Sala ya siku 3, je kama nchi tuna nini? Tunaomba huku hakuna juhudi za kupambana na corona? Wenzetu wanasali au wanawekeza kwenye afya?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

©Bibi Happy J
 
Ukiangalia maneno ya Magufuli binafsi kwenye hii issue ya Corona kusema kweli bora angekuwa kimya amuache Waziri wa Afya awe mzungumzaji.

Mwanzo alituambia ka- Corona tusitishane, idadi ya wagonjwa ikaongozeka, na taarifa za vifo zikaanza kusikika pia.

Wakati huu tupo katikati ya kupambana na janga anatuambia tusali kila mtu kwa imani yake, lakini wote tunaotakiwa tusali tuna maarifa, na mojawapo ya hayo maarifa ndio yaliyomtoa yeye DSM, yakampeleka Dodoma, kisha Chato, hiyo sio accident anaikimbia Corona.

Mengine ni kuvaa mask, kunawa mikono kwa sanitizers, n.k, hivyo badala ya kusisitiza kwenye kusali, vyema akasisitiza na njia nyingine za kupambana na huo ugonjwa, na huko kwenye kusali muende mmevaa mask, vinginevyo....!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

©Bibi Happy J
Mwenye masikio na asikie,mwenye macho naye ataona.Tusisali kwa Mungu kwa kumjaribu,ina maana wenzetu dunia nzima hawasali wala kumwomba Mungu hadi wateketee kwa Corona?
Sala ziendelee na tufuate masharti ya kujikinga na Corona kwa kufuata best preventive measures kama wenzetu wafanyavyo.Hatupo tofauti na hatuishi ndani ya cube.
 
Hakusema uwekezaji upungue kwenye sekta ya afya kisa Mungu yupo, Trumple aliwah pia kutangaza siku 1 ya maombi ya kitaifa hvo wenye iman zao waendelee kuamini ata kama kuna jaribio kubwa kama hili but haimaanishi wamuache wamuaminie.
 
Kutumia akili na maarifa ni zaidi ya sala, ni kumuiga Mungu.

Tumekuwa tunasali miaka yote na bado hakuna maajabu makubwa yanatokea zaidi ya kuwaneemesha Matapeli wa Imani kina G boy, Mwa Mpesa, Mzee wa Kupaka na wengine.

Sio kwenye Michezo, Elimu, Uchumi tulipoitikisa dunia kwa sala zetu na kumataja Mungu kila kukicha.
 
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

©Bibi Happy J
Naona tunarudishwa kwenye Vita vya majimaji. KINJEKITILE NGWALE
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom