Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Wakizungumza katika mkutano wa Baraza hilo lililofanyika mjini Dodoma jana, wazee hao Katibu wa CCM, Yusufu Makamba, Kaimu Kamanda wa Vijana, Kingunge Ngombale Mwiru na Mshauri wa Vijana Mzee Rashid Kawawa waliwaonya wagombea wote na wapambe wao kuacha kukikosoa chama hicho badala yake wawe wapole.

Oneni hawa wazee wanacho sema hapa hii ni wazi ukiwa ndani ya CCM huna haki ya kukemea maovu.

Akizungumza kwenye baraza hilo, Makamba alisema kuwa kijana yeyote anayependa kukikosoa chama hafai kuwa kiongozi kwani kila anayetaka kuwa kiongozi ni lazima awe mpole na akubali siku zote kuwatii wakubwa.

Huyu Makamba hivi ni kweli kiongozi au anasifa za kuwa kiongozi kweli ??Hii inakumbusha kuwa mkubwa sikuzote hakosei ikidhihilika kakosea aaah basi kapitiwa.....duh kazi tunayo hawa viongozi wa kubebwa bebwa sijui itaisha lini.
 
Hiyo mbona haitishi!hawa UVCCM wamechemsha,

Nimemsikia Fransis Isaack Akiongea kwa Jazba kwenye Power Break fast,nachelea kuona nae chamtema kuni kinampata hivi karibuni.

Ndugu wanaJF hili la kumsimamisha Nape mbona wamejipalia moto wakina chimbi (Mzee wa... au Mtaalamu wa ....) nani asiye mjua?

Ni hivi:

Kesho CCM ndio wankaaa chini ya mwenyekiti wao walikuwa wanangoja atoke Safarini subirini mtana moto wake kesho. Kwa ufupi Nape bado ni shujaa haendi popote na ataendelea kubaki CCM kwani kwa wanaoona mbali katika chama hawawezi kumuchai hivi eti kisa ameingilia maslahi ya mtaamu wa... (Mh.Nchimbi).
 
Hivi ni kwa nini viongozi wa juu wa CCM wanafuata upande wa Nchimbi badala ya kumtetea Nape?? Je mzee Kawawa naye ni fisadi?? Kingunge je? Kuna mwenye kujua mali za Kingunge??? au familia yake?
 
hapa ndiyo CCM imedhihirisha ni chama cha aina gani. kinakumbatia mafisadi na hakipendi wasema ukweli. pole NAPE
 
Mali za Kingunge sio nyingi, maana kajiunga nao recently.....
 
Tatizo liko wapi? Hiki si chama chao na ni hivi wanavyotaka kukiendesha? Kama mtu haukubaliani nao au unaona umeonewa, kwa nini unabaki humo? Wenye chama wamesema usiwakosoe hadharani. Wewe unaendelea. Unatarajia nini?
 
Nchimbi afa na umri wagombea UVCCM

*Makamba 'awabwatukia' wanaoandaa mauti ya CCM

Na Joyce Kassiki, Dodoma

WAKATI Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuf Makamba akiwataka wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCC) kuacha tabia ya kukichafua chama hicho kwa kukisema vibaya hadharani, Mwenyekiti wa Umoja huo, Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka vijana hao kuchagua wagombea wenye umri unaokubalika ili kujenga timu imara .

Bw. Makamba aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM ambacho pamoja na mambo mengine, kilichuja majina ya wagombea nafasi mbalimbali za Jumuiya hiyo.


Katibu huyo, alisema kufanya hivyo ni sawa na kukiletea chama mauti kwani tabia hiyo inaweza kuibomoa UVCCM na wakati huo huo kudhalilisha chama.


Alisema Jumuiya za vijana ndio chimbuko la kupata viongozi wa juu wa Taifa hivyo vijana hawana budi kukipenda chama chao na kuepuka majungu yanayoweza kukibomoa chama hicho.


"Mambo mengine yanayofanywa na vijana ni mauti kwa chama,kuisema Jumuiya ni kuibomoa Jumuiya hiyo na chama kwa ujumla halafu baadaye tutakosa viongozi mahiri wanaoweza kuongoza nchi,"alionya Bw. Makamba


Awali akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa UVCCM,Bw. Emmanuel Nchimbi aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kuchagua vijana wenye uwezo wa kuongoza badala ya kuangalia sura na jina la mtu.


Alisema ili kupata viongozi wazuri watakaongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, wajumbe hawana budi kuchagua wanachama wenye umri stahili na kupima utendaji wa wagombea hao.


Akifafanua suala la umri, Bw. Nchimbi, aliwataka wajumbe hao kutomwonea haya mgombea yeyote aliyevuka umri kwani lengo la umoja huo ni kuwa na timu nzuri ya Baraza lijalo.


Aliwataka vijana kuwa na mapenzi mema na chama chao badala ya kujenga chuki na ubinafsi jambo ambalo alisema linasababisha makundi yasiyokuwa na msingi ndani ya Jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.


Kauli ya Mwenyekiti huyo imeonesha kuweka wazi msimamo wake kuhusu vuta ni kuvute kati yake na mmoja wa wagombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM, Bw. Nape Nnauye ambaye anadaiwa kuvuka umri huo.


Bw. Nnauye mwanasiasa kijana machachari, amekuwa akipinga jambo hilo na kuliona kama 'fitna za kuchongwa' dhidi yake baada ya kufichua kile alichoeleza, ufisadi mkubwa ndani ya mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha Jumuiya hiyo lililopo kando ya barabara ya Morogoro, jijini Dar es Salaam.


Katika sakata hilo, Bw. Nnauye alimshutumu moja kwa moja Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamani wa UVCCM, Bw. Edward Lowassa na viongozi wengine wa juu, kuingilia mkataba huo aliobainisha kuwa hauna maslahi kwa umoja huo.


Kauli ya kada huyo kijana, imezua mtafaruku mkubwa na migongano ya kauli ndani ya chama hicho kikongwe nchini, huku kundi moja likimuunga mkono na kutaka hatua zaidi zichukuliwe kubaini kasoro za mkataba huo na kundi lingine likipingana na jambo hilo na kumwona amekiuka taratibu za chama hicho kwa kuanika jambo hilo hadharani.
 
Jamani inasikitisha sana mpiganaji kama huyu wanamfukuza uanachama halafu mafisadi /majambazi waliobaka mali ya watanzania wanaachwa.jamani Tanzania, ni lini tutakubali ukweli?hasa hawa viongozi wetu.NAPE KAKA ANGU JIPE MOYO TAFUTA CHAMA CHENYE MSIMAMO KAMA WAKO WA KUTETEA MASLAHI YA NCHI ACHANA NA HAO MAFISADI.NA kwa hili nakwambia utabata baraka za watz kibao.
 
When are we planning for Revolution in Tanzania? We need to wake up, a few dedicated to withdraw (eliminate) hii miamba ya ssm na ssm kwa ujumla. Justice in never in ssm? huu ni ukandamizaji wa wazi kabisa. To Nape be carefully with ssm. My tears shade when i remember hero, Horace Kolimba. Those who are close to Nape mwambieni aondoke kimya na asikaribie kabisa any member wa ssm hata kama ni rafiki yake. Money is powerful as the scene is behind Lowasa na yule Subash. Do you know Subash alisoma na JK Primary school? Issue ya Nape ni complicated. Nape asitegemee kuwa hata kama ataendelea kuwa mwanachama wa ssm hatakaa apate madaraka hata ya kufagia ofisi za UVCCM na hatimaye Lumumba years to come. Thanks.
 
