Siku ya Furaha duniani: Je unatambua kuwa bila ya kuwajibika(responsibility) haiwezekaniki kabisa kuwa na FURAHA ya kweli? Siongelei RAHA

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,070
Je? mtu anaweza kuwa na furaha bila ya kuwajibika. Hapana. Hiyo haipo kabisa. Kwa nini ninasema hivyo? Kabla sijaanza naomba kuanza na ufafanuzi kiasi;

Furaha inahusianishwa na hisia za utulivu na kutosheka na kile kilichopo (what IS). Utulivu wa moyo unakuja pale ambapo mtu anahisi anao uwezo wa kuamua mazingira yake na hata kuyabadili apendavyo. Kimsingi kuyaendesha, yaani mfano anaweza kuamua kujongea au kutulia tu.

Hicho kitendo cha kuyaendesha na kuwa na uwezo wa kutia nia na matakwa binafsi kufanya mambo yatokee ndio inaitwa UWEZO.

Tukizungumzia uwezo,ninafahamu wapo watu wengi tu ikiwamo mdogo wangu mmoja wanaofikiri kwamba hiki ndio kitu cha juu kabisa. Lakini mimi nafikiri kwamba huu ni mwanzo tu. Tena ni wa pili kwa wajibu. Yaani unaanza wajibu halafu ndio uwezo. Mwenye wajibu mkubwa ndio anapata kuwa na uwezo mkubwa!

Hivyo basi uwezo wa kuyafanyia kazi matakwa ya mtu unampa kuendesha mambo na mwisho utulivu wa moyo unaopelekea FURAHA. Tafakari hilo kwa muda, na chukua hiyo point.

Jambo hili linahusiana vipi na furaha;

Mtu hujisikia furaha pale mambo yanapokuwa yanaenda kulingana na matakwa yake. Ikiwa mtu atawajibika na kuchukua jukumu la kuendesha visababishi vingi zaidi basi ataweza kuamua na kuathiri matokeo kwa kutenda impasavyo.

Watu wawili wanaweza kupokea kitu kimoja kiletacho raha, kwa mfano kufaulu alama za juu(A+) katika mtihani. Yule ambaye atakuwa na furaha ya kweli ni yule atakayewaza kuwa alifanya bidii na amewajibika kupata matokeo hayo. Yule aliyeibia mtihani na majibu hatakuwa na furaha ya kweli. Weeh! Subiri kidogo!, Huyo mtu anaweza kuwa na furaha vilevile maana naye pia akifikiri juhudi zake katika kuiba/kuangalizia huko zimempatia hiyo A+. Atakayekosa furaha hapa ni yule tu ambaye kufaulu huko ni kinyume na matakwa yake. Labda malengo yake ilikuwa kufeli.

Mfano nilioutoa juu unaweza ukakuchanganya kiasi, hebu tuangalie mfano mwingine. Mungu anafahamu kabisa kwamba watu watakuwa na furaha zaidi ikiwa watawajibika katika kuleta matokeo. Yeye angeweza kufanya kila kitu lakini bado ameruhusu na ameupa thamani kubwa mchango wa mwanadamu. Tunaomba kisha tunapokea. Tunaishi kisha tunachagua kwenda mbinguni au kufa tu (kupatwa na mauti ya pili). Mbinguni patajawa na mandhari ya furaha kwa sababu patafurika watu wawajibikaji. Kama watu wangebebwa tu na kupelekwa mbinguni bila hili wala lile wasingeiishi furaha ukilinganisha.

Katika kuishi nimejionea. Kwamba hata kama matokeo ni machungu kweli, yule mpokeaji wa athari hizo anaweza asihuzunishwe hata kidogo. Hii ni hususani pale ambapo anajihisi kuwa alitaka mambo yawe hivyo na amewajibika kikamilifu kwa hilo. Hapa watakaoweza kung’amua jambo hili ni wale tu wenye-uwezo-wa-kuhiari.

Pale ambapo mtu mwenye kuwajibika anaumizwa na jambo. Hawezi kuipoteza furaha yake yote na kuwa mwenye huzuni. La. Ataangalia kwenye visababishi vilivyopelekea maumivu. Atatazama ni vipi angeweza kuviendesha na atakavyoviendesha kwa hapo baadaye. Hivyo kimsingi mtu huyu mwisho wa siku atakuwa na furaha kwa sababu amepata funzo UJINGA wake umeshapona sasa.

