Mama Salma asimulia Kikwete alivyowateka mabinti!

mwanausangi

JF-Expert Member
Nov 4, 2021
548
608
Dar es Salaam. Miaka 72 ya kuzaliwa kwa Rais wa awamu ya nne (2005-2015), Jakaya Kikwete imekuwa na simulizi nyingi zinazogusa maisha yake, kubwa ni kutoka kwa mkewe, Mama Salma Kikwete.

Wawili hawa ambao wapo kwenye ndoa kwa miaka kadhaa, walikutana kwa mara ya kwanza Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi ambapo Salma alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu na Kikwete alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilayani humo.

Katika mahojiano yao na Clouds Media leo Alhamisi, Oktoba 7, 2022 nyumbani kwao, Msoga, mkoani Pwani ikiwa ni kusherekea siku ya kuzaliwa ya mme wake, Mama Salma amesema hakuwa akifahamiana na Kikwete kabla na kwa mara ya kwanza walikutana kwenye mkutano wa kuhamasisha siasa uliofanyika chuoni kwao.

“Mimi nilikuwa naimba kwenye kwaya, yeye amekuja kuhamasisha vijana masuala ya siasa kwa hiyo nilitimiza jukumu langu la kuimba na yeye akaweka siasa zake jukwaani shughuli ikaisha,” amesema.
“Basi walivyoondoka na kamati yake ya siasa na siye tukaendelea na shughuli zetu, tuliporudi bwenini mazungumzo ya wasichana wote yalikuwa ni kumhusu yeye (Kikwete) na muonekano wake akisifiwa kuwa mzuri. Hata hivyo, Mungu humpa amtakaye baada ya muda tukaoana, “ amesema Mama Salma.

Mama Salma amesema pamoja na upendo kutawala maisha yao, kikubwa kinachowafanya waendelee kuwa na furaha hadi sasa ni uvumilivu kati yao.
“Ninachowasisitiza vijana wa sasa ni uaminifu, mimi simu yangu anapokea mume wangu kikubwa ni kuaminiana, jiaminishe wewe ndio mke au mume hakuna mwingine zaidi yako,” amesema mbunge huyo wa Mchinga (CCM).

Akichangia katika hilo Kikwete amesema, “labda niwaambie haiwezekani sisi tumekaa zaidi ya miaka 30 halafu isitokee tumepishana kauli hata siku moja.

“Kinachotakiwa ni kumuelewa mwenzako, kuna siku huyu mama anapandisha sasa nikimuona hivyo mie nakaa kimya, nikisema na mimi nipandishe lazima mtakorofishana,” amesema “Ukimuona mwenzio kakasirika bora unyamaze kimya, ukiondoka ataona umemdharau. Kitu muhimu ni kutoziacha tofauti zenu hadi zikakua na kukubali hakuna mwanadamu aliyekamilika,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa mama salma anataka kusema.kwa umri.wake bado wapo wanawake wanaweka nywila simu zao kwa ajil ya michepuko?

Kwa mwanaume sawa ila kwa yeye mh

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu Mzee JK kasema wanaume msipojifunza kitu basi tena

Kuwa hata ye muda mwingine Mama akikiwasha anaona sio kesi anapotezea ananyamaza

Watu wa Pwani raha sana
Huyu Baba ataishi miaka mingi ka Mwinyi
Mtu na nyota yake
Ndo part uliyoielewa
 
Mama Salma amesema pamoja na upendo kutawala maisha yao, kikubwa kinachowafanya waendelee kuwa na furaha hadi sasa ni uvumilivu kati yao.

“Kinachotakiwa ni kumuelewa mwenzako, kuna siku huyu mama anapandisha sasa nikimuona hivyo mie nakaa kimya, nikisema na mimi nipandishe lazima mtakorofishana,” amesema “Ukimuona mwenzio kakasirika bora unyamaze kimya, ukiondoka ataona umemdharau. Kitu muhimu ni kutoziacha tofauti zenu hadi zikakua na kukubali hakuna mwanadamu aliyekamilika,” amesema.

WANAHARAKATI NA WAPINGAJI WA NDOA, HAWATAKI KUSIKIA HII YA 'UVUMILIVU'. WANASEMA NDOA NI RAHA TU
 
Back
Top Bottom