Hakuna sheria Zanzibar inayokataza kula mchana wakati wa ramadhani

DUMPER

JF-Expert Member
Sep 19, 2017
531
865
Polisi zanzibar ni waongo sana, hakuna sheria yoyote Zanzibar inamkataza mtu kula wakati wa ramadhani.

Miaka ya nyuma kesi zote zilizopelekwa mahakamani mashitaka yalisomeka tofauti, badala ya shitaka la kula mchana wakati wa ramadhani, mashitaka yote yaliletwa mahakamani kwa kosa la uzururaji.

Hakuna sheria zozote hao watu ni wajinga tu.

====

Kusoma zaidi kuhusu marufuku za kula wakati wa ramadhani pamoja na marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
 
Polisi zanzibar ni waongo sana, hakuna sheria yoyote Zanzibar inamkataza mtu kula wakati wa ramadhani.

Miaka ya nyuma kesi zote zilizopelekwa mahakani mashitaka yalisomeka tofauti, badala ya shitaka la kula mchana wakati wa ramadhani, mashitaka yote yaliletwa mahakamani kwa kosa la uzururaji.

Hakuna sheria zozote hao watu ni wajinga tu.
Hakuna sheria hiyo ila kuna Shariah
 
Wewe nenda kale uone ,tangu lini mkawa na msimamo wala nguruwe 😅😂

Ishu ya Joshuq Mollel mliishia wapi?
 
Badala ya kuishi kwa matamko ya viongozi; suala la kutokula kipindi cha Ramadhan huko Zanzibar lingerasimishwa kwa kutungiwa sheria au kuingizwa kwenye katiba zote mbili - ya Zanzibar na ya Muungano ili kila mwananchi afahamu na liwe enforceable na wasimamizi wa sheria bila ukakasi.

Sio sawa kuishi kwa kuviziana.
 
Polisi zanzibar ni waongo sana, hakuna sheria yoyote Zanzibar inamkataza mtu kula wakati wa ramadhani.

Miaka ya nyuma kesi zote zilizopelekwa mahakani mashitaka yalisomeka tofauti, badala ya shitaka la kula mchana wakati wa ramadhani, mashitaka yote yaliletwa mahakamani kwa kosa la uzururaji.

Hakuna sheria zozote hao watu ni wajinga tu.
Kosa la uzururaji lenyewe ni la kizushi sana.

Kwa sababu Mtanzania kuzurura sehemu yoyote iliyo open to the pubkic Tanzania ni haki yake ya kikatiba.

Sasa, uzururaji maana yake nini? Na kwa nini kumpa mtu kosa la uzururaji wakati katiba inatoka haki ya kuzunguka nchi nzima, si kuvunja katiba?
 
Kila siku tunasema hapa Muungano uvunjwe, maana upo kitapeli na kinyonyajii, kwan mama kizimkazi si auvunje tyuuh.

Watu tumeshachoka na manjegeka ya wana Paje.
 
Mijitu imefunga bado inabambikia watu kesi za uwongo..
Kuna mkuu wa wilaya huko unguja anasema ile video ya jamaa alikuwa anachapwa ni ya 2017 na ni kwa kosa la ulevi.
Huku akitanabaisha kwamba zanzibar hakuna sheria inayokataza mtu kula
Ni uhuni tu wa vijana wasio na kazi kusumbua jamii 🙂🙂
Jamaa dini yao wanaona aibu wao
 
Back
Top Bottom