Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga


Kweli wapo wajinga watakaoshangazwa na majina kama Mbowe na Slaa kuhusishwa kushiriki katika mikakati hii ya kigaidi lakini wenye akili zetu hatutashangaa!..Si walisema wenyewe kwamba watahakikisha nchi hii haitatawalika?...kumbe walilenga kuigombanisha Serikali na wananchi kwa kuua watu wasio na hatia ili kujenga chuki baina ya Serikali na watu wake!... laana inawatafuna sasa!
 
Kwaheri CCM ....haya yanayoendelea ni kutapatapa tuu. Kizuri zaidi wananchi wameshawaelewa! Kwaheri CCM!
 
Nataka Mwigulu, Membe na wengine waingizwe kwenye hili sakata. Wasipowaingiza hao na wengine, kesi hii ni upuuzi mwingine na dhulma dhidi ya upinzani.


Acha pupa subiri hii yenye vithibitisho vya wazi ikamilike kwanza ili jamii hasa waandishi, viongozi wa dini na madaktari watambue nani mbaya wao!
 
Kesi yenyewe kama magumashi vile,ya kuchongwa chongwa au ya kuungaunga. Hao wengine basi wakamatwe mapema.

Kina Lwakatare wameshaanza kutaja wahusika wenzao wanaoshiriki katika matukio ya kigaidi wewe unasema kesi ya kuungaunga? wee kweli hopeless!
 
Acha pupa subiri hii yenye vithibitisho vya wazi ikamilike kwanza ili jamii hasa waandishi, viongozi wa dini na madaktari watambue nani mbaya wao!

Mnakera sana na vielelezo vyenu vya kuchonga!

Lazima tupambane na utawala dharimu mbaka mwisho!
 
Mnakera sana na vielelezo vyenu vya kuchonga!

Lazima tupambane na utawala dharimu mbaka mwisho!

Lwakatare mwenyewe amekiri video yake na ameanza kuwataja wauaji wenzake, wewe hutaki kukubali!...ndio kusema unampenda sana Lwakatare kuliko unavyoupenda ukweli au?
 
Nataka Mwigulu, Membe na wengine waingizwe kwenye hili sakata. Wasipowaingiza hao na wengine, kesi hii ni upuuzi mwingine na dhulma dhidi ya upinzani.

Ikumbukwe katika moja ya mada yangu wiki iliyopita nilisema Rwekatare anaweza kukumbuka tukio ambalo alikuwepo na movie kuchuliwa. Hiyo movie ndiyo iliyotumika kuhariri uingizwaji wa editing ya sauti.

Mhusika mkuu hapa ni Ludovick ambaye anaonekana ni wa TISS alikuwa kazini. Baada ya tukio tukio la kuwa pamoja siku hiyo na Rwekatare Tundu Lissu anasema Ludovick aliwasiliana na Mwigulu Mchemba kwa simu. Siku mbili baada ya tukio hilo la Rwekatare na Ludovick kuwa pamoja Mwigulu Mchemba alijitokeza TV kutoa tamko kwamba anao ukanda wa movie unaoonyesha Chadema kupanga mikakati ya mauaji. Huyu ndiye mhusika mkuu aliyejivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu mkali.

Baada ya kushikwa Rwekatare Ludovick alikimbilia Iringa kwa kumwambia Mjengwa kwamba ana shughuli ya kufanya Iringa. Ameitwa baada ya Rwekatare kumtaja kwamba siku hiyo walikuwa pamoja.

Unaona mtu huyu Ludovick alijipenyeza hadi kwa Mjengwa blog eti alifanya kwa kujitolea kumbe alikuwa kazini.

Kuna uwezekano anayosema Mwampamba kuwa Ludovick alikuwa anafanya kazi makao makuu Chadema, possible alipenyezwa huko ili awe anachota habari za Chadema toka chunguni.

Hata hapa Jamii forums wapo tena baadhi ni moderators utaona kukiwa na mada ambazo zinahusu sana serikali na CCM baadhi zinaonekana kunyofolewa haraka au kuyumbishiwa jukwaa ambalo halichangiwi na watu wengi.

Siri moja ya kuwajua hawa wa TISS utaona wanalazimisha sana urafiki hata wako tayari kujitolea kwa kila njia na hapo utafikiri ni rafiki mzuri sana kumbe yupo kazini.
 
