Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

Yeah, maelezo yake ni yale ya funika kombe mwanaharamu aselebuke!!!
Anakubali kuwa malipo ya 51% shares ni 1.2 billion, hapo hapo anasema mali ya UDA ni kwenye tune ya 13 billion...
Kama assets zilifika 13billion kwa share 49% tungetarajia shirika lipate mwekezaji kwa thamani zaidi ya mali zilipo toa madeni, labda tuambiwe madeni ya UDA ni zaidi ya 13billion. Ninachoweza kusema tu ni kwamba serikali, Iddi Simba, Simon Kisena, ccm na mafisadi wote eleweni kwamba watanzania sio mbumbumbu tena kama mlivyo zoea iko siku watachoka kusikia na mtajikuta mnachomewa ndani ya nyumba zenu
 
UDA; Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam, limekwishakufa lakini bado tu, mazishi. UDA limekufa kishujaa kama mwanamuzi Dk. Remmy Ongalla anavyosema akimsifu samaki kuwa ni shujaa maana anavuliwa, anakatwakatwa, anapikwa au kukaangwa na hata kuliwa, lakini kwa ushujaa wake, samaki anaendelea kuangalia tu, maana siku zote kilio cha samaki machozi huenda na maji.
Machozi ya UDA nayo yanatiririka hata kwenda na maji; maji yaliyojaa harufu ya uchafu wa ufisadi. Huu ni ufisadi ambao umeanikwa hadharani hivi karibuni kiasi cha kumfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kumwagiza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kulichunguza shirika hilo ili kujua limetafunwa na mchwa wa aina gani.
Agizo la Waziri Mkuu limekuja baada ya kuziangalia nyuso za wawakilishi wa wananchi waliokuwa wakichangia mjadala bungeni; walikuwa na hisia kali kwelikweli. Ni hisia hizo zilizomfanya kumbe hata Waziri Mkuu azinduke kuwa hapo, kuna jambo na hivyo, kuagiza uchunguzi makini ili kwamba, atakayebainika kutaka kunenepa kwa gharama za maisha ya wengine, basi achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Swali linabaki, je, nini hatma ya uchunguzi wa sakata hili hasa kutokana na kuwepo tuhuma kwamba kuna watu wakubwa na watoto wa vigogo wanahusika katika ufisadi huu? Je, ni suala la kufunika kombe ili mwanaharamu apite?
Hata hivyo, wakati Watanzania hasa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanayaelekeza macho na masikio yao kujua ni uchafu gani utafichuliwa, tayari wanapigwa konde la malumbano makali baina ya wabunge wa Jijini la Dar es Salaam na viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, akiwamo Meya wa Jiji.
Kinachoshangaza kwa upande mwingine kikafurahisha na kuthibitisha usemi kuwa vita ya panzi ni furaha kwa kunguru au basi hasira za mkizi faida kwa mvuvi ni kwamba, viongozi hao sasa wameanza “kufumua mabomu” mengine ambayo ama walikuwa “wamefumbiana macho” kwa “kulindana”, au basi walikuwa wameyakalia bila wao wenyewe kujua.
Ndiyo maana, wakati Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akisema uchunguzi wa kuhusu ubadhirifu wa mali za jiji utaendelea na kutamba kuwa hakuna mtu wa kumzuia, wachunguzi wa mambo ya kijamii wanasema Dk. Masaburi anatoa “vitisho vya nyau” ili kuwaziba midomo wabunge hao. Kwamba alikuwa wapi kama aliyajua hayo!
Itakumbukwa kwamba wabunge hao wakiongozwa na Abbas Mtemvu waliuelezea umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa, wanasikitishwa na uchafu wa kifisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za kulinda maslahi ya umma uliofanywa na Meya huyo pamoja na Mkurugenzi wa UDA, Bakari Kingobi.
Gazeti moja litolewalo kila siku; toleo la Jumapili Agosti 7,2011, limemnukuu Masaburi akiapa kwa paa na ayala wa porini kuwa sasa lazima afanye uchunguzi wa mikataba yote yeye mwenyewe akishirikiana na wataalamu mbalimbali wenye uwezo wa kubaini wizi ndani ya mikataba na wala sio kwa kuunda kamati kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Kwamba kinachofanywa na wabunge wa Dar es Salaam wakiongozwa na Abbas Mtemvu (Mbunge wa Temeke) na Musa Zungu (Mbunge wa Ilala) ni kumtisha asiendelee kuchunguza maovu yao, kitu alichosema kwamba katu hakitamzuia.
Anaitaja miradi itakayochunguzwa kuwa ni pamoja na Machinga Complex ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Ilala, Musa Zungu; Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) linaloongozwa na Mtemvu (Mbunge wa Temeke) akidai huko kuna ufisadi mkubwa unaowahusisha watunga sheria hao na makada wenziye wa CCM.
Anakwenda mbali na kusema anafahamu baadhi ya wabunge wanahusika na ufisadi huo wa mali za Jiji la Dar es Salaam na kwamba ndio maana wanatafuta visingizio vya kumng’oa kwa kushinikiza ajiuzulu wakati mikataba yote ya UDA ilifanyika akiwa hayupo, na badala yake wabunge hao ndio waliohusika.
Kwa upande wao, wabunge wanasema kwa vyovyote iwavyo hawakubali hili lipite maana mchakato wa kuliuza shirika hilo (UDA) kwa Kampuni ya Simion Group Limited umejaa utata; umejaa rushwa na wanakwenda mbali zaidi na kusema kuwa, zipo taarifa kuwa hata Masaburi mwenyewe tayari “amekatiwa chake”.

