Salma Kikwete na WAMA vipi?

PM itakuwa vema ukiweka ushahidi pia....!!!

Mkuu nahisi wewe utakuwa mmoja wa wanafamilia wa kifisadi fisadi kwa maana una crash kitu kinacho eleweka hapa......ukweli si huo WAMA Singida wameenda?WAMA Sumbawanga wameenda?Au huko hakuna wanawake?
 
jamani hata mama bush nae ana ngo

mama mkapa alikuwa nayo


?????????????? mama salma jamani???????????mbona hivyo huyu mama mkapa ameiba na kula vingi hamkuonge ije swala la lindi kelele!!!!!!!!mbona mama mkapa hakupeleka moshi na hamkuuliza yyyyyyyy anatumia dar na sehemu nyingine nasi nyumbani kwake


sijui ncheme ??????

Tunajua Mama Mkapa alikuwa na EOTF (Equal Opportunity Trust Fund). Hatujui usajili wake ulisemaje, je ulisema ni NGO ya mke wa Rais au ilisajiliwa kama NGO zingine?

Mama Salma Kikwete, yeye amesajili NGO yake WAMA (Wanawake na Maendeleo). Hatuna uhakika kama imesajiliwa kama NGO ya mke wa Rais au la?

Ma-First Lady Kama Mama Maria Nyerere, Sitti na Khadija Mwinyi hatukusikia kama walikuwa na NGO, japo walijishughulisha na masuala ya kijamii kama wake za Marais.

Ninachohitaji kujua kama from legal point of view kama ni makosa kwa wake wa Rais kuwa na NGO na kama wakiwa nazo zisajiliwe kama NGO za mke wa rais au kama NGO zingine za kawaida?

Mimi binafsi ninaunga mkono jitihada zozote zinazofanywa katika juhudi za kumkomboa mwananchi wa kawaida husan wanawake. Vilevile ninaelewa hali duni zinazowakabili wanawake wa mikoa ya Lindi na Mtwara na hata mikoa mingine. Sasa anapotokea mtu akaja na ajenda ya kutatua matatizo ya akina mama wa Lindi tunahoji kana kwamba Lindi haistahili. Sijasoma ripoti ya mwaka ya WAMA lakini nadiriki kusema kuwa kama kuna manufaa ambayo yamepatikana basi nina amini yalikwenda across the board kwa maana yalikwenda kwa wengi wa wanawake wahitaji.
 
philemon mikael,lunyungu,pundamilia,fidel08,

..mwacheni Mama apeleke maendeleo Lindi,Pwani,Mtwara, na mikoa mingine ya "pembezoni."

..wakati wa uraisi wa Mkapa ilikuwa ni aibu kubwa kwani jimbo alilozaliwa ndiyo lilikuwa linaongoza kwa kutia mimba watoto wa shule, pamoja na utoro.

..pia sijui kama mliona picha za mashule ktk jimbo la Raisi Kikwete wakati wa kampeni za Uraisi. kwa kweli ilikuwa ni aibu ya kutisha ukizingatia kwamba Kikwete alikuwa waziri kwa miaka zaidi ya 15 kabla ya hapo.

..mimi usongo wangu uko kwa wale wanaochota Tanzania na kupeleka nje.

..kwa Mama Salma yeye aendelee kuchota huko nje na kupeleka Mtwara na Lindi. ndoto yangu ni kesho na keshokutwa vigogo waanze kusomesha watoto wa Lindi na Mtwara, siyo Mbeya na Kilimanjaro tu.
 
Mkuu nahisi wewe utakuwa mmoja wa wanafamilia wa kifisadi fisadi kwa maana una crash kitu kinacho eleweka hapa......ukweli si huo WAMA Singida wameenda?WAMA Sumbawanga wameenda?Au huko hakuna wanawake?

kaka nafikiri Mjadala uliuvamia...Hukujua nimehitaji ushahidi ktk jambo gani...

Kukujulisha kuwa Philimone Michael amesema Bi. Salma Mke wa JK kuwa amepewa msaada wa $10 Millions(zaid ya Billion 10 in TZS)...tumemuomba ushahidi hadi sasa hajaleta. kaja kubwabwaja tu tena. Mtu mzima lkn Uongo kauweka Mbele...

Philimone..Nakuunga mkono kwa Hoja ya kuwa Hizi NGO za wake za Marais ziwe audited in the sense wanapata fedha kwa mgongo wa Rais..si vibaya.Nafikiri watu wa kuwabana ni Taasisis inayosajili hizi NGO. Nafikiri Kila NGO inatakiwa ku-submit mapato na matumizi yake kwa kadri taratibu za msajili wa NGO zilivyo....Hii isiwe tu kwa taasis za WAMA bali pia na the so called taasis za Ukimwi na nyinginezo ambapo viongozi wake baada ya kupewa pesa 80-90% ya Pesa wanazopewa zinaishia ktk administration wakati 10-20% inawafikia walengwa!!!
 
20080829-4_p082908sc-0099-515h.jpg

Bush.jpg
 
Mkulu Lunyungu huwa una chemsa big time, kabla hujakurupa na kupost allegations nzito kama hizi uwe unafanya ka homework kadogo basi...
 
Lunyungu uliwahi kuja na issue ya Dr. Dau kujenga Msikiti Dodoma...Hadi leo umeshindwa kuthibitisha uzushi wako!!

Ukaja hapa kwa NickName ingine kumshambulia Mh. Batilda kuhusu Mhudumu wake...madai ya Uzushi..

Leo umekuja na hili....it seems umekuwa dedicated kuwachafua waheshimiwa in the sense ya mfumo wa maisha wao...!!!

Take care ur being watched


Chuma shalom
Mkuu Chuma mimi si mbabaishaji kama unavyotaka watu wanielewe.Mie nikiibua issue inakuwa issue sana.Chuma kaangalie tena issue ya Batilda sikuilketa mimi .Mimi nilichangia kama wengine na ushahidi wa jambo lile ni mwingi sana na yeye wala wewe hujawahi kukanusha jwa niaba yake .

Swala la Salma liko wazi na tafadhali soma michango ya wana forum wengine ndipi utajua ninacho kisema wacha kuja na historia ya ajabu kukwepa hoja .Unaweza kukaa kimya kama hoja ni nzito .
 
Mkulu Lunyungu huwa una chemsa big time, kabla hujakurupa na kupost allegations nzito kama hizi uwe unafanya ka homework kadogo basi...

Mkuu Masatu
Mimi sijaelewa unacho kibisha ni kitu gani hasa .Kuna watu wameleta hoja zao huko nyuma lakini hakuna anaye kataa kwaba kuna kiini machi katika WAMA.Kama wewe unaniita muongo na una facts tafadhali zimwage hapa uthibitishe ukweli wako na uongo wangu .Mimi nimesha fanya uchunguzi sana na tena wa kina ndiyo maana nimekuja kuleta hoja hii .Na tena naomba usome bandiko langu liko vipi .Sijatoa tuhuma kokote bali nimeweka maswali ambayo mimi ninayo na kuuliza kama kuna mwenye habari tofauti.Sasa unalialia nini ?
 
Chuma shalom
Mkuu Chuma mimi si mbabaishaji kama unavyotaka watu wanielewe.Mie nikiibua issue inakuwa issue sana.Chuma kaangalie tena issue ya Batilda sikuilketa mimi .Mimi nilichangia kama wengine na ushahidi wa jambo lile ni mwingi sana na yeye wala wewe hujawahi kukanusha jwa niaba yake .

Swala la Salma liko wazi na tafadhali soma michango ya wana forum wengine ndipi utajua ninacho kisema wacha kuja na historia ya ajabu kukwepa hoja .Unaweza kukaa kimya kama hoja ni nzito .

Lunyungu,

Msikiti alio jenga Dr Dau kwa pesa za NSSF Dodoma upo wapi? Huna haya unakanusha suala la Batilda nani asie jua kuwa Nakandamiza Kibara ndio wewe Lunyungu? acha zako hizo unafahamika kwa udini unachafua watu pasi na sababu yeyote
 
Lunyungu,

Msikiti alio jenga Dr Dau kwa pesa za NSSF Dodoma upo wapi? Huna haya unakanusha suala la Batilda nani asie jua kuwa Nakandamiza Kibara ndio wewe Lunyungu? acha zako hizo unafahamika kwa udini unachafua watu pasi na sababu yeyote

Siwezi kupoteza muda wangu kujadili yaliyo wazi .Kukanusha kwangun ni kupi juu ya msikiti ama jina lililo tumika ? Mie naomba nibakie kwenye issue .Mimi ni Lunyungu na majina mengine si issue kwangu .Narudia kusema issue ya WAMA mwenye maelezo ya kina atupe .Batilda sijaona uongo wake maana ni kweli si yeye tu na wamkubwa wengi serikalini wana waajiri wageni bila ya vibali .Kuna siri gani tena kwenye hili ?

Msikiti nadhani rudia usome bandiko la wakati huo na comments zangu.Kwa sasa issue ni WAMA na Salma .
 
kama itaruhusiwa waume wa marais (endapo rais akiwa mwanamke) waje na NGO zao
but this is bullshit. why cant they open a common office for first ladies? they are using goverment infrastructure as well as taxes we pay to run private firms, I believe if western will know this, they will say poor tanzanians....
Only suggestions
 
...Teh! teh!! Charity au ufisadi????

Huu ni Ufisadi in kind .Maana ni daraja la kuwapa mahela ya kuishi hadi wafe kwa kiinimacho cha WAMA nk .Ndiyo maana nimekuja hapa na kuuliza je kuna jambo gani hapa Salma hajafika Tarime na WAMA ama Magu au Ukerewe kila siku ni Lindi tu ?
 
Na Mwandishi wa HabariTanzania.com,
Tarehe 26 Oktoba, katika gazeti mojawapo litolewalo kila siku, tulisoma habari iliyotutia wasi wasi na mshawasha kutaka kujua kulikoni. Habari hii ilihusu uzinduzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali liitwalo Wanawake na Maendeleo (WAMA), ambayo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, imeanzishwa na Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

Si vibaya kuanzisha NGO kama zilivyozoeleka hapo nyumbani. Lakini kwanini aanzishe baada ya mumewe kuwa Rais ? Je hapa kunani? Kwanini sasa? Je huu nao ni mtindo mpya wa mke wa mtawala naye kuwa mtawala ?

Kwa kumbukumbu 'mchezo' huu ulianzishwa na mke wa Rais aliyewahi kuwepo madaraka yake. Bila kumung’unya maneno, Ngo ya Mama Ben iliyojulikana kama Ulaji Sawa kwa Wetu, ilikuwa mali binafsi ya mama huyo kiasi cha kuzua manung’uniko juu ya utendaji wake. Kwa mfano iliwahi kubainika kuwa misaada mingi iliyokuwa ikitolewa kwa Taasisi hiyo,ilikuwa ikitumika kwa upendeleo.

Iliwanufaisha sana wananchi wa maeneo ama alikotoka mwenye ‘mradi’,mumewe au mashoga zake au wale waliotaka kuitumia kisiasa lakini naye akanufaika kwa njia moja au nyingine. Katika hali hii ikawa vigumu kumtofautisha mke wa Rais (First Lady) na mfanya biashara wa kawaida wa kike (Businesswoman). Ilifikia mahali ikawa vigumu kutofautisha kati ya msaada kwa mhusika au rushwa.

Hili siyo siri. Atakayekuwa na shaka aombe mahakama itoe kibali tukague jumla ya pesa na miradi vilivyotolewa. Utauona ukweli mweupe japo wa kuchukiza. Ndiyo. Kwani mara ngapi tumehoji kwanini wahusika walitangaza mali zao wakati wa kuingia madarakani na kuondoka bila kuzitaja ili tuone kama walikuwa waadilifu ?

Kwa mara nyingine tunawapa shime wafanye hivyo ili waache kuandamwa na jinamizi la shutuma za rushwa na wizi. Wakiendelea kula jiwe tutajiridhisha bila shaka kabisa kuwa walituibia wakati wakiwa madarakani.

Kitu kingine ni kwamba taasisi za namna hii kwa kuzingatia uzito wa wamiliki,zinatia ushawishi wa rushwa kwenda kwa mkuu wa nchi. Kwani wanaotoa misaada kwenye taasisi hizo wengi wao ni watu wa kutia mashaka na wanafanya hivyo kwa vile Bi Mkubwa anaweza kuongea na Mzee wakati wowote.

Je hapa usalama wa nchi haujatiwa msambweni !

Nani mara hii kasahau jinsi ukaribu wa Mama Awamu ya pili ulivyotaka kumuyumbisha mumewe pale ilipogundulika kuwa wajanja walikuwa wakimtumia,japo hakuwa na NGO, kujipatia mikopo na viwanja ? Nani kasahau kashfa zilizojitokeza ilipofikia hata kijana mmoja wa kihindi kudiriki kumuita shemeji ?

Nani huyo kasahu Mwalimu alipoutolea uvivu mchezo huu kwa kutahadharisha kuwa Ikulu ni sehemu takatifu ? Sawa na Yesu alivyowatimua wabadilisha pesa kwenye hekalu la baba yake,Nyerere aliuliza Ikulu kuna biashara gani ? Jamani msiturudishe huko.

Licha ya hilo, Mwalimu alituachia hekima moja juu ya shutuma dhidi ya mke wa Kaisari. Unajua alisemaje ? Achilia mbali kuzini, hata kushutumiwa tu kunatosha kumtia matatani mke wa Kaisari. Au nanyi mnaingia na awamu ya nne ambayo inaweza kuwa awamu ya pili ya RUKSA ?

Tueleze tujue chonde chonde mama. Maana hadi tunaandika, ukiondoa serikali ya awamu ya kwanza, awamu zilizofuata na ya mumeo ikiwemo zinatawala bila falsafa zaidi ya kauli mbinu ! Hapa ndipo mvua inapoanza kutunyeshea kiasi cha kila mlaji kula anavyojua na kiasi anachotaka. Katika mchezo huu wote wanaoumia ni wananchi.

Nani mara hii kasahau kuwa Bi Mkubwa aliyepita aliondoka serikalini bila kujibu maswali mengi ambayo yalitokana na shutuma zilizo mhusisha na upatikanaji wa pesa na biashara ambao kwa vigezo vyote una walakini ?

Kwa kuangalia kwa haraka ‘uchafu’ na mashaka yanayozunguka ngo za wake wa wakubwa,kuna haja ya kumwambia mama Salma kuwa maji anayotaka kuyaingia yaliishajaa ruba.

Si hilo tu. Kama Rais Jakaya atataka watu waendelee kumpenda na kumuamini,inabidi achukue mfano wa Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Hakuruhusu mkewe awe mfanya biashara hata kwa sekunde tano.

Kwani hakujua uchafu na ushawishi unaoandamana na madaraka hasa mhusika anapojiingiza kwenye upatu uitwao biashara ? Aliepusha madhara yatokanayo na hali hii ambapo ni mke wa Kaisari kuanza kushukiwa na kushutumiwa. Na isitoshe wananchi walimchague yeye tu, na siyo mkewe na mashoga zake.

Hatuna nia mbaya na mama Kikwete. Lakini tukizingatia kuwa historia ni mwalimu mzuri, hakuna haja ya serikali ya sasa kufanya kile waingereza waitacho ‘monkey see monkey do’

Tutajuaje kuwa, kama waliomtangulia,ufanyabiashara wake hautayatia matatani madaraka na sifa za mumewe? Tutajuaje kama wajanja hawatamchangia ili baadaye wapate upendeleo fulani kama ilivyotokea kwa waliomtangulia? Tutajuaje kama lengo lake ni kujitajirisha kama waliopiata? Tutajuaje kama ana nia nzuri?

Je muda wa kumhudumia mumewe utapatikana wapi iwapo kila saa atakuwa kwenye biashara zake kama sinema iliyopita juzi juzi ambapo hata umbea mwingi ulianza kusikika kuhoji juu ya kuwepo kwa ndoa au la kati ya walopituka hao wawili!

Tutoe hoja, mama Salma, huu ni ujumbe wako. Chonde chonde achana na ufanya biashara na usasi wa ngawira umhudumie mzee ambaye mzigo unaendelea kumlemea. Ungejua kuwa watu hata wanahoji mantiki ya kuwemo wanenu kwenye ujumbe uliokwenda New-York, nadhani kama hujui sasa utajua na kuachana na biashara ya ubuyu. Kama kuna haja ya kujali maendeleo ya kina mama, tunadhani wizara ya wanawake na watoto ndiyo kazi yake. Lakini siyo kazi ya mke wa Rais.
Chanzo: www.habaritanzania.com

Kwani hawa wake wa viongozi hawawezi kusaidia jamii nje ya migongo ya waume zao? Kuna ulazima wa wao kuanzisha NGOs za namna hii?
 
Nijuavyo mie ni kuwa hii WAM alianza kuiunda muda kidogo na ni mradi wake kwa kifupi km wa mama Mkapa na kikao kilikuwa kinafanyika Obay ile nyumba aliyokuwa anaishi yeye na mumewe baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM na kifupi kiingilio ilikuwa ni 50,000 kama ulikuwa unataka uanachama, but ni full mindugu ndani ya hiyo ofisi teh teh sasa sijui fukara km mie ilikuwaje maana niliogopa kiingilio chake duh balaa! Hongera yake na akimaliza uongozi mumewe na mwingine atakae ingia bas mkewe ataanzisha yake kaazi kweli kweli ila tutafika tu!
 
huu ni ufisadi mwingine ikulu, muda si mrefu tutasikia ya ANBEN, hawa wamama wanaushawishi mubwa sana kwa wazee wao, so tusubiri
 
mama first lady naomba basi uje na kwetu utuanzishie NGO tunakuhitaji sana sisi kina mama wa kisasa
 
Nijuavyo mie ni kuwa hii WAM alianza kuiunda muda kidogo na ni mradi wake kwa kifupi km wa mama Mkapa na kikao kilikuwa kinafanyika Obay ile nyumba aliyokuwa anaishi yeye na mumewe baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM na kifupi kiingilio ilikuwa ni 50,000 kama ulikuwa unataka uanachama, but ni full mindugu ndani ya hiyo ofisi teh teh sasa sijui fukara km mie ilikuwaje maana niliogopa kiingilio chake duh balaa! Hongera yake na akimaliza uongozi mumewe na mwingine atakae ingia bas mkewe ataanzisha yake kaazi kweli kweli ila tutafika tu!

maria Roza na wewe umetoa jingien kwa hiyo hapo ni full ukooo

binamu , bibi,babu ,mjomba ,nyanya yake ,shemeji akina yakhe tutapata kweli??

nipe Contact nidepost ka 50,000.00 lakini in 10years 2 come katazaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom