Hongera Rais Samia kwa kutimiza miaka mitatu tangu uape kuwa Rais

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,053
49,737
1710900343692.png

Nawashukuru nyote kwa salamu za kheri na upendo katika kumbukizi ya miaka mitatu toka nilipoapa kuitumikia nchi yetu katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aendelee kutuongoza na kutudumisha katika haki, amani, umoja na utulivu ili yote tunayopanga na kutekeleza katika kila kona ya nchi yetu yakawe baraka kwa kila Mtanzania popote pale alipo.

Kazi Iendelee.

.....,............

Leo imetimia miaka 3 Tangu Rais Samia aape kuwa Rais wa Tanzania.

Kwa miaka hii 3, Nchi imepata mafanikio makubwa kwenye nyanja zote za Uchumi na kijamii Kwa mda mfupi kushinda wakati mwingine wowote kwenye historia ya Tanzania.

Ni wazi amesimama na kuonesha Wanawake Wana weza zaidi ya kuweza tofauti na kasumba ambayo ilikuwepo Kwa miaka Mingi.

Mojawapo ya mambo ambayo amefanikiwa na kuonesha Uongozi unaoacha alama kubwa ni haya hapa 👇👇

-Kutekeleza na kukamilisha Miradi Mikubwa Iliyoanzishwa awamu ya 5
-Demokrasia na Uhuru wa Maoni/Habari
-Kero ya NIDA
-Maji
-Afya
-Elimu
-Miundombinu hasa Vijijini
-Utalii
-Diplomasia ya Uchumi.
-Kilimo
-Michezo na Sanaa

Pia soma: IKULU, DAR: Mama Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Naskia wananchi wamebubujikwa na machozi wakisherehekea miaka mitatu ya mama
Uchumi umepanda.
Gharama ya maisha imeshuka tofauti na kipindi cha JPM.

Nidhamu makazini imeongezeka.

Usafi kwenye majiji yote ni wa kuridhisha sana.

Na nilichomkubali zaidi Mama kwenye umeme , kwa kweli umeme haukatiki mara kwa mara tofauti na awali..

Ni mengi sana Mama amefanya kiukweli ametisha
 
Back
Top Bottom