Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Mhalifu hawi mhalifu hadi pale itakapothibitika!

Sakata la mfalme Zumaridi (Kiongozi wa kanisa la Zumaridi huko Mwanza) Linaacha midomo wazi kwa wapenda haki na utii wa sheria!

Sipo hapa kumtetea Mfalme Zumaridi, Bali nashangaa namna ya uharamu wa ukamtaji!

Taratibu za ukamataji kwa mujibu wa sheria ziko wazi kabisa lakini mamlaka zimekuwa zikionesha kufeli Mara kwa Mara kutekeleza sheria hiyo jambo ambalo limekuwa likitweza utu wa watu wasio na hatia.

MFANO! mambo kama haya yalitokea huko mtwara hadi kufedhehesha uongozi wa polisi ambayo yalianza hihivi kwa kufumbafumba mambo,

Mfano 2. Ni huko ARUSHA Kuna taarifa ya askali mzalendo kulalamika kutaka kuuwawa na polisi wenzake kwa mambo Yale Yale kama ya mtwara na serikali iko kimya.

SASA NI HILI SAKATA LA TATU LINALOTIA KICHEFCHEFU

Ni TUKIO LA zumalidi Siku ya kwanza inaripotiwa kwamba polisi waliruka ukuta/geti ili kuingia kwa Zumalidi! Kitendo hiki kilitakiwa kulaaniwa na kila mtu! (Waliruka kwa Zumalidi kesho wataruka kwako)

Kama kulikuwa na ulazima wa kufika pale kwanini hawakufuata utaratibu wa upekuzi unavyotaka? Kwanini hawa kumshirikisha mwenyekiti wa mtaa/mjumbe? Kwanini waliruka ukuta kama jambazi! (VIPI KAMA ZUMARIDI ANGEJIBU MASHAMBULIZI KWA KUFYATUA RISASI KWA POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIPORUKA UKUTA?) Ina maana wangejibu kwamba walikuwa kwenye mapambano na majambazi au?

Kwa utaratibu walio utumia polisi hauna tofauti na utarabu wa kijambazi! Na hili linachangia sana siku hizi RAIA kutokutofautisha kati ya jambazi na polisi.

Tukiachana na mbinu ya ukamataji!

Riport ya polisi ina ukakasi mkubwa juu ya mtuhumiwa Zumaridi!

Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Mbona jumuiya na taasisi kibao tunawaona wanakusanyika na kukesha na haijawahi kutajwa kuwa ni kosa?

Zumalidi kasafirisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?

Hapo taifa juzi wakatoliki walikusanyika mbona haikutamkwa kuwa ni usafirishaji wa binadamu?

Kina mwingira na wachungaji kibao Tanzania kila kutwa wanakusanya watu na haisemwi ni usafirishaji,

INAKUWAJE JAMBO LILE LILE LIWE HALALI KWA MWAMPOSA LAKINI LIWE HARAMU KWA ZUMARIDI?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Nawashauri TAKUKURU WAINGILIE KATI!
Haiwezekani sheria zipo wazi, kwanini zisingefuatwa kama kweli ZUMALIDI anamakosa makubwa hivyo!

Mimi kwa utashi wangu nahisi sakata la Zumaridi lina maslahi binafisi!

TUKIRUHUSU HAYA YA UKIUKWAJI WA SHERIA HAKUNA ATAKAYEBAKI SALAMA!

Itakuwa mtu akikosana na polisi wanakuja kuluka ukuta! Na majambazi nao watatumia mwanya huohuo kufanya uharifu!

Updates
ZUMARIDI Aiambia mahakama kwamba wakati polisi walipovamia nyumbani kwake walimpiga na kuchukua pesa kiasi cha 19milioni alizokuwa Nazo kama sadaka

Updates FEB 2023
DPP Atupilia mbali sakata la Zumaridi baada ya kujiridhisha hakuwa na kosa!

Wengine hili tuliliona mapema
Screenshot_20230208-202220.png
 
Nakubaliana nawe kwa maana ya ukiukwaji wa sheria ila mfalme wako anakashfu imani za watu wengine kitu ambacho kinaweza sababisha uvunjifu wa amani
Report ya polisi haijasema hayo! Imesema amekamatwa kwa kusafilisha binadamu? Jiulize hao binadamu Zumalidi kakutwa nao anawapeleka wapi kwenye wapi kwa maslahi gani hadi iwe jinai?