Amefukuzwa uanachama wa UVCCM atabakia kuwa mwanachama wa kawaida asiye kuwa na wadhifa wowote ule...
Makosa 3 anayo tuhumiwa Nape haya hapa;-
1.Kutoa tuhuma nzito za mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu la umoja huo, liliko jijini Dar es Salaam, wakati suala hilo lilikwisha kuamriwa na baraza.
2.Kutoa tuhuma hizo nje ya kikao na kukiuka ibara ya 18b ya kanuni za umoja huo.
3.Kusema uongo dhidi ya mradi huo, ambapo amevunja kanuni ya 17c.

Lakini jamani si mnakumbuka Nchimbi alisha aapa kumshughulikia huyu kijana alisema labda yeye si Nchimbi.....sasa tusubili madudu atakayo fumua Nape kuhusu Nchimbi sasa tunaamini kuwa Nchimbi naye ana % yake kwenye hilo jengo lenye utata.
 
Amefukuzwa uanachama wa UVCCM atabakia kuwa mwanachama wa kawaida asiye kuwa na wadhifa wowote ule...
Makosa 3 anayo tuhumiwa Nape haya hapa;-
1.Kutoa tuhuma nzito za mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu la umoja huo, liliko jijini Dar es Salaam, wakati suala hilo lilikwisha kuamriwa na baraza.
2.Kutoa tuhuma hizo nje ya kikao na kukiuka ibara ya 18b ya kanuni za umoja huo.
3.Kusema uongo dhidi ya mradi huo, ambapo amevunja kanuni ya 17c.

Lakini jamani si mnakumbuka Nchimbi alisha aapa kumshughulikia huyu kijana alisema labda yeye si Nchimbi.....sasa tusubili madudu atakayo fumua Nape kuhusu Nchimbi sasa tunaamini kuwa Nchimbi naye ana % yake kwenye hilo jengo lenye utata.

Hapo ndo ilipo hofu yangu, atamshughulikiaje? direct ama indirect? make mhhhhhhh.. nyoka alisha tung'ata hivo tukiona mjusi lazima tupige mbio.
 
Hiki kitu ni uhakika?

Maana naona tunaenda mbaaaali bila kupata undani wa tukio. Wamemvua kwa utovu gani wa nidhamu? Na agenda iligeuka lini kutoka uchaguzi kwenda kwenye uanachama wa mgombea?

Yebo Yebo ukipata habari zaidi tuwekee Mkuu.

Kuhani,
Habari hii bado ni 50/50 kwani source yake haiaminiki. Mimi bado nasubiri 50 nyingine from reliable source.
 
Mkuu Mwawado huyo Mwenyekiti naye pia ni fisadi anajua fika kwamba Urais kaupata kwa kutoa rushwa ya hali ya juu, na hichi ndiyo kinamfanya aogope kuchukua hatua zozote dhidi ya mafisadi. Ndiyo matatizo ya kuingia madarakani kwa njia za haramu. Kama anaona hawezi kutetea maslahi ya Tanzania kwa kuogopa naye kulipuliwa na mafisadi wenzake ni bora aachie ngazi mapema ili kuiepusha Tanzania kuangamia.
Mi siku zote nasema huyu JK si uoga tu bali na yeye ni fisadi kabisaaaaaa. Hivi mnasubiri mpaka atoke madarakani ndio mumseme kwamba ni fisadi?

Unajua hata viongozi wa seerikali wanajua ni muoga.

Kwani mmesahau hotuba fupi na makini ya Six iliyokuwa ikijibu hotuba ya muungwana ya maasa kibao isiyokuwa na kitu? Alimwambia mtu mzima shida inayomkabili ni pamoja na uoga kwa mafisadi wenzie
 
Kuhani,
Habari hii bado ni 50/50 kwani source yake haiaminiki. Mimi bado nasubiri 50 nyingine from reliable source.

Kaimu katibu mkuu wa UVCCM ameongea redioni LIVE leo. Wewe unataka mpaka JK akupigie simu?
 
