Binti wa Masaburi kuburuzwa mahakamani sakata la kunyang’anya ndugu mirathi

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Ndugu wa marehemu aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam, Dkt. Didas Masaburi wamepanga kumburuza mahakamani binti wa marehemu Juliana Masaburi kwa kile kilichodaiwa kupanga njama ya kuwadhulumu mali za urithi walizokabidhiwa kimila kama wasimamizi wa mirathi ya marehemu.

Ndugu wanadai kuwa mali hizo ziligawanywa kwa ndugu kimila kwa kufuatia usia aliouacha marehemu kabla ya kufariki, kuwa mali zigawanywe kwa sheria za kimila kutokana na mfumo wa maisha ya Marehemu aliyoishi.

Marehemu aliomba kuwa akifa azikwe Chanika na mirathi yake iendesheshwe kama taratibu za maisha yake aliyoishi jambo ambalo lilitimizwa na wasimamizi wa mirathi yake.

Wanaopanga kumburuza mahakamani mbunge huyo wa viti maalum CCM ni watoto wa nje wa marehemu, kaka na wadogo zake masaburi wakiongozwa na mdogo wa mwisho wa masaburi aitwaye Otieno masaburi.

Wengine waliopangana kuungana na familia hiyo ni wadeni waliokuwa wanamdai marehemu kwani baada ya mazishi kukamilika kulitokea ugomvi na mvutano wa kulipa madeni hayo ambayo hadi sasa hayajalipwa.

Ndugu wanadai kuwa binti huyo wa marehemu alitumia nguvu ya ushawishi wa kiongozi mkubwa serikalini ambaye alikuwa na mahusiano naye kimapenzi kuwanyang’anya mirathi ya halali jambo ambalo ndugu wanasema ulikuwa na mkono wake kwa kumuwekea kifua Juliana.

Baadhi ya ndugu wamelalamika kunyang’anywa mali kinguvu kwa kusarenda na wengine kufunguliwa kesi za unyang’anyi ila hali si wanyang’anyi. Dk. Didas Masaburi (56), alifariki katika hospital ya Muhimbili Dar es Salaam kwa ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatitis B) Mwaka 2016.

Dk. Masaburi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1995. Amewahi kufanya kazi Wizara ya Elimu, Utamaduni na Michezo kupitia mradi maalumu wa Benki ya Dunia (WB).

Marehemu aliacha Shule ya Sekondari ya Dk. Didas Masaburi iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam pamoja na anamiliki Chuo cha Ugavi na Manunuzi kilichopo Chanika.

Umaarufu wa masaburi uliibuka Agosti 6, 2011, Dk. Masaburi baada ya Kuingia malumbano na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walimtaka ajiuzulu kutokana na kukiuka taratibu katika uuzwaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).
 
Ehehehehehe huyu si alikuwa nyumba ndogo ya aliyelala huko chato. Kimemramba
Marehemu alivyokuwa hana aibu akamlala binti wa rafiki yake.
 
Matajir wa kiafrika wa kitanzania wakifa mirathi ni patashika nguo kuchanika sijui.kwa nini
Hapa tunapata somo Kwa Sisi ambao tupo hai kuwa kwenye maisha yetu tuepuke kuzaa hovyo na wanawake tofauti pia ndoa za mitala ni majanga Tu na haya ndiyo matokeo yake...
 
Hapa tunapata somo Kwa Sisi ambao tupo hai kuwa kwenye maisha yetu tuepuke kuzaa hovyo na wanawake tofauti pia ndoa za mitala ni majanga Tu na haya ndiyo matokeo yake...
Hata wasiozaa nje shida hiyo hiyo wakifa
Ndugu wa wa mwanaume hujitosa hasa mume akifariki kutaka mirathi

Ndugu huanzisha vurugu hasa kwenye mirathi kuzitaka
 
Hapa tunapata somo Kwa Sisi ambao tupo hai kuwa kwenye maisha yetu tuepuke kuzaa hovyo na wanawake tofauti pia ndoa za mitala ni majanga Tu na haya ndiyo matokeo yake...
Mbona inaonekana wenye shida ni ndugu!? Makaka na wadogo zake!? By the way zilikuwa Mali za wizi Wacha zirudishwe Kwa wahitaji wengine
 
Back
Top Bottom