Sala ya siku 3, je kama nchi tuna nini? Tunaomba huku hakuna juhudi za kupambana na corona? Wenzetu wanasali au wanawekeza kwenye afya?

Lakini tambua kuwa Rwanda wanafanya testing, sisi hatufanyi. Kwa kuwa hatufanyi, hatujui hata idadi ya walioambukizwa. Tunasuburi mtu aumwe ndiyo apimwe au ahisiwe kuwa ameambukizwa, ndiyo apimwe.

Rwanda wanafanya testing. Wanawagundua walioambukizwa hata kabla ya kuanza kuumwa. Kwa takwimu zilizopo, mpaka sasa hakuna raia wa Rwanda aliyepoteza maisha kwa Covid 19.
Asante kwa kumuelewesha.Hakika unafatilia yanayoendelea nchin kwetu.Pia drones hupita angani kila Mara zikihamasisha kupima na kuelimisha watu juu ya corona kwa sababu tunaamin si wananchi wote wenye access ya kupata taarifa kupitia tv,simu au radio.
 
Nilifikiri wewe ni Mtu wa kiroho kumbe hujui kitu unaleta siasa siasa kwenye mambo ya Mungu.
Hujasoma Mfalme Daudi alipoteseka na njaa miaka mitatu mfululizo alimtafuta Bwana na akamwambia chanzo cha tatizo la njaa na namna ya kulimaliza.Maombi aliyoagiza Rais yanaweza toa solution nzuri zaidi ya kumaliza tatizo siyo copy na paste za Wazungu ili kupata msaada wao.
2Samweli 21:1...
Tusali Sana sio kwa siku tatu tu kila siku, uzuri sisi kila siku tunasali na tunaomba corona iishe ,
Sema tusali kwa tahadhari nahisi hujamuelewa mtoa mada,

Kitu kingine hata hizi dini pia tumekopi kwa wazungu aisee,
Kwa hiyo ni vyema kukopi mazuri na tukaacha mabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati yao waliowekeza kwenye afya ni nani aliyefanikiwa kuishinda korona?.
mimi naona bora magufuli aliyeweka matumaini yake kwa MUNGU.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Tuambie ni wapi walikowekeza kwenye sala badala ya Afya na wakatoboa!China wamefanikiwa kupunguza tatizo kwa hatua walizochukua!Huyu wa kwetu anatwambia tusitishike,tuchape kazi kwani Corona ni kaugonjwa kadogo!
 
Binafsi yangu MAGUFULI YUPO SAHIHI KATIKA HILI..
mimi naamini sana katika MUNGU muweza wa yote.
Wala sina wasiwasi TUTASHINDA tukimtegemea yeye..
Magufuli ameonesha kuwaamini viongozi wa dini . naamini hawatamuangusha.
TUSEME TU UKWELI SAYANSI KWA SASA IMESHINDWA

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Sayansi imeshindwa vipi?Mungu ndio katupa hayo maarifa ili kupitia sayansi tupate ufumbuzi!Ni sayansi ndio imetuambia namna ugonjwa unavyoambukizwa na namna ya kujikinga,tiba itapatikana inshallah maana ni gonjwa jipya!
 
View attachment 1421428
Maji ya kutiririka ni kutoka kwenye vidonga na vidumu
huyu ndo anajua kujikinga swahihi
1587109008920.png
 
Mungu ametupa nguvu,Mungu ametupa maarifa,tutumie maarifa kupambana na Corona sio tu kulilia tu bila kuweka juhudi na maarifa ya kubuni njia ya kuishinda Corona.
Tusishindwe kutekeleza wajibu wetu tukakimbilia kutoa matamshi ya huruma tu.
Kumcha Mungu sio kilemba cha ukoko.
 
Mungu hubariki jitihada za mwanadamu pale anapotumia akili, nguvu na afya aliyopewa na mwenyezi Mungu.

Huombi Mungu akupe unga, mchele, au sukari. Wala huombi Mungu akupe flagyl au panadol ila unamwomba Mungu abariki jitihada zako za kilimo au kazi yako ili uwe na uwezo wa kula na kuilisha familia yako.

Unaomba ili dawa unayotumia ikafanye kazi katika mwili wa mgonjwa au Mungu awaongoze matabibu katika kumtafutia mgonjwa wako tiba sahihi, huku wewe ukihangaika kutafuta hela ya kulipia matibabu. Kushindwa kumlipia mgonjwa wako wakati una akili, nguvu na afya njema, ni kushindwa kutimiza wajibu wako. Ni dhambi.

Paulo alikuwa akishona nguo ili kupata hela ya matumizi. Pamoja na miujiza yote Mungu aliyoitenda kwa kupitia Paulo lakini Paulo alifanya kazi ili apate kuishi.

Mungu alimwokoa Nuhu na gharika kwa kumtaka atengeneze mashua. Nuhu aliokolewa na Mungu kwa kufanya kazi.

Mtoto Musa aliokolewa kwa kupitia Mama yake ambaye alitoroka naye. Akamtengenezea kikapu, akamhifadhi kwenye mto ambako binti ya Farao alizoea kwenda. Mama yake Musa ilibidi afanye kazi ili kupokea uokoaji wa Mungu.

Herode alipoamru watoto wote wa kiume wauawe, Mungu alimwambia Yusuf aondoke na Mariam kwenda Misri ili mtoto asiuawe. Mariam na Yusuf walifanya kazi ili kumwokoa mtoto Yesu.

Katika kuwaokoa Waisrael waliokuwa wakiuawa na Goliati, Daud alitengeneza kombeo alilolitumia kurushia jiwe. Na jiwe hilo Mungu akalipatia nguvu, na hata kumwua Goliati. Daud alifanya kazi ili kuwaokoa wana wa Israel.

Wakati mbalimbali Waisrael walipoonewa na maadui zao, waliandaa jeshi lao. Walienda mstari wa mbele. Walipigana, huku makuhani wakiomba. Mungu alibariki jitihada zao, hata wakaweza kushinda vita. Walifanya kazi.

Bikira Maria, alipewa nafasi ya kuwa mbarikiwa kuliko wanawake wote. Na baraka hiyo aliipata baada ya kukubali kubeba mimba, kutembea nayo kwa miguu umbali mrefu mpaka Betlehem, na kwenda kujifungulia kwenye zizi la wanyama. Hakushtukia mtoto yupo mkononi. Alifanya kazi. Alitumia akili pia.

Mungu wetu hutafuta mahali pa kuweka baraka na neema katika jitihada mbalimbali tunazozifanya. Kama hatujapatengeneza mahali pa Mungu kushushia baraka, neema na ulinzi wake, kamwe hatutapata baraka na wala hutapokea neema wala ulinzi wake.

Kutotimiza wajibu wako ni dhambi.

Kama wewe ni kiongozi mkuu wa nchi, wajibu wako mkuu ni upi katika kipindi hiki cha janga la Covid 19? Usipotimiza wajibu huo, unatenda dhambi.

Kama wewe ni kiongozi wa kiimani, wajibu wako kwa wakati huu ni upi? Usipoutimiza wajibu huo ni dhambi.

Kama wewe ni tabibu, wajibu wako mkuu wakati huu ni upi? Usipoutimiza wajibu huo, umetenda dhambi.

Kama wewe ni mfanyabiashara, mkulima, mkuu wa idara, mkuu wa majeshi, Polisi, n.k; wajibu wako ni upi? Usipoutimiza, hutapokea baraka wala ulinzi au neema za Mungu.

Mimi kama mwananchi wa kawaida, mwanataluma, mfanyakazi wa kawaida, mpiga debe wa daladala, mmiliki wa biashara mbalimbali, wajibu wangu ni upi? Usipoutimiza huwezi kupata ulinzi, kupokea neema zake wala baraka zake.

Kila mmoja ana wajibu wake. Ndiyo maana ya viungo ni vingi lakini mwili ni mmoja.

Mkuu wa nchi asifanye kazi ya unabii au ukuhani. Mkuu wa mkoa asijifanye mhubiri au mwombaji, daktari asijifanye kuhani. Kila mmoja atimize wajibu wake.

Tatizo letu kwa sasa, kwa kushindwa kutimiza wajibu wetu, kila mmoja anataka awe kuhani, nabii au mhubiri.

Kila mmoja aende kwenye wajibu wake. Maana Mungu atampima kila mmoja kwa wajibu aliomwekea.

Kusali na kuomba wakati wote ni jambo muhimu lakini tunaomba kitu gani?

Tunaomba ili siku moja tukiamka tuone ugonjwa haupo? Mbona haikuwa hivyo kwa ugonjwa wa plague (1720), kipindupindu (1820), Spannish Flu (1920), kifua kikuu, au ndui iliyoua zaidi ya watu 300m.

Sisi tunamwomba Muumba wetu abariki jitihada ambazo kila mmoja anazifanya kupambana na ugonjwa huu kama vike-

Mungu awaongoze wanasayansi wafanikiwe kupata chanjo ili ugonjwa utokomezwe kama ilivyotokomezwa ndui;

Mungu awaongoze wanaofanya tafiti kuujua ugonjwa huu vizuri, wapanuliwe ufahamu ili tujue kuenezwa kwake, kujikinga kwake, na tiba sahihi;

Mungu awajalie neema ya upendo wa kweli wanaowahudumia wagonjwa wetu ili waishi katika upendo na faraja mioyoni mwao wanapowahudumia wagonjwa wetu;

Mungu awajalie ufahamu wale wenye nafasi yoyote ya kusaidia, waongozwe kwenye utayari na kujua njia sahihi za kusaidia.

Mungu hashushi ulinzi na neema kwa watu wajinga. Ndiyo maana anasema, watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu wetu hujivunia watu werevu, wenye bidii na wasiokata tamaa.
 
MAOMBI MAALUM YA SIKU TATU YA KITAIFA
KWA AJILI YA UGONJWA WA COVID-19
SIKU YA KWANZA (17.4.2020)
Utangulizi
“Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe?” (Yon.3:6-10).
Habari ya Ugonjwa wa COVID-19 imemfikia Rais John Pombe Magufuli. Amepiga mbiu kwa Watanzania wote, kama alivyofanya mfalme wa Ninawi. Wito mkuu wa maombi haya ni TOBA na KUMLILIA Mungu kwa ajili ya KUIPONYA Nchi yetu ili TUSIANGAMIZWE. Kwa hiyo, tuombee mambo yafuatayo:
SHUKURANI
1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Rais kuona haja ya maombi ya kitaifa.Soma kwa sauti Zaburi yote ya 33.
2. Mshukuru Mungu kwa ajili ya kupata nafasi ya kufanya maombi haya.
3. Mshukuru Mungu kwa ulinzi wa Nchi yetu hadi sasa.
TOBA
1. Tubu kwa ajili ya dunia iliyopota na kumuacha Mungu(Zab.53). Soma kwa sauti Zaburi yote ya 51 kwa niaba ya dunia nzima.
2. Tubu kwa ajili ya kutokusikiliza mausia ya Neno la Mungu linalohubiriwa kila siku. Soma kwa sauti Daniel sura ya 9 yote.
3. Omboleza kwa ajili ya yanayotupata sisi kama wanadamu. Soma kwa sauti Maombolezo sura yote ya 5.
4. Muombe Mungu kwa damu ya Agano Jipya ya Yesu Kristo akumbuke rehema zake kwa watu wake(Hab.3:2)
MAOMBI
1. Omba Mungu akumbuke maombi ya Raisi wetu na kuiponya Nchi yetu na uharibifu wowote kiafya, kiulinzi na kiuchumi (Isa. 38:6).
2. Ombea uponyaji kwa wagonjwa wa COVID-19(Mt.8:17).
3. Kataa nguvu za kaburi na roho ya mauti juu yao. Soma kwa sauti Hosea.13:14 na 1Kor.15:55-57.
4. Omba ulinzi kwa wasiougua na omba kwamba ugonjwa usiendelee kusambaa kwa watu wengine. Soma kwa sauti Zaburi yote ya 91.
5. Futa maneno yaliyosemwa na watu kuwa Afrika itashuhudia maiti zikizagaa mitaani kwa sababu ya COVID-19. Tuma malaika mharibu akaue maneno hayo katika ulimwengu wa roho (Isa.54:16, 17).
6. Ombea ulinzi wa Damu ya Yesu juu ya watalaam wa afya. Pia Mungu awape hekima na upendo wa kuwahudumia wagonjwa(Isa. 11:2,3)
MWISHO
1. Mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi ya kuungana na watakatifu wengine duniani kufanya maombi haya maalum.
2. Muombe Mungu ashughulike na mahitaji yako binafsi. Atakabali sadaka yako hii ya maombi(Zab.20:1-4)
AMINA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha kwanza nimuombee Rais, shenzi type niache kuombea wagonjwa nimuombee Rais.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
wewe unaona sayansi imefaulu kwenye corona?
sayansi IMESHINDWA.
Na ndo maana wenyewe wanatuambia "STAY HOME FOR US".
Yaani mpaka wenyewe wamekiri kuwa corona imewashinda.
SASA TEGEMEO LINGINE NI LIPI ZAIDI YA MUNGU PEKEE MUWEZA WA YOTE?
Sayansi imeshindwa vipi?Mungu ndio katupa hayo maarifa ili kupitia sayansi tupate ufumbuzi!Ni sayansi ndio imetuambia namna ugonjwa unavyoambukizwa na namna ya kujikinga,tiba itapatikana inshallah maana ni gonjwa jipya!
adoringallah1_20200410_1.jpg
growingislam_20200408_7.jpg
growingislam_20200408_3.jpg


"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Back
Top Bottom