Naam yamewakuta sisiemu. Yamewakuta.

Nakumbuka wakati Chadema ilipomundoa katika wadhifa na (si kumfukuza) marehemu Wangwe, hao hao sisiemu walishika bango na kushutumu chadema kwenye vyombo mbali mbali vya habari. uhakika tumeuona kupitia waraka aliozungusha Makamba mara alipofariki Wangwe.

Leo mimi nadhani afadhali hata ya Chadema maana walishutumiwa ukabila. Lakini shutuma dhidi ya sisiemu siku zote ni ufisadi, ubabe wa madaraka, na kutopenda kukosolewa. Hawa ni wabaya zaidi.
Habari ndiyo hiyo
 
Nape ni shujaa na CCM wameshakuwa mafisadi wanaogopa vivuli vyao...yaani wanona heri wamkumbatie lowasa na upumbavu wote alioufanya wanamtosa mwanamapinduzii aliethubutu kuwakemea?

CCM mnakwenda wapi jamani.....kwani mnafikiriaa bila lowasa,na mafisadi wengine kina nchimbi nchi haitaenda ??kwa nini mnawakumbatia?? Nahisi kuna kitu kikubwa sana kitafuata soon maan najua hata jeshi limechoka na longolongo......nguvu za fikra zinahitajika...kikundi kidogo cha watu kinaendesha nchi kubwa hivi kwa matakwa yao hakuna wa kuwanyoshea kidole inauma sanaaaaaa
 
NGUVU YA UMMA TUINDAE 2010. KAMA Chechescu NA WSOSHALIST WALITOKA SEMBUSE CCM? KAMA APARTHEID ILIANGUKA TUSHINDWE KUKATA NA KUANGUSHA CHAMA CHA MAFISADI? KIJANA MWENZANGU JIULIZE, VOTING BLOCK YA VIJANA INAWEZA KUIONDOA CCM 2010. OBAMA KAWEZA KUITENGENEZA HII UNDERUTILISED VOTERS BLOCK. SHIME VIJANA WENZANGU.TUPAMBANE KUAKIKISHA CHAMA HIKI HAKIPATI JAPO WINGI WA WABUNGE HAPO TUTAKUWA TUMEWAPIGA BAO.THEN TUTAANZA SAFISHA SAFISHA TUKIANZIA NA KATIBA. THIS TUNATAKA KATIBA KUJENGWA NA UMMA NA SI CCM. SHIME VIJANA KWA NINI TUSIANZISHE PRESSURE GROUP YA KUHAKIKISHA VIJANA WANAJIANDIKISHA KWA WINGI. WIKI JANA, NIMEPATA KUTEMBELEO OFFICE ZA CAMP YA OBAMA, KUNA MIKAKATI MIZURI NIMEPATA . BADALA YA KUPIGA KELELE AMBAZO HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI, TUPANGE MIKAKATI YA 2010 KISHA TUWEKE LENGO LA JUU NA LA CHINI.
NAOMBA KUWAKILISHA. ( sorry for the caps)


Mkuu,

Nimefurahishwa sana na huu ujumbe wako.Count me in Buddy. Najua hapa JF pia kuna vijana wengi wenye Uchungu na nchi ambao wangetaka kuona mabadiliko,tuanzishe Vuguvugu kubwa la mabadiliko,kama mimi sasa naanzisha Waridi Movement for Change-Tanzania(WMC-Tanzania) na tunataka kuungana na wazalendo wa tawi la New Delh na vitongoji vyake la New Liberation Movement-Tanzania(NLM-Tanzania)

Wakuu wote wenye moyo wa dhati wa kulikomboa taifa letu kutoka ktk makucha ya mkoloni Mweusi tunaomba mtuunge mkono
 
Masatu,

Nape alikuwa sahihi ila timing ilikuwa mbaya. Angengoja wampitishe kwanza!

Tatizo la viongozi wetu bongo kukosa washauri wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom