Nimeamsikia Nchimbi akisema kijana huyo hatapita,labda yeye siyo Nchimbi
Hivi bado yuko India huyo kijana?
Maana ni heri abaki huko huko kwani kila aliyetangaza kugombea Uenyekiti wa UVccm...Basi Nchimbi aliwashughulikia.
Sasa wamesahau ya Chifupa.
Hata hivyo ni hatua nzuri..Ila utekelezaji wake utaiyumbisha ccm establish kwani huwezi kohoa kwa wanamtandao ndani ya ccm la sivyo wata kukolimba!
Wamesahau hata wabunge wenyewe wanasuwasuwa?
Ndio iwe mtu anayepiga kelele kwasababu tu anataka uongozi?
Hawa watu hawajuwi ccm imekufa?
Wasifikiri eti Nape Nnauye ndiye atakayekikomboa chama...Anahitaji ushirikiano.
Yeye anampigia kelele mtu ambaye hata mwenyekiti wa chama kamshindwa na hata NEC yenyewe ni mafisadi.
Mi naona ni kelele za kampeni tu!
Unless aungwe mkono na viongozi wakuu wenye ushawishi na ama wale wasiokuwa mafisadi!
Kwani tumeona kuwa mafisadi wana influence kubwa na ndio maana mara baada ya kashfa zote waliwatumia hao hao kina Nape na wengineo walioko UK kufuguwa matawi ya kuendeleza libeneke la UFISADI KWA STYLE YA KIMATAIFA!
Kama wana nia nzuri wafanye mapinduzi na sisi tutajiunga!
Lakini hizo kelele eti kwasababu tu ni mtoto wa Nnauye kasema...Ama mtoto wa Kawawa nk...Hilo halina mantiki!
Kama ni ufisadi ushapigiwa kelele sana tu na hadi CHINGA NA WALALAHOI NA HATA WANAFUNZI WANAUJUWA NA WALISHA MZOMEA HATA MKAPA NA MAKAMBA...
Bado zamu ya JK.
Na hao kina Nape pia wawe makini wasilete POLITICS KWANI WATAUMBUKA!