Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Nape peke yake hawezi.Anahitaji nguvu ya Frank Uhaula.
Ukimtamkia Nchimbi hilo jina anakuwa mdogo.Nape akumbuke yaliyotokea siku za nyuma kwani yeye si mara yake ya kwanza kuingia kwenye hicho kinyang'anyiro.
Awe makini this time.

Kaka huijui historia ya umoja wa vijana wa ccm, Nchimbi hawezi kumuogopa Frank Uhaula.mwaka 1998 wakati nchimbi akitoka tu shule alikutana na frank uhaula kwenye uchaguzi huo.

Pamoja na uhaula kupigiwa kampeni nchi nzima na moses mnauye yani baba yake nape,bwana frank alichapwa kama amesimama...mwaka 2003 alimsaidia nape,haikumsaidia nape,hapo bwana nape alichapwa kama amesimama.

Kwa mara nyingine tena Nape amepanua wigo wa wapinzani.....nchimbi nyamaza...usifadhaike moyo wako...maneno ya nape tutalipiza kwa niaba yako..nape atalipia...nitapigana vita hii kwa niaba yako.nitapigana bila kuchoka....vita hii si yako ni vita ya wana ccm wote..vita hii si yako ni vita ya wana uvccm wote..ni vita mpya dhidi ya nape na kundi lake dhalimu la kina fieldmarshal, Malecela etc.
 
While we are discussing Ridhwani does anyone know who the other contestants are? one name has popped up 'Jerry'
 
Nchimbi amekataa kulizungumzia hili. Anasema masuala hayo aulizwe katibu mkuu wa UVCCM. Anasema Lowassa, ambaye ndiye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya jumuiya naye hapaswi kuulizwa kwa sababu katibu wa jumuiya pia ndiye katibu wa bodi ya wadhamini na ndiyo yenye dhamana na mali za jumuiya. Anasema kwa utaratibu, katibu wa bodi ndiye mtendaji mkuu, hivyo aulizwe yeye
 
Kaka huijui historia ya umoja wa vijana wa ccm, Nchimbi hawezi kumuogopa Frank Uhaula.mwaka 1998 wakati nchimbi akitoka tu shule alikutana na frank uhaula kwenye uchaguzi huo.

Pamoja na uhaula kupigiwa kampeni nchi nzima na moses mnauye yani baba yake nape,bwana frank alichapwa kama amesimama...mwaka 2003 alimsaidia nape,haikumsaidia nape,hapo bwana nape alichapwa kama amesimama.

Kwa mara nyingine tena Nape amepanua wigo wa wapinzani.....nchimbi nyamaza...usifadhaike moyo wako...maneno ya nape tutalipiza kwa niaba yako..nape atalipia...nitapigana vita hii kwa niaba yako.nitapigana bila kuchoka....vita hii si yako ni vita ya wana ccm wote..vita hii si yako ni vita ya wana uvccm wote..ni vita mpya dhidi ya nape na kundi lake dhalimu la kina fieldmarshal, Malecela etc.

Whaat? Can you clarify please!
 
So long as hii issue haina maslahi ya Taifa bali ya CCM wenyewe sioni taabu sana. Waache waibiane tu. Ukiwa mwizi ni mwizi tu, hujui vya nyumbani wala jirani....eeh Mola tuokoe na hili janga!

Ninavyofahamu mali ya CCM ni mali ya watanzania wote iliyonyakuliwa na CCM na wanaoifaidi ni CCM peke yake.
 
I hope Nape hajachukua hela toka kwa Rostam, kama Mtikila,

Lakini otherwise ni mwanzo mzuri huu aliouanza, piga nyoka kichwani bila kujali where the chips may fall, Tanzania tunahitaji wanasiasa kama huyu bwana mdogo wanaoweza kuita Spade a Spade,

Sio akina Pinda, wanaotuambia Meremeta ni mali ya jeshi huyu kijana hata akishindwa tutajua ni uzembe wetu wananchi lakini ukweli uko wazi kuwa kwa mara nyingine tena Lowassa na Nchimbi, yaani wale wale ni mafisadi hata huko kwenye UV-CCM, sasa ni wakati wa wananchi werevu wa siasa kuanza kumpa msaada huyu kijana kwa sababu kwanza anajua mengi na atasema mengi sana mpaka huu uchaguzi uishe,

Mimi nitampa mchango wangu kumsaidia asonge mbele, maana huyu ana ubavu huyu wa kusema wazi, ambao wengi bongo hatuna, kuanzia wananchi mpaka viongozi wetu na hasa wanaotuambia kuwa Lowassa alionewa, so much na kuonewa, Fisadi bwana kila mahali yeye ni ufisadi!