Kalaghabaho acha kujitekenya na kucheka.ngoma inogile na magamba wameshikwa pabaya.

hapa aliyeshikwa pabaya nani? Magamba au wale wanaojikanganya kukiri au kuikana video inayoonyesha mipango ya mauaji ya watanzania wasio na hatia? usiwe na pupa! Uchunguzi wa Gazeti lenu tukufu la Raia Mwema linasema kuna orodha ya washiriki wa matendo ya kigaidi itakayowasononesha sana!
 

kwani si Dr slaa alisema nusu ya usalama wa Taifa wanaripoti kwake? leo hii wamekuwa maadui?...na bado kuna mengi sana yakakuja yatakayowaacha midomo wazi!
 

Rwekatare kitabasabu baada ya kuwa chini ya ulinzi


​
Ikumbukwe katika moja ya mada yangu wiki iliyopita nilisema Rwekatare anaweza kukumbuka tukio ambalo alikuwepo na movie kuchuliwa. Hiyo movie ndiyo iliyotumika kuhariri uingizwaji wa editing ya sauti.

Mhusika mkuu hapa ni Ludovick ambaye anaonekana ni wa TISS alikuwa kazini. Baada ya tukio la kuwa pamoja siku hiyo na Rwekatare Desemba tarehe 28, Tundu Lissu anasema Ludovick aliwasiliana na Mwigulu Mchemba kwa simu. Siku mbili baada ya tukio hilo la Rwekatare na Ludovick kuwa pamoja Mwigulu Mchemba alijitokeza TV kutoa tamko kwamba anao ukanda wa movie unaoonyesha Chadema kupanga mikakati ya mauaji. Huyu ndiye mhusika mkuu aliyejivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu mkali.

Movie hiyo haijawekwa hadharani licha ya kuambiwa aionyeshe tangu Desember 28 mwakajana Mwigulu alipotoa tamko hilo, maana yake muda wote huu alikuwa anaifanyia editing. Nikawaida ya tabia ya hawa watu kuwa marafiki wakaribu sana ili kujifunza mengi ikiwa tabia, sauti, miondoko na mengineyo wanayokusidia kufanya kwa mtu yule wakiwa na mtu mmoja wa karibu sana ili kutengeneza image wanayokusudia. Pengine hulazimisha urafiki hata uonyeshe hali ya kutomtaka anakuwa mvumilivu na kufanya kila awezacho hata kujitolea ili mradi awe karibu nawe.


Baada ya kushikwa Rwekatare Ludovick alikimbilia Iringa kwa kumwambia Mjengwa kwamba ana shughuli ya kufanya Iringa. Ameitwa baada ya Rwekatare kumtaja kwamba siku hiyo walikuwa pamoja.

Unaona mtu huyu Ludovick alijipenyeza hadi kwa Mjengwa blog eti alifanya kwa kujitolea kumbe alikuwa kazini.

Kuna uwezekano anayosema Mwampamba kuwa Ludovick alikuwa anafanya kazi makao makuu Chadema, possible alipenyezwa huko ili awe anachota habari za Chadema toka chunguni.

Hata hapa Jamii forums wapo tena baadhi ni moderators utaona kukiwa na mada ambazo zinahusu sana serikali na CCM baadhi zinaonekana kunyofolewa haraka au kuyumbishiwa jukwaa ambalo halichangiwi na watu wengi.

Siri moja ya kuwajua hawa utaona wanalazimisha sana urafiki hata wako tayari kujitolea kwa kila njia na hapo utafikiri ni rafiki mzuri sana kumbe yupo kazini.
 
Mkuu Juve, kwanza asante kwa maoni yako, hili la mamlaka ya DPP, mimi nimeisha lizungumza sana humu jf, mfano hapa katika uzi huu wa Andrew Nyerere, Topic: Omega Ngole,Never Say Never - Jamii Forums


Mwaka 2009 katika uzi wa Mkuu BAK, DPP wetu kizuizi katika mapambano dhidi ya ufisadi - pia nilizungumzia mamlaka ya DPP,
Hivyo kwenye hili la Chadema kuhoji mamlaka ya DPP sina cha kuongeza zaidi ya haya ambayo nilikwisha kuyasema nyuma.
Pasco

 
kwani si Dr slaa alisema nusu ya usalama wa Taifa wanaripoti kwake? leo hii wamekuwa maadui?...na bado kuna mengi sana yakakuja yatakayowaacha midomo wazi!