Watu wanaweza kukusanyika kwa mtu kufurahi ,kusali au kufanya msiba, je ni kosa watu kukusanyika kwa mpendwa wao?
 
Sheria ipi?
Hawa wapuuzi wakamatwe maana wanawafanya watu kuwa wajinga wazembe na wapumbavu... She deserved hiyo treatment kuharibu watoto wa watu si sawa
Ahukumiwe iwe fundisho kwa matapeli wa mfano wake
Ahukumiwe kwa kosa gani?
 
Mhalifu hawi mhalifu hadi pale itakapothibitika!

Sakata la mfalme Zumalidi (Kiongozi wa kanisa la Zumalidi huko mwanza)

Linaacha midomo wazi kwa wapenda haki na utii wa sheria!

Sipo hapa kumtetea Mfalme Zumalidi, Bali nashangaa namna ya uharamu wa ukamtaji!

Taratibu za ukamataji kwa mujibu wa sheria ziko wazi kabisa lakini mamlaka zimekuwa zikionesha kufeli Mara kwa Mara kutekeleza sheria hiyo jambo ambalo limekuwa likitweza utu wa watu wasio na hatia!

MFANO! mambo kama haya yalitokea huko mtwara hadi kufedhehesha uongozi wa polisi ambayo yalianza hihivi kwa kufumbafumba mambo,

Mfano 2. Ni huko ARUSHA Kuna taarifa ya askali mzalendo kulalamika kutaka kuuwawa na polisi wenzake kwa mambo Yale Yale kama ya mtwara na serikali iko kimya.

SASA NI HILI SAKATA LA TATU LINALOTIA KICHEFCHEFU ...

Ni TUKIO LA zumalidi Siku ya kwanza inaripotiwa kwamba polisi waliruka ukuta/geti ili kuingia kwa Zumalidi! Kitendo hiki kilitakiwa kulaaniwa na kila mtu! (Waliruka kwa Zumalidi kesho wataruka kwako)

Kama kulikuwa na ulazima wa kufika pale kwanini hawakufuata utaratibu wa upekuzi unavyotaka? Kwanini hawa kumshirikisha mwenyekiti wa mtaa/mjumbe? Kwanini waliruka ukuta kama jambazi! (VIPI KAMA ZUMALIDI ANGEJIBU MASHAMBULIZI KWA KUFYATUA LISASI KWA POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIPORUKA UKUTA?) Inamaana wangejibu kwamba walikuwa kwenye mapambano na majambazi au?

Kwa utaratibu walio utumia polisi hauna tofauti na utarabu wa kijambazi! Na hili linachangia sana siku hizi RAIA kutokutofautisha kati ya jambazi na polisi.

Tukiachana na mbinu ya ukamataji!

Riport ya polisi inaukakasi mkubwa juu ya mtuhumiwa Zumalidi!

Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Mbona jumuiya na taasisi kibao tunawaona wanakusanyika na kukesha na haijawahi kutajwa kuwa ni kosa?

Zumalidi kasafilisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?

Hapo taifa juzi wakatoliki walikusanyika mbona haikutamkwa kuwa ni usafirishaji wa binadamu?

Kina mwingira na wachungaji kibao Tanzania kila kutwa wanakusanya watu na haisemwi ni usafirishaji,

INAKUWAJE JAMBO LILE LILE LIWE HALALI KWA MWAMPOSA LAKINI LIWE HARAMU KWA ZUMALIDI?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Nawashauri TAKUKURU WAINGILIE KATI!
Haiwezekani sheria zipo wazi, kwanini zisingefuatwa kama kweli ZUMALIDI anamakosa makubwa hivyo!

Mimi kwa utashi wangu nahisi sakata la Zumalidi lina maslahi binafisi!

TUKIRUHUSU HAYA YA UKIUKWAJI WA SHERIA HAKUNA ATAKAYEBAKI SALAMA! Itakuwa mtu akikosana na polisi wanakuja kuluka ukuta! Na majambazi nao watatumia mwanya huohuo kufanya uhalifu!
Hawafati tena PGO.Bora enzi za IGP Mangu
 
Back
Top Bottom