Sasa wale watetezi wake Lowassa hapa vipi na hizi shutuma za Nape? Au naye ametumwa na Mwakyembe kumuonea Lowassa?

Bravo Nape!
 
Ningependa kwanza Bwana Nape (MNEC-CCM),aniondolee shida ninayopata kufuatia tuhuma nzito (kama ni kweli) alizozitoa kwa uongozi wa UVCCM na kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa UVCCM Mh.E.Lowasa.

Kimsingi ni tuhuma nzito sana ambazo kwa kweli zinapaswa kuangaliwa kwa undani sana.
Sina tatizo na hatua ya bwana Nape kutoa madai ya kuwatuhumu wahusika.Ni haki yake ya msingi.Lakini pia ni jambo jema haswa kama ni madai yenyewe ni ya kweli. Lakini maswali yangu yanajikita katika maeneo yafuatayo?

1.Mnauye ni mjumbe wa baraza kuu la UVCCM.je alishawahi kuhoji na kuomba kupewa ufafanuzi juu ya madai hayo ndani ya kikao halali na kukubwa kwa mujibu kanuni ya UVCCM?
2.Nape Mnauye,pia ni mjumbe wa NEC ya CCM.Je, kama kwa sababu moja ama nyingine alishindwa kuwasilisha hoja au madai yake hayo mbele ya baraza kuu la UVCCM,aliweza kuwasilisha madai hayo mbele ya NEC au uongozi wa chama kwa hatua za uchunguzi zaidi? Kwa sababu ni muhimu kufahamu kwamba jumuiya zote za CCM ziko chini ya CCM.Na kama kuna ukiukwaji wa maadili katika jumuiya husika,CCM inaingilia kati.Tumeshuhudia haya kwa jumuiya ya Wazazi na Wanawake(UWT).
3.Mwisho nadhani bwana Nape anafahamu kwamba kwa mujibu wa muundo wa jumuiya ya UVCCM,Mwenyekiti hawezi kufikia maamuzi mazito yeye binafsi bila vikao husika.Kwa hiyo kama ni tuhuma, basi ningeelewa zaidi kama angezielekeza kwa kamati nzima ya utekelezaji ya baraza kuu la UVCCM .Na angetoa wito kamati hiyo ijiuzuru.

Lakini pia kwa utaratibu,kamati ya utekelezaji nayo lazima iwasilishe mapendekezo yake kwa baraza kuu kwa baraka zake,ambako Nape ni mjumbe.Kwa hiyo kama baraza kuu lilibariki madai yanayotolewa ,basi bila shaka na yeye Nape ni sehemu ya maamuzi hayo.Kwa hiyo hata yeye anawajibika.

Iwe aliunga mkono hoja au hakuunga mkono hoja,ukweli unabaki kuwa naye alikuwa sehemu ya maamuzi kwa mujibu wa kanuni na taratibu za vikao. Sasa kama hakuridhika na uwajibikaji wa pamoja,basi njia pekee ya kunishawishi niamini kuwa anania ya dhati ya kuleta mageuzi ndani jumuiya,basi alipaswa kujiuzuru ujumbe wake wa NEC alioupata kwa tiketi ya UVCCM,kutokana na kutoridhishwa na ukiukwaji wa maadili,kanuni na taratibu ndani ya UVCCM.

Sasa anapokuja na madai hayo mazito wakati wa kuchukua fomu za kuomba uongozi,kunanipa tabu sana kushawishika kuamini kama kweli dhamira yake ni kuleta mapinduzi ndani UVCCM.Vingenevyo nashawishika kuamini kuwa huu waweza kuwa ni mkakati maalumu.
 
......cha muhimu hapa ni kama kuna ukweli wa shtuma zake dhidi ya Lowassa na Nchimbi,

na hawezi yeye kama mjumbe wa NEC kukurupuka na accusations znito namna hii, ya vikao sasa tumechoka maana kule kuna kina Serukamba, sasa dawa ni hii kama ya Rostam kwa Mtikila, ni kumwaga hazarani wanaachi tuamue ukweli na uongo ulipo!

Bravo tena kwa Nape.
 
Who does Nchimbi think he is au anapanga kumu-ipyana??

...Heri mimi sijasema...

Lakini tutaiogopa hii mpaka lini? afterall Mungu wetu ni mkuu kuliko wote and for sure yuko upande wa ukweli, kweli tupu itashinda.
 
