Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Hapo ndipo mizizi itapochimbika kama itakuwa kweli, sijui kama hizo ndoto zitatimu, lakini waache wafu wazikane wenyewe.
 
Ahaaa haaa, ilikuwa zamani siku hizi huo ubavu hana kwa sababu akina JK walishamtumia na hawana shida naye tena! Huyu Nape ana nafasi kubwa sana, and, to be honest, he could the best among those who have declared their intentions so far!.

Taasisi ya umoja wa vijana ni bora kuliko maslahi binafsi ya watu wachache,ili taasisi iweze kuwa imara ni lazima haki itendeke na pia wote wanaotendewa haki hio waione,ushindani wa kushindana na hasiye shindana ni sawa na kuchanganya wakimbiaji wa special olympic na wa olyympic ya kawaida...lakini msingi wa mashindano yoyote ni ushindi na mbinu za kufikia ushindi huo ni tofauti na kwa wanasiasa waliokomaa wanapaswa kuwavumilia vijana wanapojifunza siasa na huko ndiko kulea vema.
 
Mkuu Gembe,

mbona kauri hizi zinafanana na za kule kwa Jongwe (Robert Mugabe)! Hivi yale makeke ya Tanzania na Demokrasia yako wapi?
hapo naweza kusema kuwa "unamuwazia,unamtungia,unamsemea then unamuhukumu kwa kusema mambo ambayo umemsemea wewe.hapo hakuna haki ambayo wote mnaililia hapa.
 
Ahaaa haaa, ilikuwa zamani siku hizi huo ubavu hana kwa sababu akina JK walishamtumia na hawana shida naye tena! Huyu Nape ana nafasi kubwa sana, and, to be honest, he could the best among those who have declared their intentions so far!.

Huyu ameanza kama Wangwe tofauti yao ni shule. Naona tumuite Nape kuwa ni Wangwe wa UVCCM.
 
Kitila,
Kila mtu anataka Nape Apite,ila kuna kitu nyuma..hawampendi nape..so fara waliochukua Fomu ni kama ifuatavyo

1.Jerry silaa
2.Musa Mnyeti
3.Beno Malisa


wengnie sifahamu...

Kwa wanaomfahamu Jerry Silaa, je ana uhusiano wowote na Dr. Slaa? Just curious.
 
Kwa wanaomfahamu Jerry Silaa, je ana uhusiano wowote na Dr. Slaa? Just curious.
Kubwa jinga bwana,

Dr. W. Slaa
Jerry Silaa

hope you have seen the difference.hawana uhusiano wowote zaidi ya ule wa kufanana herufi za majina yao
 
Kubwa jinga bwana,

Dr. W. Slaa
Jerry Silaa

hope you have seen the difference.hawana uhusiano wowote zaidi ya ule wa kufanana herufi za majina yao

Gembe,kwani umesahau kama jina lake ni KUBWAJINGA
HAHA!
 
Akizungumza muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, Nape amesema kuwa Lowassa na nchimbi wanahusika na mkataba wa kifisadi wa mradi wa kuendelea jengo mla umoja huo katika eneo la Lumumba, Dar es Salaam.

Amesema kuwa mwekezaji aliyepewea kuendeleza jengo hilo amepewa umiliki wa asilimia 75 ya hisa wakati umoja huo ukibakiwa na hisa 25 tu wakati mwekezaji huyo hakutoa hata senti moja katika mradi huo.

Alisema alichofanya mwekezaji huyo (ambaye hakumtaja) ni kutumia hati za umiliki wa jengo na kiwanja hicho kuombea mkopo benki ambao anautumia kuendeleza jengo hilo.

Amesema kinachosikitisha zaidi ni sehemu ya mkataba huo kinachoeleza kuwa makubaliano hayo ni ya masiaha, ikimaanisha kuwa familia ya mwekezaji huyo itaendelea kula fedha kupitia mgongo wa Umoja wa Vijana wa CCM.

