Duh! Hii CCM ndiyo mufilisi kabisa 🙁 Badala ya kumkumbatia Shujaa Nape wameamua kuwakumbatia mafisadi akina Lowassa na mafisadi wa kihindi. Mafisadi wote wa EPA, Richmond, Rada, Ndege ya Rais, Helicopters na magari ya jeshi bado wamekumbatiwa ndani ya chama hicho!! lakini mpambanaji wa mafisadi ndiyo wa kumfukuza!!! Sasa tumepata uthibitisho rasmi kwamba kweli CCM ni Chama Cha Mafisadi na hawastahili kabisa kuwepo madarakani kwa kuwa matatizo yetu mengi Tanzania yanasababishwa na CCM. CCM ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya Tanzania.