Hamad Masauni: Taasisi ya dini ya Mfalme Zumaridi haijasajiliwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali itazichukuliwa hatua taasisi zote za kidini ikiwemo taasisi inayoendeshwa na Diana Bundala maarufu ‘Zumaridi’ ambazo zinajiendesha kinyume na tamaduni za Kitanzania.

Akizunguma katika kikao kati yake na viongozi wa mashirikisho na mabaraza ya kidini, amesema miongoni mwa taasisi hizo ni zile ambazo hazijasajiliwa likiwemo kanisa la Zumaridi.

“Zipo tasisi ambazo zinaibuka kama huyo Zumaridi, hajasajiliwa. Ametoka huko anajiita yeyeni kiongozi wa dini. Utakuta wengine wanahamisisha mapenzi ya jinsia moja, mwingine anajiita yeye ni Mungu, wanazungumza mambo ya ajabu ambayo hayawezi kukubalika,” ameonya Masauni.

Amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua kwa wote wanaokwenda kinyume na sheria kimaadili, mila na desturi pamoja na kueleza kwamba inapobainika kuna vikundi vya kidini vinavyotia shaka, ni vyema kutoa taarifa Ofisi ya Msajili ili kuiweka jamii katika hali ya usalama.

“Nichukue fursa hii kuwasihi viongozi wetu wa kiroho, kutoleta taharuki katika jamii kutokana na mafundisho mnayoyatoa yanaweza kutugawa katika kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili,” ameeleza.

---
Pia soma
- Serikali endeleeni kumchekea Zumaridi mpaka atakapoleta madhara
 
HATUDANGANYIKI!!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Zumaridi analelewa sana, sikui kuna mtu mwenye mamlaka nyuma yake? Hebu angalia hii clip hapa
 
Sasa anatwambia sisi iki tufanyeje? Anataka tujichukulie sheria mkononi?
 
Huyu mzanzibari asitutoe kwenye reli ili tusiwabane ndugu zake waliotuingiza chaka
Halafu ukiitwa mbaguzi ukatae. Hivi wewe na akili zako finyu umeona clip inayozagaa inayoonyesha mfalme zumaridi akiwa brain washed watoto wenu wa kitanganyika? Sasa kiongozi wa serikali anatowa tamko juu ya kuwalinda wadanyika wenzenu na huridhiki na badala yake unaleta ubaguzi wako. Ama kweli mdanyika ni mdanganyika tu!
 
HATUDANGANYIKI!!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hizi hoja peleka kanisani zijadiliwe na ppengo
 
Nimemsikia mwandishi wa habari kanjanja wa Ayo TV analalamika Zumaridi kujiita mungu!
Ukiachalia mbaya hili sio kosa kwa sheria za nchi hii huyu mwandishi wa habari hajui hata kuficha hisia za upande wake katika kazi yake.
 
Back
Top Bottom