Salamu ya Rais Samia Suluhu 'Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano' ni salamu bomba sana

Je tunaitikia vipi?
Suali zuri sana,
Nadhani tuitikie hivi!
''Tanganyika na Zanzibar'' - Hapa tunajikumbusha asili ya Jamhuri yetu ili vizazi vijavyo vijuwe nchi zilizounda muungano
au
''Tanzania Idumu milele na milele''- Hapa tunaiombea nchi iendelee kuwepo daima kwa jina halisi la Taifa.
 
Ni mbwembwe za wanasiasa tu kujionyesha wako karibu na Mungu sana ila waendelee kukubalika.
Hizo salamu ni ushenzi na unafiki tu Mambo ya kikazi na salamu za nyumba za ibada wapi na wapi
 
Kiongozi " Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano" wananchi wanaitika Jumahuri Yetu Idumu"

Kiongozi Tena " Jamhuri Yetu Idumu"

Wananchi" Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano"
 
Lakini jana kuna sehemu nimeona kasema asalaam maleko na akasema bwana asifiwe
 
Ki ukweli hata Mimi huwa sioni logic ya kutumia salamu nyingi kiasi hiki:

Asalaam Aleykum

Bwana Yesu asifiwe

Tumsifu Yesu Kristo

Mwanakondoo ameshinda

Nk nk nk

Ingetosha tu Kama ni Muislam asalimie kwa kadiri ya dini yake mara moja tu inatosha maana ukisema Asalaam Aleykum na mwingine akasema Bwana Yesu asifiwe lengo ni lile lile la kumtukuza Mungu kwa kadiri ya Imani yako, sio lazima useme salaam za dini zote.

Hiyo ya "Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" nayo sioni Kama imekaa vizuri labda Kama iliwahi kupendekezwa na ilikuwa kwenye nyaraka zao huko ila binafsi naona sio salamu maana hata hatujui tunaitikiaje.

Binafsi naona salamu nzuri ni "Habari za saa hizi mabibi na mabwana" inatosha kabisa

Akipenda kama ni mchana,

Habari za mchana mabibi na mabwana

Asubuhi, habari za asubuhi mabibi na mabwana

Jioni, habari za jioni mabibi na mabwana

Hii ndo salamu inayotambulika hapa kwetu Tanzania ndiomaana hata wageni wanaotutembelea toka mataifa mengine tunawafundisha salamu hizo

Sijui kwanini viongozi wengi huwa wanapata kigugumizi kwenye salamu hii!

Wanapenda kujivika kilemba cha kusalimia kidini hata pasipohusika

Mungu yuko kila mahali na ni kweli kabisa lazima tumtangulize kwenye kila shughuli, lakini kwenye hii mikutano ya viongozi wa kiserikali itoshe tu kusalimia kwa salamu yetu ya kawaida

Kama Kuna viongozi wa dini watatufungulia shughuli yetu kwa sala inatosha kabisa

Alichokifanya Mama Samia jana ni kigugumizi tu cha asalimieje? Ukisoma body language, anaona kero kutamka salamu zote hizo wakati hata sio lazima. Kwa kadiri ya mazoea anaona akitamka moja na nyingine akaziacha atazua maswali mengi

Mimi naona haya hiyo ya Jina la muungano aachane nayo arudi kwenye salamu yetu ya siku zote "Habari za saa hizi" inatosha sana.
 
"Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

Salam hii imepokelewa kwa hisia tofauti:

Wapagani wasio na dini wamempongeza sana.

Baadhi ya waislamu wamelaumu kwanini ameshindwa kumtambua Allah

Baadhi ya wakristo wamesema walijua tu huyu mama hawezi kusalimia Bwana Yesu Asifiwe kwa kuwa ni kosa kubwa kwa muislamu safi kumkubali Yesu kuwa ni Bwana. Wengine wakasema hata alipikuwa makamu kwenye salamu zake alikuwa anaogopa sana kutaja Yesu.

NB: ni mapema sana tumuache mama afanye kazi.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Hii ni salamu bora kutokea toka tumepata uhuru.

Mama endelea kutumia hii salamu kila mara.

Salamu hii haina ubaguzi, ni salamu yenye kuunganisha Taifa.
Kwa sasa mama anaenda vizuri sana hasa baada ya kumtoa yule jamaa aliyetaka kuendeleza chuki na kuwagawa watanzania
 
Dakika chache mida hii Mama Mtukufu ambaye ameanza kuelewa maana ya nchi na mbingu amedikrea interesti kwa kusema salamu hii; NAWASALIMIA KWA JINA LA JAMUHULI YA MUUNGANO WA TANZANIA na kamalizia kwa kufundishi kujibu kwa kusema KAZI IENDELEE. Tawile!!
Haya mbambo ya Asalamu aleikumu ni msikitini na arabuni.
Na mambo ya bwana yesu asifiwe ni kanisani na huko Yulopa.
Tuvumiliane watu wa dini za kigeni.
 
Nawasalimu katika Jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.......KAZI IENDELEE

Salaam hii wachambuzi wa mambo inaashiria nini?

Je, ni zama mpya za wazalendo wa kweli?

Je, ni namna ya kulinda Imani binafsi ya kila mtu na kuepuka salaam zisizokuwa na undugu na mtoa salaam?

Je, ni namna ya kuukana utata ulikuwepo kwenye salaam ambazo zilikuwa haziwakilishi matendo ya wahusika?

Maana si kila aliitiae jina la Muumba anamaanisha.....Rais anataka kutufundisha nini hapa?

Napokea kutoka kwenu!

Kazi iendelee.
 
"Kazi iendelee" kwanini isiwe "Kazi na bata ziendelee"? Yetu macho na muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Back
Top Bottom