Mama Salma asimulia Kikwete alivyowateka mabinti

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,814
4,547
Dar es Salaam. Miaka 72 ya kuzaliwa kwa Rais wa awamu ya nne (2005-2015), Jakaya Kikwete imekuwa na simulizi nyingi zinazogusa maisha yake, kubwa ni kutoka kwa mkewe, Mama Salma Kikwete.

Wawili hawa ambao wapo kwenye ndoa kwa miaka kadhaa, walikutana kwa mara ya kwanza Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi ambapo Salma alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu na Kikwete alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilayani humo.

Katika mahojiano yao na Clouds Media leo Alhamisi, Oktoba 7, 2022 nyumbani kwao, Msoga, mkoani Pwani ikiwa ni kusherekea siku ya kuzaliwa ya mme wake, Mama Salma amesema hakuwa akifahamiana na Kikwete kabla na kwa mara ya kwanza walikutana kwenye mkutano wa kuhamasisha siasa uliofanyika chuoni kwao.

“Mimi nilikuwa naimba kwenye kwaya, yeye amekuja kuhamasisha vijana masuala ya siasa kwa hiyo nilitimiza jukumu langu la kuimba na yeye akaweka siasa zake jukwaani shughuli ikaisha,” amesema

“Basi walivyoondoka na kamati yake ya siasa na sie tukaendelea na shughuli zetu, tuliporudi bwenini mazungumzo ya wasichana wote yalikuwa ni kumhusu yeye (Kikwete) na muonekano wake akisifiwa kuwa mzuri, hata hivyo, Mungu humpa amtakaye baada ya muda tukaoana, “ amesema Mama Salma.

Mama Salma amesema pamoja na upendo kutawala maisha yao, kikubwa kinachowafanya waendelee kuwa na furaha hadi sasa ni uvumilivu kati yao.

“Ninachowasisitiza vijana wa sasa ni uaminifu, mimi simu yangu anapokea mume wangu kikubwa ni kuaminiana, jiaminishe wewe ndio mke au mume hakuna mwingine zaidi yako,” amesema mbunge huyo wa Mchinga (CCM).

Akichangia katika hilo Kikwete amesema, “labda niwaambie haiwezekani sisi tumekaa zaidi ya miaka 30 halafu isitokee tumepishana kauli hata siku moja.

“Kinachotakiwa ni kumuelewa mwenzako, kuna siku huyu mama anapandisha sasa nikimuona hivyo mie nakaa kimya, nikisema na mimi nipandishe lazima mtakorofishana,” amesema

“Ukimuona mwenzio kakasirika bora unyamaze kimya, ukiondoka ataona umemdharau. Kitu muhimu ni kutoziacha tofauti zenu hadi zikakua na kukubali hakuna mwanadamu aliyekamilika,” amesema
 
Inaonekana hii ndio njia pekee ya kuishi na Mwanamke, hata Mke wa Mobutu sese seko juzi amesimulia kwamba waliishi hivi,na maneno ya mwisho mume wake aliyasema kabla hajafa ni "nisamehe"
labda niwaambie haiwezekani sisi tumekaa zaidi ya miaka 30 halafu isitokee tumepishana kauli hata siku moja.

“Kinachotakiwa ni kumuelewa mwenzako, kuna siku huyu mama anapandisha sasa nikimuona hivyo mie nakaa kimya, nikisema na mimi nipandishe lazima mtakorofishana,”
 
Back
Top Bottom