Vikao vya nini kama havileti mapinduzi ya kweli?watu wamekuwa wajanja siku hizi kama ana habari ya kweli anamwaga tu,maana huko vikaoni wajumbe wananuliwa mapema kabla ya vikao.
Kuna miungu watu nchi hii.Majengo maarufu ya vitega uchumi analazimisha kwa cheo chake kuwa na hisa,Hawatosheki nata vitalu vya kuwinda wanyama anahodhi mtu yule yule.Kila mradi mkono wake upo.NAPE mwaga vitu,furumusha hata yale yaliyosalia
 
Ningependa kwanza Bwana Nape(MNEC-CCM),aniondolee shida ninayopata kufuatia tuhuma nzito (kama ni kweli) alizozitoa kwa uongozi wa UVCCM na kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa UVCCM Mh.E.Lowasa..

Du, Yaani kuna watanzania bado wanamwona Lowassa ni MHESHIMIWA.....heshima ya nini? Kweli fikira za ubepari uchwara ni tatizo kwetu..

Tanzanianjema
 
Du, Yaani kuna watanzania bado wanamwona Lowassa ni MHESHIMIWA.....heshima ya nini? Kweli fikira za ubepari uchwara ni tatizo kwetu..

Tanzanianjema

Unajua tatizo la hawa wanaCCM ni kuamini kuwa hata kama mtu amekosea lakini wadanganyika hawatauliza makosa wakipewa sh. 2000 tu basi wanapiga kura, kumbukeni sherukamba ambaye alithubutu kusema kuwa wananchi hawatauliza RDC bali watauliza utekelezaji wa ilani ya CCM.

Hawa wanatuona watanzania kama wajinga tusiojuwa wajibu wetu, but the time has changed masha was asked about Deep Green Finance by his votters last month ikabidi aitose serikali kauli ambayo hadi leo serikali haijakanusha kama yuko sahihi au amekosea, wezi wa pesa za wananchi ni serikali yenyewe kupitia CCM.

Kwahiyo wakiibiana wenyewe kwenye mikataba mibovu ya majengo yao hilo sio tatizo kwani litawatafuna wenyewe.

Wakumuonea huruma ni huyo kijana aliyeropoka bila kuangalia kuwa White shark amepanua mdomo wake akisubiri mawindo yake yaingie ndani ya mdomo. He may be the next balali kama hakuwa makini.
 
Wandugu,

Naomba Cv ya Nnauye.

Zaidi ya kuwa ameshiriki kikamilifu kufungua Tawi ya CCM India, sijui kingine alichokifanya.

Pia, 2005 alikuwa kambi ya ip, Mtandau au ile zile nyingine?

Kitumia Neno Fisadi kunaweza kumuharibia; sababu CCM wanalikataa hili neno kwa sababu limeazishwa na Chadema.
 
Yeye kama ana akili timamu anatakiwa aandae ajenda na namna jinsi atakavyoongoza UVCCM. Na sio kuwashambulia watu ambao kisiasa bado ni wakubwa kwake naweza kusema pia huyu atakuwa amekurupuka na huu sio mwanzo mzuri kwake kisiasa. Unachukua fomu ya kugombea uongozi halafu unaanza kuwashambulia watu kuwa hawafai ooh mafisadi ni ukosefu wa sera, manifesto na ushauri. Huyu jamaa anataka kujijengea umaarufu kupitia migongo ya hao anaowatuhumu awe mbunifu.
 
mkuu,
Kwenye Siasa Hizi Za Maji Taka,kauli Kama Aliyotoa Nape Ina Maana Kubwa Sana,sidhani Kama Kakurupuka Kuwavaa El Na En, Kuna Secure Base Nyuma Yake Inayompa Kusema Aliyosema.
Kumbuka Sisiem Haiwezi Kamilika Bila Kuwa Uvccm Ktk Kueneza Propaganda Zao.
Hata Hao Anaowatuhumu Kuwa Mafisadi Hawawezi Kumvamia Tu Bila Kujua Hii Nguvu Inayompa Kutamka Hivo Inatoka Wapi.

Nami Naamini Hivyo, Huyu Kijana Lazima Anaongea Akiwa Kwenye Ngome Kubwa Ya Kumuhifadhi Na Kumlinda Dhidi Ya Mikikimikiki Mithili Ya Wareno Walivyokuwa Wanajichimbia Pale fort Jesus Ya Pale Mombasa!
 
Enzi za zama za kuogopana inamalizika CCM.

Nape tupo nyuma yako, husitie shaka. Mafisadi watakimbia mwaka huu.
 
Back
Top Bottom