Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

Matapeli wawili wakikutana..................................
a) hujitahidi kufilisi nchi
b) siri zao hujulikana wazi
c) hutamjua anayesema ukweli.
 
Idd Simba hawezi kuwa shujaa wa anything, zaidi ya ufisadi huyu ndiye aliyeuza NBC akishirikiana na Kigoda, na Sumaye, walipojaribu kuuza NMB ndipo wajanja wakampa Mzindakaya info za ufisadi wake wa kuuza sukari ya jeshi kwa mwendo wa kifisadi, akajifanya yeye ni rafiki wa karibu sana wa Mkapa, wabunge wakamgomea kwamba ajiuzulu, Sumaye kutaka kumuokoa akamwita Mkapa, kwenye kikao dharura cha wabunge wa CCM Dodoma, Mkapa akaingia kwenye kile kikao na matusi mazito sana dhidi ya Mzindakaya kwamba "anajifanya mlipuaji mabomu, kumbe ni mpumbavu tu!", ndipo wabunge karibu wote wakamgomea Mkapa kwamba ni lazima Idd Simba aondoke tena haraka sana,

- Mkapa akawaita Chamwino wabunge ili awanyamazishe, wabunge wakamgomea kwamba ni lazima aondoke, na Mzindakaya akamuahidi Mkapa kwamba atamlipua mpaka na yeye, ndipo Mkapa akampa hela za kutoka BOT lakini kwa compromise na Simba kuondoka uwaziri, siku alipoondoka uwaziri Mkapa akasema amepokea hati ya kujiuzulu kwa Simba kwa moyo mzito sana, baada ya kuondolewa uwaziri Simba akaanza mbio za kutafuta urais, kwa kuwashinikiza Waisilamu kuandamana na kuleta fujo kama kawa wazito wakamgundua kupitia kwa KK, ndipo akaitwa CC na kuonywa kwamba atarudishwa kwao Burundi mara moja asipoacha huu ujinga,[/SIZE]

- Hakukoma bado akaanza mambo ya uzawa again akitafuta urais, ndipo CCM wakamtupa nje kwenye uenyekiti wa Wazazi, na kumpa onyo na karipio kali sana kwamba asichezee moto, onyo ambalo alipewa na Kawawa ndani ya CC, sasa leo ni shujaaa? Is that so au tunajaribu kudanganyana kwa makusudi kukiwa na lengo kubwa sana behind it!

- Idd simba ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalum ya bunge iliyotumwa na bunge kumchunguza Mbilinyi na Mkapa mwenyewe akiwa Rais, kuhusu shutuma za hela za rushwa za minofu ya samaki info ambayo Mrema alipewa na Mzindakaya, akatoa ripoti kwamba Mbilinyi alihusika na rushwa hizo lakini akawa bubu on mkapa, hapo hapo yeye na katibu wake Masilingi wakapewa uwaziri, leo huyu ni shujaaa?

- Hivi huwa hatufuaitlii siasa za taifa letu or what? i mean haya mambo mbona hata hayana miaka mingi toka yatokee? richimonduli si imefanyika majuzi tu, ndio maana tunasema kuna kampeni kubwa sana inyaoendeshwa hapa, au ni simply arrogancy tu ya kujifanya kujua na wengine wote ni wajinga, maana nikisema mimi basi JF watakubali tu, maana this thing does not make a sense at all, vile vibali vya sukari ya jeshi walivyotajirikia navyo Marwa na Kinje, walivitoa wapi kama sio kwa huyu Idd Simba?

Jamani hebu oneni huruma kidogo na hili taifa, Idd Simba sio shujaa ni fisadi tena original, anastahili kuwa Segerea!

Respect
 
Idd Simba hana uchunju na taifa letu kwa kuwa yeye ni Mrundi. Huu ndio ubaya wa kuweka wakuja kwenye nafasi za maamuzi. Lazima wajipendelee wao na matumbo yao.
 
Mil 285, Je
1. Anayo registered company na papers zote zinazomtambua kama mshauri wa maswala ya uwekezaji
2. Amelipa kodi kiasi gani out of that money
3. Je alitoa invoice na receipt

Haya ndiyo maswali ya mwanzo kabisa
 
hii kesi itahamuliwa na TISS chini ya usimamizi mkali sana wa MAGOGONI , wote si watoto wa mjini bwana
 
Uuzwaji wa UDA kwa Simon Group ni kwa faida ya walalahoi wa Dar es Salaam, watanzania ni watu wa ajabu sana, angekuwa ameuziwa mgeni msingekuwa na tatizo lolote lakini leo kauziwa mtanzania mwenzenu basi maneno kibao,lipi jema kwenu, acheni wivu,*

Mkuu sana ETM

UDA wameuza share 51% kwa Simon Group kwa gharama ya 1.2 bil makubaliano ilikuwa ni kwa Simon Group kulipa fedha hiyo kwa mikupuo kadhaa, aliyewaingiza mkenge watanzania ni mwenyekiti wala siyo Simon Group. Mkuu UDA ina mali za zaidi ya 13.5 billion, viongozi wenu wameuza 51% shares at 1.2 bil, kweli.????.. Halafu watu badala ya kuhoji maswala ya msingi kama haya, mnaendekeza roho ya wivu, hapana siyo vizuri.