Kwa taarifa yako hawa TISS ni kama walivyo CIA hawako kwa masilahi ya taifa au serikali au chama fulani. Wapo kwa shughuli zao binafsi na huko serikalini wameshinikiza na kujishikiza ili kulazimisha serikali ziwape mafao wanayotaka. Ndio maana Taifa la Marekani iliamua kuanzisha taasisi nyingine ya uchunguzi ya FBI. Kama CIA wangefanya kazi kwa weledi kulikuwa na haja gani ya kuwa na Taasisi nyingine ya uchunguzi?

Tanzania licha ya kuwa na TISS mambo ya rushwa hayakwisha na kuendelea kushamiri ndipo serikali ilipolazimika kuanzisha idara nyingine ya uchungu ya TAKUKURU, kama TISS wangekuwa wanafanya kazi yao kwa weledi na kutoa ushirikiano kwa serikali sioni kama kungekuwa na sababu ya kuwa na TAKUKURI.

Hawa TISS wanatumiko kote kote mradi kuna masilahi, wamegawanyika na kila kukiwa na donge zuri wanakugeuka kisiri huku wakionekana kufanya kazi nawe. Inabidi kuwa na uangalifu katika sharing ya habari.

Ludovick mhusika mkuu kuchukua movie ya Rwekatare
 
Taarifa zilizovuja siku moja kabla ya Lwakatare kufikishwa mahakamani zinadai ya kwamba, yapo baadhi ya mambo ambayo Lwakatare aliyakana na kutoyatambua ambayo yamejionyesha katika picha ya video iliyopachikwa kwenye mtandao wa jamii forum, wiki iliyopita lakini pia, kwa upande mwingine, inadaiwa kuna ambayo yaliyomo kwenye video

hiyo kuwa alikiri kuyatambua
. Gazeti hili linashindwa kufichua yapi aliyakana Lwakatare na yapi aliyatambua kutokana na suala hilo kufikishwa mahakamani tayari.

Hapo ndio najiuliza na kutaka kupata ukweli kumbe hata madai kuwa ni video fake yanaweza yasiwe na mashiko tena !!
 
