GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Yote ni majeshi, lakini Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ni linatumika Zanzibar pekee na Polisi linafanya kazi pande zote za Muungano.
Kwa uelewa wangu, JKU ni kama ilivyo JWTZ.
Japo JWTZ na POLISI yote ni majeshi, lakini kwa mtazamo wa watu wengi, hasa Watanyika(sijui Sheria inasemaje katika hilo), JWTZ linaizidi Polisi kwa hadhi.
Kwa muktadha huo basi, JKU kule Zanzibar inaweza kuwa na hadhi iliyo nayo JWTZ upande wa Tanganyika?
Nauliza hivyo kutokana na tukio lililowahi kutokea kule Zanzibar, la askari wa JKU kuvamia kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ambacho ni Kituo Kikubwa cha Polisi cha Unguja Mjini, na kushikilia mateka askari Polisi aliyemkamata mwenzao kwa kosa la kukiuka Sheria ya usalama barabarani.
Ujasiri wa kukivamia kituo Kikuu cha Polisi waliutoa wapi? Hapo ndipo kulipo na ofisi kuu ya Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi. Kwa hiyo ni sawa kusema walivamia makao makuu ya Jeshi la Polisi Mjini Magharibi.
Walikuwa na silaha nzito kuzidi za Jeshi la Polisi?
Kati ya Jeshi la Polisi na JKU, lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?