Mhindi, Mwarabu, Mzungu, Mrundi, mgogo, msukuma au Mjaluo anaetambulika kisheria ni Mtanzania na hatuna matatizo wala ubaguzi katika upande huo.

Lakini kama sheria ya nchi inasema kuwa wewe sio raia wa Tanzania basi wewe sio raia wa Tanzania hata kama ulisoma na kufanya kazi Tanzania au kabila lako liko katikati ya Tanzania (Mluguru au Mgogo). Huo sio ubaguzi ni misingi ya kisheria.
 
Hili siyo suala la ukabila na ni wenye ubaguzi wa Kikabila wanajulikana. Ukiangalia post yangu ya mwanzo kabisa na zote zinazofuata hakuna hoja ya Kikabila upande wangu, kwani mimi napinga ukabila katika hali zake zote.

Hoja iliyopo ni ya kiraia. Je kutokana na udugu na umoja wa nchi zetu na jinsi ambavyo tumeingiliana na nchi jirani kutokana na mipaka mibovu tuliyoirithi je tuamue kufuta uraia. Kwamba hakuna raia wa Tanzania na sisi sote ni watu wa moja tu alimradi tunaishi karibu karibu. Hivyo mtu toka Malawi, Zambia, n.k aingie Tanzania na kufanya kazi yoyote hata kama tunajua kuwa ni mtu kutoka sehemu hizo? Je tufute Uraia wa Tanzania na tuingize uraia wa Afrika?
 
Nimepata habari ana matatizo makubwa kwney ndoa yake sijui kama ni kweli au la
 
Back
Top Bottom