Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

sisemi mengi sasa na nyodo za kina uneducated makamba,phony & unqualified Nchimbi,200yrs old Kawawa,out of touch Lowassa na mafisadi wengine naona zimenipa steam ya kutosha to do something right...its hard to believe hiki ndio chama tawala na tunasubiri kitatuongoza vizuri kwa haki na kupata maendeleo hii karne ya 21,kuanzia leo nitafanya kila niwezalo kuing'oa CCM na nitaanzia jimboni kwangu kwenye nafasi ya ubunge...i'll use every weapon to my disposal kuanzia money,brain,influence,time etc,kukubali kutawaliwa na kushindwa kila chaguzi na CCM sasa ni kitu kisichokubalika na siamini kama hawa ni soooo smart kuendelea kutushinda...kila mtu afanye kitu sio kulalamika hapa tuu!


Mkuu,

Kila la kheri,kila mtu ana uwezo wa kufanya at least something.Kama mimi jimboni kwangu na kuambia CCM haipenyi 2010.Tutaona huo moto,na ni lazima hata kama si leo usambaae Tanzania nzima,CCM nasema wanapumua pumzi ya mwisho,hata wale wanamapinduzi wa kisasa na wanaotaka kuijenga nchi ya kanaani wajitokeze na kutuunga mkono.CCM si dola ya Roma,hata kama ingekua bado ingeporomoka tu kama Roma.Their days are numbered
 
Ni nape yule yule brazameni alikuwa anasomeshwa COVENTRY na Salmin Amour au mwingne?

Hivi alikosa dili zaidi ya kuingia kwenye siasa?
 
walikuwa wanamkejeli...moto ndo huo hata uanachama wanataka kumvua.. kazi ipo
 
wadau hebu tuhabarishane,hivi ni kweli kuwa CC imemchinjia Nape baharini na kubariki mkataba wa jengo la UVCCM?

Wakuu,

Unajua nimegundua tukitaka kuharakisha kifo cha CCM kwa mtindo huu ni rahisi sana.

Wale woote ambao wanataka mabadiliko ya kweli na wanatamani radical changes,basi jiungeni na CCM kwa lengo moja TU nalo Ni KUIUA.Ingia simamia ukweli,jenga influence maanke na jua CCM kuna watu wasafi pia tena wengui tu,basi watu kama akina Kingunge na Makamba,Nchimbi nk. wataamua kukushughulikia utakapoibuka na kui-defend ishu serious kwa maslahi ya Taifa.Hapo sasa usikubali kupoa au kutoka kimya kimya bali make sure wafuasi wako wako tayari kwenda na wewe popote.Nakuambia CCM hawatakuvumilia na pia in return wanachama hawatavumilia umafia mtakaokua mnafanyiwa kila mara
 
walikuwa wanamkejeli...moto ndo huo hata uanachama wanataka kumvua.. kazi ipo

Ngioja waone,na mimi namshauri Nape asikubali kulala mpaka kieleweke.Watu wasijifanya wao ndiyo Mwamba ulioshikilia taifa Letu.Shame on them!
 
Mkuu,

Nimefurahishwa sana na huu ujumbe wako.Count me in Buddy. Najua hapa JF pia kuna vijana wengi wenye Uchungu na nchi ambao wangetaka kuona mabadiliko,tuanzishe Vuguvugu kubwa la mabadiliko,kama mimi sasa naanzisha Waridi Movement for Change-Tanzania(WMC-Tanzania) na tunataka kuungana na wazalendo wa tawi la New Delh na vitongoji vyake la New Liberation Movement-Tanzania(NLM-Tanzania)

Wakuu wote wenye moyo wa dhati wa kulikomboa taifa letu kutoka ktk makucha ya mkoloni Mweusi tunaomba mtuunge mkono

Am over 50 naruhusiwa kuunga mkono?????
 
Masatu,

Nape alikuwa sahihi ila timing ilikuwa mbaya. Angengoja wampitishe kwanza!

Tatizo la viongozi wetu bongo kukosa washauri wa kisiasa.


Sure..ukionesha msimamo mkali from the very genesis they are likely to eliminate you mapema sana!

Binafsi the first spot namwona Nape anaongelea zile inshu B4 mchakato then nikajua this fella hatofika mbali despite the fact that 'he was right!

If cant be against them..them be with them and finally be against them.

To oust him suppose angekuwa ndani ya system ingekuwa ngumu kidogo!

Poor Nape...Poor CCM....Poor 'we'..i mean the citizens.
 
Nape asikubali kupoa.Apambane mpaka mwisho ,ukitaka kumkomoa Nyang'au ni kupambana nae hadi mwisho ingawa utajeruhiwa,na mwisho atoke ajiunge na Upinzani.Nadhani hata CHADEMA kuna kufaa zaidi ambako ni tanuru la mafisadi
 
Hapo ipo kazi, yaani hawaoni taabu, CCM wanajua kuwa wao ndiyo wao haku mwingine zaidi, Hawaoni shida hata kama wakimfukaza huyo mpiganaji, wanajua kuwa wao ni washindi siku zote.
 