Kutokutulia moyoni, unyonge na huzuni huwa vinaenda pamoja kama tu ambavyo uwajibikaji, uwezo na furaha vinavyoenda pamoja
 
100%. Kufanya kwa bidii na weledi kazi halali ndiyo msingi wa furaha ya kweli.

Ndiyo maana wale wanaopata pesa za burebure wanaishia kuzitawanya na kuzitapanya baa, kwa vimada, makahaba, show-offs, kununua vitu vya kifahari wasivyohitaji, nk. wakidhani kwa namna hiyo wanaweza kuipata furaha.

Utasikia wakisema eti walevi ndio watu wakarimu zaidi, lakini wanasahau kwamba utoaji wao ni kwa kusudi la kujitafutia starehe binafsi wao wenyewe.

Na pia utoaji wao si wenye manufaa. Watakununulia bia hata mia, lakini ni nadra sana kwao kumsaidia mgonjwa au mhitaji.

Mtu anaweza kuwa na kipato kiduchu ila akawa na furaha kuliko tajiri mwenye mamilioni ya dola.

Hata hivyo bila uchumi mzuri, furaha ni kitendawili kizito.

Uwajibikaji bora huleta kipato (na hata afya ya akili, mwili na kijamii) -- hivi huchangia asilimia kubwa sana kuleta furaha ya kweli na maisha marefu yenye manufaa.

Tunaweza kuwasaidia wengine vyema zaidi iwapo sisi wenyewe tuna furaha. Bila furaha hata ufanisi katika majukumu hunakisika.

Uwajibikaji + kuridhika + kumtegemea Mungu = furaha.
 
Mke wangu ananipa furaha.
Safi sana, haujaishia kupata raha kwa mkeo. Na ndio inavyotakiwa katika familia.

Umefikia kiwango cha kupata furaha kwa kuwajibika kwako kuwa mume wa huyo mke wako, naye anapokubaliana na wajibu wako kwake na kuuishi nuie ndio furaha yenu wote.🤔🤔....

I mean, hata mi nikirudia kusoma hiyo aya niloandika inanikomfyuz kidogo ☺😅😅. Anyway jongera saana
 
FURAHA ni moja ya matunda ya Roho Mtakatifu (Roho wa Mungu) ndani ya mtu. Ni zao lipatikanalo baada ya mtu kumkubali na kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake [yaani kuzaliwa mara ya pili]. Mtu yeyote mwenye hili tunda la Roho Mtakatifu, haijalishi atapitia mambo gani magumu au mabaya, Bado utamwona akiwa na furaha na tumaini la kweli. GAL 5:22-23.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
FURAHA ni moja ya matunda ya Roho Mtakatifu (Roho wa Mungu) ndani ya mtu. Ni zao lipatikanalo baada ya mtu kumkubali na kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake [yaani kuzaliwa mara ya pili]. Mtu yeyote mwenye hili tunda la Roho Mtakatifu, haijalishi atapitia mambo gani magumu au mabaya, Bado utamwona akiwa na furaha na tumaini la kweli. GAL 5:22.


JESUS IS LORD&SAVIOR
Wagalatia 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²² Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
²³ upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
 
FURAHA ni moja ya matunda ya Roho Mtakatifu (Roho wa Mungu) ndani ya mtu. Ni zao lipatikanalo baada ya mtu kumkubali na kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake [yaani kuzaliwa mara ya pili]. Mtu yeyote mwenye hili tunda la Roho Mtakatifu, haijalishi atapitia mambo gani magumu au mabaya, Bado utamwona akiwa na furaha na tumaini la kweli. GAL 5:22-23.


JESUS IS LORD&SAVIOR
Galatians 5:22-23
[22]But the fruit of the [Holy] Spirit [the work which His presence within accomplishes] is love, joy (gladness), peace, patience (an even temper, forbearance), kindness, goodness (benevolence), faithfulness,
[23]Gentleness (meekness, humility), self-control (self-restraint, continence). Against such things there is no law [that can bring a charge].
 
Sikubaliani na hayo maelezo ya kidini

Ila hoja yako ni nzuri

Hata ubongo wako unaachilia hormone ya dopamine, ukipania kitu sana, ukakitafuta halafu ukakipata

Hiyo hormone inakufanya uhisi furaha na inakupa motisha
 
Back
Top Bottom