Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.
Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.
Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.
Sasa tunaingia magotini....
Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?
Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.
LAKINI
Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..
Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.
Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?
Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.
Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.
Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...
SERIKALI.
Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.
Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...
SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.
©Bibi Happy J