Omega Ngole,Never Say Never | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Omega Ngole,Never Say Never

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Andrew Nyerere, Nov 20, 2008.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Inashangaza kuona kwamba Nd. Omega Ngolle anasema kwamba ofisi ya DPP haioni sababu ya kuwataja wahusika katika Kampuni ya Kagoda Agr. Ltd.
  Hili ni jambo ambalo linawakatisha tamaa wananchi kwamba haki itatendeka. Bado wanachi wanaombwa kuwa na subira,ili majalada yatazamwe. Hayo majalada yanasomwa mpaka lini. Wananchi wameonyesha subira kubwa sana. Tokea Waziri Mkuu,Mizengo Kayanza Peter Pinda alipoanza kazi,aliwaambia wawe na subira. Mpaka leo unawaambia wawe na subira. Kwa kufanya hivi,wanataka watu wafikirie kwamba wamiliki wa Kampuni ya Kagoda ni wa maana sana kiasi kwamba hawawezi hata kutajwa. Kama amri imetoka kuwakamata hao watu,DPP lazima awakamate na kuwapeleka Mahakamaini ,aendelee kwa kasi kubwa kufanya kazi yake,mpaka hiyo amri itakapobadilishwa. Asitafakari amri. Kama amri haijabadilika,aendelee na utekelezaji.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yangekuwa ni mafaili ya Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vilivyogoma au kina Mkoba yangeshafika mara moja kwa DPP pia wangeshatajwa publicly siku nyingi sana!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  jAMANI JAMANI HAO WAMILIKI SI WANAJULIKANA TU?RA NA LOWASA.......PIA CHANGANYIKENI EL NAE YUMO
   
 4. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli madaraka mazuri..Omega Ngole alikuwa mpiganaji, mfuasi mwema na muadilifu wa Chachage na Shivji alipokuwa Ud hasa kunapotokea suala la haki. Leo amegeuka porojoziiiiiiiiiiiiii nyingi well well ushauri kwa Omega, tumia hekima kijana, umri na uwezo wako unakuruhusu ku influence hao wahusika wa Kagoda watajwe...wape haki yao Watanzania waliovuta subira bila kheri
   
 5. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Porojo alikuwa nazo tokea tulipokuwa naye Umbwe.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Mkuu Andrew, kumbe huyajui mamlaka ya DPP!, hafanyi kazi kwa shinikizo la yoyote, akisema fulani hana kesi, hana kesi na sio hana kosa!. Kagoda imekwapua bilioni 40 kwa ajili ya kugharimia uchaguzi wa Chama chako CCM!, DPP ameangalia watu wa kuwakamata angeanzia kwa aliyekuwepo, aliyepo, MOF, Director wa TISS na hao players wa RA, akaona sii busara kuwakamata, akaamua wasikamatwe na Kagoda haina kosa. Maamuzi ya DPP ni final na hayahojiwi na mamlaka yoyote!.

  Kwa kukusaidia tuu, pia DPP anayo mamlaka yanaitwa Nolle ambayo ana uwezo wa kuingilia kesi yoyote ya jinai ikiwa katika hatua yoyote kabla ya hukumu na kuiondoa mahakamani pasi kutoa sababu wala kuhojiwa na yoyote!.

  Kwa maoni yangu, uamuzi wa DPP kutoishitaki Kagoda, ni uamuzi wa busara sana unaozingatia maslahi ya taifa kama alivyofanya kwa kutoichunguza Meremeta na Deep Green etc, kwa maslahi ya Taifa!.

  Wewe hili ulilijua?. Na baada ya kukutajia wahusika wakuu wa Kagoda, bado ungependwa wachunguzwe?.

  Pasco.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, hoja hii ya Andrew Nyerere kuhoji mamlaka ya DPP, iliibuliwa mwaka 2008, na haya yalikuwa majibu yangu mwaka huo, juzi DPP ameyatumia mamlaka haya kuiondoa kesi ya Rwakatare, nimesoma mahali humu jf kuwa wanasheria wa Chadema wanafungua kesi mahakama kuu kuhoji mamlaka hii ya DPP, kwa maoni yangu, this is wastage of time!, kwa vile mamlaka hayo, yako kikatiba, the right forum ni au kufungua kesi ya kikatiba, mahakama kuu itamke mamlaka hayo ni kinyume cha katiba kwa sababu yanakinzana na kifungu fulani cha katiba, hivyo kuiamuru serikali kupeleka bungeni marekebisho ya katiba, au kushinikiza katiba mpya kuyapunguza mamlaka hayo ya DPP.
   
Loading...