Amesema kama vile ambavyo viongozi wa UWT na WAZAZI walivyowajibishwa kwa kushindwa kusimamia mali za jumuiya hizo, lowassa na nchimbi nao wanapaswa kuwajibishwa au kuwajibika kwa kushindwa kusimamia maliz a UVCCM.

Nape amesema kwua ameamua kuwania nafasi hiyo ili kukisafisha chama kutokana na kuchafuliwa na mafisadi.

So long as hii issue haina maslahi ya Taifa bali ya CCM wenyewe sioni taabu sana. Waache waibiane tu. Ukiwa mwizi ni mwizi tu, hujui vya nyumbani wala jirani....eeh Mola tuokoe na hili janga!
 
Kama mama Malecela mwenyewe na Influence yake na kuwepo pia bungeni alishindwa kukohoa..Huyo naupe anataka kusema nini nje ya bunge?

Hizi ni siasa za kukifufua chama cha mapinduzi!

Hatuhitaji vijikada vya ccm vitueleze namna ya kupambana!

Apige kelele ripoti za Ufisadi zitolewe na si kudai waachie ngazi kwenye chama!

Nani kasema chama kina nguvu zaidi ya KATIBA?

Sheria hapa ikishafanya mambo yake..Basi hata Nape na yeye hatapata shida!

Hivyo mimi kwangu hizi ni propaganda za chama za kisiasa!
 
Anacheza huyo, akiingia huko kwanza atategewa mtego mdogo tu wa kupewa pesa au kutafutiwa pesa na kupewa na kuingizwa kwenye kundi lao na yeye atakuwa kimya. Ndivyo wanavyosema wakiwa wanatafuta nafasi wakiingia, mwendo mdundo.
 
Ina maana katumwa na wapinzani kama vile wangwe alivyotumwa na ccm?
Be specific pls.


Kwa ile mentality iliyomuondoa Wangwe, CCM nao wana haki ya kuchagua mchawi. Labda watasema Nape alionekana Bilcanas akiwa na Mbowe.
 
duh! huyu jamaa kajua labda hawezi kupita, akaona potolea mbali wacha atume ujumbe!
 
Bora hili jengo watapeliwe kama CCM walivyotutapeli Wadanganyika nakutaifisha mali za umma kwa kisingizio kwamba ni mali za CCM.
 
Mwenyewe anaahidi kwua safari hii yuko determined kuhakikisha kuwa anasafisha uchafu ndani ya chama. Sijui kama ni dhamira ya dhati au maneno ya kuombea kura tu. Tusubiri tuone
Nape peke yake hawezi.Anahitaji nguvu ya Frank Uhaula.
Ukimtamkia Nchimbi hilo jina anakuwa mdogo.Nape akumbuke yaliyotokea siku za nyuma kwani yeye si mara yake ya kwanza kuingia kwenye hicho kinyang'anyiro.
Awe makini this time.
 
Swali kwa Nape, huo ufisadi ameujua leo au kaujua toka zamani? kama ana mapenzi mema na chama kwannini hakuanza kuåingana nao tangu hapo awali ili tumuone shujaa basi na hata kura zetu angepata bila nguvu yoyote. Hii style aliyotumia tuita siasa za abunuwasi tu, hakuna lolote atakalofanya, hapa anaanza kujiwekea mirija ya kuja kunyonyea hapo baadae kama akibahatika kuupata huo u-wenyewekiti. Baadae atakuja na ile ile style ya Rostam ukisema nakulipua!!
 
Mwenyewe anaahidi kwua safari hii yuko determined kuhakikisha kuwa anasafisha uchafu ndani ya chama. Sijui kama ni dhamira ya dhati au maneno ya kuombea kura tu. Tusubiri tuone

Anaweza akafanikiwa kwani wapo wengi ndani ya CCM na hata UVCCM waliochoshwa na vitimbwi vya akina EL, RA na hata JK.

Keep it up Nape boy. Usibadilishe msimamo hata ukishindwa. There is future in what your belief is positioned at.
 
Back
Top Bottom