SAKATA la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, kufunguliwa kesi ya ugadi akidaiwa kupanga mikakati ya kudhuru watu, limechukua sura mpya baada ya chama hicho kudai kunasa mawasiliano ya watu kinaowatuhumu kuandaa video hiyo.
Pia CHADEMA imesema kuwa mawakili wake wamepeleka hati ya dharura katika Mahakama Kuu wakiiomba iingilie kati kwa kuitisha mafaili yote mawili ya kesi hiyo inayomkabili Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph.
Lwakatare alikamatwa Machi 13 mwaka huu na kuhojiwa kwa siku nne kisha kufikishwa mahakamani Machi 18 na kufunguliwa kesi namba 37/2013 yenye mashtaka manne huku Ludovick akisomewa mashtaka matatu.
Akizungunza na waandishi wa habari jana makao makuu ya CHADEMA, mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, alidai kuwa wamenasa mawasiliano ya watu mbalimbali wanaowahisi kuhusika kurekodi video hiyo.
Lissu aliwataja watu hao kuwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky, Ludovick na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mwigullu Nchemba.
Alifafanua kuwa Desemba 27 siku moja kabla ya video hiyo haijarekodiwa kulikuwa na mawasilano ya simu kutoka kwa Msacky kwenda kwa Lwakatare akimuulizia sehemu alipo.
Alisema katika mawasiliano hayo, Msacky anayetajwa kudhuriwa na mkakati huo alimpigia simu Lwakatare na kumuulizia mahali alipo ambapo alijibiwa kuwa alikuwa yuko njiani kurejea Dar es Salaam.
Lissu ambaye pia ni mmoja wa jopo la mawakili wanaomtete Lwakatare, aliongeza kuwa Desemba 28, Ludovick alifika nyumbani kwa Lwakatare siku ambayo video hiyo ilirekodiwa saa 11:59.
Aliongeza kuwa kulikuwa na mawasiliano baina ya Ludovick na Nchemba kwa kutumia namba za simu ya Nchemba inayoonekana katika kitabu cha Bunge.
Lissu alidai kuwa baada ya mawasiliano hayo kati ya Desemba 29 mwaka jana na Januari 2 mwaka huu, Nchemba alinukuriwa katika kituo cha televisheni akisema anayo video inayowaonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga njama za mauaji.
"Tumegundua mengi katika haya na kama tutafika mahakamani jaji au hakimu atakayekuwa anasikiliza tukiwa na hoja zetu atamaliza kesi hii ndani ya saa zisizozidi tatu," aliongeza Lissu.
Alipotafutwa Msacky kwa simu yake ya kiganjani ili afafanue madai hayo, alikataa akidai kuwa kesi iko mahakamani.
Kuhusu kupeleka hati ya dharura kuiomba mahakama iitishe mafaili yote mawili na kutengua uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka wa kumfutia Lwakatare mashtaka uliotolewa juzi, Lissu alisema wanatambua mamlaka ya kiongozi huyo katika kufungua na kuiondoa kesi mahakamani.
Alisema lengo ni kulinda maslahi ya taifa au kuboresha utendaji wa haki, suala alilodai halikufanyika katika dhamira nzima ya kufuta kesi ya kwanza ya Lwakatare.
"Tumekaa jopo la mawakili watano; tumeiomba mahakama kuu iingilie kati na kuitisha mafaili yote mawili ya kesi hii na kisha ijiridhishe kama sababu ya kufutwa kwa kesi ya kwanza ni kwa ajili ya maslahi ya taifa," alisema.
Alisema maombi mengine katika hati hiyo ni pamoja na kuiomba mahakama ichunguze ili kuona kama haki imetendeka kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, pia wameiomba ifute hati ya kufutiwa mashtaka kwa Lwakatare na ifute amri ya kumaliza kesi hiyo.
Pia alieleza kuwa wameiomba mahakama kuu iiamuru mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuendelea na kesi ya awali iliyofunguliwa Machi 18 mwaka huu na pia itamke kuwa kilichofanywa na mawakili wa serikali ni kuingilia uhuru wa mahakama wa kufanya uamuzi.
Aliongeza katika kesi ya awali walihoji uwepo wa hati ya ridhaa ya DPP juu ya mteja wao kushtakiwa kwa sheria ya kupambana na ugaidi na wakaonyeshwa makaratasi yasiyokuwa na nembo yoyote ya taifa, hali iliyowafanya wahoji na kumuomba hakimu aifute kesi hiyo ombi lililokuwa linatarajiwa kutolewa uamuzi juzi.
Lissu alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ugaidi ili kosa liwe la kigaidi lazima maelezo ya kosa hilo yaonyeshe kuwepo kwa malengo ya ugaidi hali aliyosema katika mashtaka yote mawili suala hilo halionekani


Baada ya matukio hayo, sasa naomba kuhitimisha kwamba,
1) Kwamba Chadema inapambana na Dola siyo ccm tena.
2) Kwamba kuna hujuma dhidi ya Chadema ni kitu kilicho wazi, siyo ishu ya mjadala tena.
3) Kwamba serikali inabagua wataznania kwa sababu juhudi zinazotumika kumlinda Msacky na kuwapata wauaji wa Barlow ingetumika pia kuwasaka kwa wahusika wa mateso na mauaji ya akina Mwangosi,Padre, Dr Ulimboka na Kibada. Na, Mwigulu Nchemba aliyedai kwamba ana video inayoonesha viongozi wa Chadema wakipanga mauaji siku chache baada ya video hiyo kurekodiwa ambayo kimazingira anaizungumizia video hii hii ya Lwakatare mbona hajahojiwa? R. Igondhu wa TISS Mbona hajahojiwa kuhusu Ulimboka pamoja na kutajwa na Ulimboka mwenyewe?. Kwa nini ya Lwakatare iwe ndo hoja nzito sana serikalini??. A million dolar questions!!


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Soma habari yenyewe kwa ufipi hapa.

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]

[/TD]
 
Nataka Mwigulu, Membe na wengine waingizwe kwenye hili sakata. Wasipowaingiza hao na wengine, kesi hii ni upuuzi mwingine na dhulma dhidi ya upinzani.

Like kubwaaaaaaa sanaaaaa, pamoja na OSCAR NYERERE aliyeingiza sauti ya Kamanda lwakatale kwenye mkanda.
 
Mwigulu nae,iramba kuna umasikini wa kutupwa yeye yupo dar anatengeneza video!hivi huyu ana hata kibanda huko kwao kiteka sidhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…