Am over 50 naruhusiwa kuunga mkono?????

Mkuu wangu,

Karibu sana .Si unajua penye wazee hapataharibika neno? Hata JK Nyerere peke yake tusingemsikia pamoja na yale aliyoyasimamia kumwondoa mkoloni mweupe.

Leo hii tunapopigani mabadiliko makubwa katika taifa letu tukufu,kumtoa mkoloni mweusi katika himaya yake ya udhalimu ni lazima tupokea ushauri na moral support kutoka kwa wazee ambao wanatamani kuyafaidi matunda ya uhuru wakiwa kivulini.


Karibu sana mkuu wangu,heshima iwe na we Daima!
 
Ngioja waone,na mimi namshauri Nape asikubali kulala mpaka kieleweke.Watu wasijifanya wao ndiyo Mwamba ulioshikilia taifa Letu.Shame on them!

ushauri wako tutaupokea lakini kumbuka kauli ya "CCM ina wenyewe"!!! hiyo dhana ya chama chetu haipo
 
Wana JF, mtasema saana na kuchanganyikiwa.

CCM imeingiwa na confusion ya hali ya juu na sasa wanachapana wenyewe kwa wenyewe!
CCM hii ina utungu, inakaribia kuzaa na punde itazaliwa CCM nyingine!
Kutimuliwa kwa Nape ni ujumbe murua kwa Spika Sitta, Mh. Anna Kilango-Malecela, Mwakyembe na wengineo wenye mlengo chanya!
Tusubiri CC na NEC, watachapana tena!
 
Lakini kuna walioko ndani yake ambao pia wanajihisi si wenye Chama....Bora apambane na hao wahuni halafu baadae aje aungane na wanamapinduzi wenzie nje yua chama najua CCM wakiona amewachachafya sana nje ya chama watamfuata tena ili arudi,na ingekua mimi ningerudi tena kwenda kuwamaliza kabisa,hapo unabii utatimia
 
Wana JF, mtasema saana na kuchanganyikiwa.

CCM imeingiwa na confusion ya hali ya juu na sasa wanachapana wenyewe kwa wenyewe!
CCM hii ina utungu, inakaribia kuzaa na punde itazaliwa CCM nyingine!
Kutimuliwa kwa Nape ni ujumbe murua kwa Spika Sitta, Mh. Anna Kilango-Malecela, Mwakyembe na wengineo wenye mlengo chanya!
Tusubiri CC na NEC, watachapana tena!
ndio maana Nyerere aliwahi kusema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na hizi ndio dalili
 
Wana JF, mtasema saana na kuchanganyikiwa.

CCM imeingiwa na confusion ya hali ya juu na sasa wanachapana wenyewe kwa wenyewe!
CCM hii ina utungu, inakaribia kuzaa na punde itazaliwa CCM nyingine!
Kutimuliwa kwa Nape ni ujumbe murua kwa Spika Sitta, Mh. Anna Kilango-Malecela, Mwakyembe na wengineo wenye mlengo chanya!
Tusubiri CC na NEC, watachapana tena!

Mkuu Ibrah,

Sasa hapo ndipo unabii utatimia.Roma haikudumu milele.
Kinachohitajika sasa hapo ni hamasa kubwa ya wanachama kumtetea Nape,pia kundi la watu liberal ndani ya chama hicho linaweza kuchochewa zaidi na watagawanyika na kuanguka kirahisi. Hawa wazee waliokosa Dira wanajifanya wana uzalendo hii Club ya mafisadi kuliko Taifa.wakumbuke mali ya UVCCM yalitokanana kodi za mababu zetu,baba na mama zetu.So wasiweke maslahi yao na club yao mbele.

Nape pambana
 
Jamani hivi habari kwangu ni ngeni hivi ni kweli amavuliwa uanachama au atachukuliwa hatua zingine tu za kinidhamu kwa ajili kutoa siri za chama kwenye vikao ambavyo sio rasmi.

Kama ni kweli basi wamemuonea kijana wa watu. Kwa nini wasimuenzi hata baba yake
 
Jamani naanza kupata uoga.wasije wakamtoa roho huyo kaka jamani.maana nawaogopa hawa watu wanaojifanya wao ndio wenye nchi.
 
Sasa CCM wanaogopa hata vivuli vyao!! Nani atakuwa anaipinga CCM ndani ya CCM?
 
Jamani hivi habari kwangu ni ngeni hivi ni kweli amavuliwa uanachama au atachukuliwa hatua zingine tu za kinidhamu kwa ajili kutoa siri za chama kwenye vikao ambavyo sio rasmi.

Kama ni kweli basi wamemuonea kijana wa watu. Kwa nini wasimuenzi hata baba yake



Mkuu,

Wafanye yote lakini wasiiguse roho ya huyo kijana......Eti,CCM wamuenzi tena baba yake?


Mkuu,utashangaa na hata wakifanya hivyo hata mie nitashtuka sana.Ni lugha ya kigeni kabisa
 
Back
Top Bottom