Mkuu point yako ni ipi hasa? kama posts zako mbili zinajikontradikti vile. Hebu fafanua zaidi Mkuu. What exactly do you want say? BTW kulikuwa na umuhimu wa kuuza UDA in the first place, ukitilia maanani ingeshirikishwa moja kwa moja kwenye DART? Mkuu hapa kuna issue mbili. Issue ya kwanza, UDA kuuzwa tena kinyume na sheria. Pili, UDA kuuzwa kwa bei chee. Fafanua Mkuu.
 
Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu
ndug usifikirie pafupi biblia inasema tumuongope mtu auaye mwili na roho wewe hapo najua roho yako na mwili vilishakufa hasa unapokuwa maskini unategemea nini? tusidanganyane huu ni ukweli wewe uko kaburini. huwezi sema uko hai huku unashindwa hata kupata mlo kwa siku
 
Aisee... inatubidi watz tuungame dhambi zetu zote... kwani kwa staili hii ya chukua chako mapema ni hatari kwa nchi. Na wahusika wako huru kabisa na wanadiriki hata kuwaita waandishi wa habari na kuanza kutoa maelezo... mlala hoi ukihisiwa tu kwa chochote hata iwe wizi wa wembe POLISI unawaona wako kazini ghafla ila mwenye pesa wanatafuta ushahidi kidizaini ili kupotezea ishu. Tuache ujinga kama ndivyo ilivyo basi tuuze kila tulichochuma tangu mkoloni, enzi za mwalimu na tugawane sote kwa ujumla wetu ili kama vipi tuanze moja bana na sio hii ya sasa kwa wachache kujipakulia keki utadhani wao pekee ndio wenye uhalali wa kula keki hiyo... ifike mahali na sisi wanyonge tuamke na tudai haki zetu tena kwa staili ile ya mpk kieleweke... Jamani viongozi mliopewa dhamani ya kuwaongoza maskini sisi tujalini kwa kuzilinda mali za nchi yetu na kwa kuwa wazalendo zaidi na si kuangalia matumbo yenu na familia zenu.
Aibu kwa mtu kama Idd kufanya mambo ya kijinga namna hiyo wkt yeye ni msomi na yuko tayari well off, pesa za PRIDE pekee hazikutoshi mkuu... ona sasa unashusha hadhi yako ktk jamii kwani PRIDE imekopesha wa2 wengi sana na wengi we2 ni wale wa kima cha chini sasa tukiwa kama wateja wako tutaanza kupungukiwa na imani.
Jamani nchi ni yetu sote na kama tukiamua kuila au kuiuza basi tuile sote na kama kuuza basi iuzwe na tugawane sote kila mmoja atajua pa kwenda bana ahaaa... inatia uchungu sometime.
Mungu ibariki Tanzania.....sana sana wabariki viongozi wake ili wajue namna ya kuwatumia watz na mali zao.
 
Waandishi wa habari wa bongo wamelala, ingekuwa nje wange mkera na kutamka yote within few hours.
Sasa hapa watu wanafanya uozo jamaa wanahamahama habari tuu hawafuatilii mpaka mwisho,
Vipi katibu Nishati na mamilioni aliyokusanya wote mmehongwa na mmenyamaza kimya hamna anayefuatilia usiku na mchana
mweeee nyie
 
Idd Simba (CCM) na Bob Makani (Chadema) Uhusiano wao Watoto wao Wameoana

Is this Conflict of Interest?

Natafuta mahali ambapo Bob Makani ametajwa kwenye UDA sipati; una maana Bob Makani na yeye yuko kwenye deal au ni board member wa UDA, PRIDE or what? Najaribu kuangalia conflict of interest uliyoitaja.
 
Siasa na biashara ni vitu viwili tofauti, hawa jamaa wa magamba wanatumia uzoefu wao wa siasa na ufisadi kwenye biashara. kwanza kabisa UDA ilitakiwa kuuzwa kwa mwekezaji on billions, then unakuja shtukia eti imeuzwa kwa milioni 285! hii kweli nchi ya mazonge
 
Waandishi wa habari wa bongo wamelala, ingekuwa nje wange mkera na kutamka yote within few hours.
Sasa hapa watu wanafanya uozo jamaa wanahamahama habari tuu hawafuatilii mpaka mwisho,
Vipi katibu Nishati na mamilioni aliyokusanya wote mmehongwa na mmenyamaza kimya hamna anayefuatilia usiku na mchana
mweeee nyie
 
Mkuu point yako ni ipi hasa? kama posts zako mbili zinajikontradikti vile. Hebu fafanua zaidi Mkuu. What exactly do you want say? BTW kulikuwa na umuhimu wa kuuza UDA in the first place, ukitilia maanani ingeshirikishwa moja kwa moja kwenye DART? Mkuu hapa kuna issue mbili. Issue ya kwanza, UDA kuuzwa tena kinyume na sheria. Pili, UDA kuuzwa kwa bei chee. Fafanua Mkuu.
Mkuu, point yake ya tatu nadhani inamweka kwenye upande wa mwangaza!!

Mil 285, Je
1. Anayo registered company na papers zote zinazomtambua kama mshauri wa maswala ya uwekezaji
2. Amelipa kodi kiasi gani out of that money
3. Je alitoa invoice na receipt

Haya ndiyo maswali ya mwanzo kabisa
 
Maelezo ya mwekezaji wetu:

"Mr Kisena said that they have already paid 750m/- to purchase the company and intend to complete payment by end of this month. He said that his company bought 52.53 per cent of UDA shares at 1.2bn/-.

‘’We have already set up plans to improve public transport in Dar es Salaam by ordering
26 buses at the tune of 110,000 sterling pounds each with the capacity to carry 150 people,” he said."


Daily News | Bunge committee faults sale of UDA

Wakati tunaambiwa mabus yanaagizwa toka ulaya, sehemu za kutengenezea magari (service bay) za UDA zimefukiwa na kugeuzwa maghala. Picha zitajieleza
C-7 003.jpg


 

Attachments

  • C-7 002.jpg
    C-7 002.jpg
    447.2 KB · Views: 649
  • C-7 004.jpg
    C-7 004.jpg
    483.7 KB · Views: 658
  • C-7 005.jpg
    C-7 005.jpg
    383.3 KB · Views: 646
Idd Simba ni mtu hatari sana kwa kuwa ameshiriki sana kwenye vitendo vya kuiba mali za umma na kuona kama vile anashiriki katika utapeli wa Taifa letu Tanzania na kumbuka historia yake
 
Kikwete uko wapi ???
Mbona kwenye kampeni ulikuwa mkali sANA
MBONA UNATUSALITI?
WEKA NDANI HAWA WATU
 
Wakuu zangu,
Pamoja na kutompenda Idd Simba lakini tujaribu kutumia akili japo kidogo ktk kutazama sakata hili..
1. Hivi kweli inawaingia akilini nyie kwamba shirika au mtu anaweza kutaka kununua hisa za UDA (shirika la Umma) akalipa sehemu ya ununuzi huo ktk account ya mtu?.
2. Nataka kuuliza hivi kweli UDA ipo ktk soko la DSE na kama haipo hawa simon walipata wapi wazo la kwamba UDA iinauza hisa zake na kwa kupitia gazeti gani la serikali.. Na hata kama ikiwa kweli ununuzi wa hisa unafanyika vipi kwa mnunuzi wa hisa ktk shirika ambalo lipo DSE. Unanunua shares kwa kupitia account ya Idd Simba kweli?.. hii kweli inaingia akilini mwenu jamani..

Hapa kuna jambo limefanyika na kwa sababu jipu limepasuka na wananchi tumelijua hili mbele ya kile kilichotaka kutokea. Kuna mchezo mchafu sana unafanyika hapa na harufu ya rushwa inaendelea kujionyesha kwani binafsi naamini kabisa kwamba Simon group walitoa fedha hizo kama hongo RUSHWA ( Hearsay and circumstantial) ili tender yao ya ununuzi wa UDA ipite, sasa ilipokuja gundulika njama nzima za Uuzaji wa UDA kila mtu anaruka na Simon group wanashindwa kuzi account milioni 285 (just under Usd 200,000) ambazo walitoa kama rushwa ktk ununuzi wa UDA..Haiwezekani 285m/- kuwa sehemu ya malipo ya ununuzi wa mali zote za UDA ikiwa leo kiwanja cha nyumba ya vyumba sita Kinondoni au Migomigo kinauzwa kwa bei hiyo hiyo..
 
Waandishi wa habari wa bongo wamelala, ingekuwa nje wange mkera na kutamka yote within few hours.
Sasa hapa watu wanafanya uozo jamaa wanahamahama habari tuu hawafuatilii mpaka mwisho,
Vipi katibu Nishati na mamilioni aliyokusanya wote mmehongwa na mmenyamaza kimya hamna anayefuatilia usiku na mchana
mweeee nyie

Mkuu wamezoea kupewa bahasha. Kwenye ufisadi unaondelea hapa nchini, vyombo vya habari navyo vinachangia. Kama issue ya Shimbo ingekuwa kwenye nchi nyingine hata Kenya, mbona tungekuwa tumeshapata verification toka kwa wahusika kama ni rumours au ukweli? Watu wanailamu JF kwa kuleta habari bila ushahidi lakini vipi vyombo vingine vya habari vinakaa kimya hata kama suala liko wazi?

Kama alivyosema Mzee Warioba hivi karibuni vyombo vya habari vina budi kuachana na tabia ya kuandika habari za siasa hasa zinazohusu viongozi na malumbano yao. Inabdi hivi vyombo viandike habari zinazohusu mustakabadhi wa taifa hili na ustawi wa wananchi wake.
 
Back
Top Bottom