 
Wote ni wale wale. Nchi imeoza na inanuka. Tunahitaji watu kama Adolf Hitler! Masaburi, Kisena, Idi Simba wote hawana historia nzuri. kISENA AMEANZIA KANDA YA ZIWA SASA AMEFIKA PWANI-AMEFIKA.Hapa hatoki. Yeye na Kapuya walizoea kudhulimu wakulima wa pamba leo ameingia BONGO-Amekwisha. Ubunge alishindwa kwa mbinu zake chafu
 
Nilifuatilia mjadala kuhusu uuzwaji wa UDA. Katika mjadala huo uliorushwa na Star TV, kisena alidai wamefungua kesi ili pesa walizolipa kwa Iddi Simba zirejeshwe kwenye akaunti halali ya mauziano ambayo ni akaunti ya UDA. Wanajamii, hamuoni huu ni ujanja kwa kuwa tayari UDA ni ya Kisena, malipo hayo yakirudishwa UDA ni sawa na Kisena kurudishiwa pesa aliyoghilibu kununulia UDA? Yaani mlipaji anadai arejeshewe malipo yake na mali alikwisha chukua?
Nasimama kueleweshwa na kukosolewa.
 
Alitoa rushwa ili aipate UDA kiulaini, sasa arudishiwe hongo wakati UDA kaishaipata? Anafurahisha kweli!
 
Niliuangalia mjadala huo. Kwa kweli Kisena alijiandaa alipangua hoja nyingi kirahisi.Kama ni tapeli basi atakuwa anacalculate muda mrefu kabla hajatekeleza mambo yake.Ila nilimpenda.Kwa umri alionao na jinsi anavyoongea mambo ya multi millions na jinsi anavyoyaendesha successfully kama anavyodai mwenyewe... Kwa kweli ni dume la mbegu.
 
Wakuu lile suala la UDA kubinafsishwa kinyemela limeishia wapi...naona watu walipiga kelele then kukawa kimya
 
Ndugu zangu
nauliza hivi iile kesi ya uda imeshia wapi jamani
nakumbuka iddi simba aliingiza million 200 kwenye account na
watanzania tumekaa kimya hivi tumejiuliza wapo iddisimba
wangapi jamani wanaingiza hela zao kwenye account zao
mi sisemi
 
Kesi iko Mahakama ya Hakmu mkazi ambayo Richard Kisena anamshtaki Iddi Simba na Meneja wa Uda. Then kuna CAG amewaaagiza outsourced auditors wafuatilie mahesabu na kanuni za uuzwaji. So tega sikio
 
Sasahivi UKAWA Wanalo jiji...kama uuzwaji haukuwa katika Armlength...inataifishwa tu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom