Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

ya ununuzi huo ktk account ya mtu?.
2. Nataka kuuliza hivi kweli UDA ipo ktk soko la DSE na kama haipo hawa simon walipata wapi wazo la kwamba UDA iinauza hisa zake na kwa kupitia gazeti gani la serikali.. Na hata kama ikiwa kweli ununuzi wa hisa unafanyika vipi kwa mnunuzi wa hisa ktk shirika ambalo lipo DSE. Unanunua shares kwa kupitia account ya Idd Simba kweli?.. hii kweli inaingia akilini mwenu jamani..

Hapa kuna jambo limefanyika na kwa sababu jipu limepasuka na wananchi tumelijua hili mbele ya kile kilichotaka kutokea. Kuna mchezo mchafu sana unafanyika hapa na harufu ya rushwa inaendelea kujionyesha kwani binafsi naamini kabisa kwamba Simon group walitoa fedha hizo kama hongo RUSHWA ( Hearsay and circumstantial) ili tender yao ya ununuzi wa UDA ipite, sasa ilipokuja gundulika njama nzima za Uuzaji wa UDA kila mtu anaruka na Simon group wanashindwa kuzi account milioni 285 (just under Usd 200,000) ambazo walitoa kama rushwa ktk ununuzi wa UDA..Haiwezekani 285m/- kuwa sehemu ya malipo ya ununuzi wa mali zote za UDA ikiwa leo kiwanja cha nyumba ya vyumba sita Kinondoni au Migomigo kinauzwa kwa bei hiyo hiyo..

Mkuu paragraph yako ya kwanza inajicontradikti na ya pli. Suggestion kwamba walitoa rushwa ili tenda yao ipite ni sawa na kukubali kuwa serikali ilitangaza tenda na watu zaidi ya mmoja walituma mambi, so Simon Group wakatoa rushwa ili yao ipite. I don't think that is the case. Hili suala lipo so straight forward hakuna hata haja ya kuja na conspiracy theories.
 
Straight foward kwa vipi?..Unajua mkuu wangu Bongo watu wanafahamu kinachokuja mbele miezi kabla ya tender kutoka. Siku tender zinawekwa mezani tayari watu wameisha zifunga - wenyewe husema - Mcheza kwao!
 
Haya ndio mambo Takukuru ilitakiwa kushughulikia! Siyo kutoa semina mashuleni!

Semina mashuleni zina per diem, na posho mbali mbali na bila kusahau trip za uzinzi, ulevi na starehe! ndio muhimu sana kwao! issue za maana haswa ambazo walitakiwa kufuatilia wamelala, au kufuatilia dili ili wapewe kitu kidogo!!
Ama kwa hakika kazi ni kwetu!!
 
Hii kwangu naona ilikuwa deal kati ya Robert Kisena & co na Idd Simba & Co lakini wakashindwa kuelewana na sasa mambo yote hadharani. Pande zote mbili maelezo yao haya make sense; wanajichanganya, wanatoa maelezo tofauti tofauti etc. Kama walivyosema wengine hawa wote ni wezi tu. Hata kama shirika lingekuwa linauzwa kiuhalali transaction yenyewe imefanyika kihuni sana. Hivi kulikuwa hamna mwanasheria aliyekuwa anasimamia? au kwamaana nyingine UDA ina mwanasheria wake?

Mkuu who knows kama wanasheria nao walipewa asilimia 10? Kwa vile interest (shares) iliyonunuliwa ilikuwa ni ya serikali, si tungetegemea Ofisi wa Mwanasheria Mkuu ihusishwe? Au hii ofisi haihusishwi kwenye kubinafsisha mashirika ya umma?
 
Kwa vipi?..

Paragraph ya kwanza ana suggest kuwa serikali haukutangaza kuuza shares zake. Paragraph ya pili ana suggest pengine Simon ilitoa rushwa ili tenda yao ipite. Kama serikali ilitangaza tenda akina nani walituma tenda ili Simon Group watoe rushwa tenda yao ipite?
 
Hv kwl govt imekosa ushaidi au ndo kulindana!Minahic sa hv wanajipanga kumchomoa swahib Iddy coz ni m2 wao mkubwa 2....na hi tabia yao ya kupeana vitengo wkt wa2 wanasota kitaa!
 
Paragraph ya kwanza ana suggest kuwa serikali haukutangaza kuuza shares zake. Paragraph ya pili ana suggest pengine Simon ilitoa rushwa ili tenda yao ipite. Kama serikali ilitangaza tenda akina nani walituma tenda ili Simon Group watoe rushwa tenda yao ipite?
Dah, mkuu maelezo hayo ni yangu yeye alinukuu vibaya tu. Kama ulinisoma vizuri niliweka kimaswali zaidi ya kuwa na uhakika ndio maana nikauliza kama UDA ni shirika binafsi ambalo linauza hisa (kulingana na madai ya Simon group), kisha nikasema kama kweli imetokea hivyo iweje mtu uweke fedha zako account ya Idd Simba kununua hisa za UDA wakati yeye sii mmiliki. Na ya pili ni ile ambayo UDA wanauza hisa zao kupitia DSE..Nikauliza kama wapo au hawapo! yote haya ni ktk ushahidi wa hearsay na circumstantial maanake sote hapa hatujui kilichotokea isipokuwa kwa uhakika tunaamini hakuna anayesema ukweli iwe Idd Simba au Simon Group..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Gazeti la majira la leo linaripoti kuwa Idd Simba anadai ile pesa aliyoingiziwa kwenye akaunt yake na mnunuzi (Simon) haihusiani na mauzo ya UDA bali ni consultancy fees (yaani malipo ya ushauri wa kitalaam) alioutoa kwa SImon Group. SImon yeye anadai hajawahi kupata ushauri wa kitaalam kutoka Idd SImba bali pesa hiyo ni malipo ya ununuzi wa UDA. Yaani ni full utata....

Habari yenyewe hii hapa

[h=3]Kashfa UDA - Idd Simba azungumzia kilichotokea[/h]

Iddi Simba ajibu tuhuma dhidi yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd.

Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela.

"Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza;

"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;

"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.

Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.

ha ha haaa!!! duh kweli drama haziishi!! je hapo kwenye nyekundu hizo pesa alizolipwa idd simba kwa kutoa ushauri zimelipiwa kodi!!?? dah kweli macho kuona...
 
Dah, mkuu maelezo hayo ni yangu yeye alinukuu vibaya tu. Kama ulinisoma vizuri niliweka kimaswali zaidi ya kuwa na uhakika ndio maana nikauliza kama UDA ni shirika binafsi ambalo linauza hisa (kulingana na madai ya Simon group), kisha nikasema kama kweli imetokea hivyo iweje mtu uweke fedha zako account ya Idd Simba kununua hisa za UDA wakati yeye sii mmiliki. Na ya pili ni ile ambayo UDA wanauza hisa zao kupitia DSE..Nikauliza kama wapo au hawapo! yote haya ni ktk ushahidi wa hearsay na circumstantial maanake sote hapa hatujui kilichotokea isipokuwa kwa uhakika tunaamini hakuna anayesema ukweli iwe Idd Simba au Simon Group..

Kumbe yalikuwa maneno yako. Probably ali-quote kimaokosa then. Nimerudi kusoma post yako ya awali na kama nimekuelewa suggestion yako ni kwamba Simon Group walitoa rushwa mapema kabisa ili tenda ya kununua UDA ikitangazwa yao ipite kiulaini. Lakini bahati mbaya kwao, deal ika leak kabla ya tenda kutangazwa. Hapo naweza kusema possibly. Au ulikuwa na maana nyingine mkuu?
 
Hawa ndio viongozi wetu,wanasiasa wetu,they just preach what they dont practice,huyu Idd Simba ukimsikia kwenye majukwa ya makongamano anavyopiga kelele kuhusu uzawa na ufisadi utafikiri kweli,kumbe naye ni one of those guys..........namuonea huruma Maranda kaenda jela pekee yake wakati Idd simba anakula kuku huku akiendelea kupiga deal kiulaiiiini.
 
Straight foward kwa vipi?..Unajua mkuu wangu Bongo watu wanafahamu kinachokuja mbele miezi kabla ya tender kutoka. Siku tender zinawekwa mezani tayari watu wameisha zifunga - wenyewe husema - Mcheza kwao!

Kama shirika la UDA lilikuwa linabinafsishwa kwa kuuzwa hisa za serikali whether ni serikali kuu au local government; utaratibu uko wazi kuwa CHC ndio wanakuwa wasimamizi wa transactions zote. Kama asemavyo Idd Simba kuwa serikali ilihusishwa katika kila hatua ya uuzaji wa shirika hilo hivyo basi tungetegemea kuwa malipo ya hisa hizo toka Simon group wala yasingepelekwa kwenye account ya UDA ambayo inasemekana ilikuwa na overdraft huko benki bali malipo kwa kawaida yangepelekwa kwenye accont ya CHC na sio accont ya Idd Simba!! Hizo zilizowekwa kwenye account ya Simba ni hongo alilopewa ili kufanikisha uuzaji wa hizo hisa kwa bei poa!!
 
"Tanzania ina vyote isipokuwa Watanzania" Hakika siamini kama haya mambo wafanyao ni watanzania wenzetu, Tatzo ya haya yote ni "JINGA KUU LA NCHI HII CCM"
 
Kumbe yalikuwa maneno yako. Probably ali-quote kimaokosa then. Nimerudi kusoma post yako ya awali na kama nimekuelewa suggestion yako ni kwamba Simon Group walitoa rushwa mapema kabisa ili tenda ya kununua UDA ikitangazwa yao ipite kiulaini. Lakini bahati mbaya kwao, deal ika leak kabla ya tenda kutangazwa. Hapo naweza kusema possibly. Au ulikuwa na maana nyingine mkuu?
Hakuna zaidi...yote ni ktk kutazama posibility ya kile kilichotokea..
Ukimsoma Simba na Kisena utaona kulikuwepo kweli mazungumzo ya kuuziana (kutapeliana). Simba akidai Simon walitaka ushauri - kuhusu nini? Simba hasemi kuhusu nini hata baada ya Kisena kusema hawakuwa na mazungumzo yeyote zaidi ya kununua Hisa UDA..Kwa hiyo hii pekee inamweka Simba ktk picha ya kuhusika.

UDA ni shirika la UMMA utaweza kununua vipi hisa mapema kabla ya hata shirika lenyewe kubinafsishwa, kutolewa tender au hata kutangazwa ktk gazeti la serikali?..Picha nzima inaonyesha Simon Group wameingizwa mjini na mzee Simba kisha anawatema kiulaini kwani consultant fee can easly be Tsh 285m/- ikiwa kweli utafanikiwa kununua hisa UDA kwa bei za serikali ya CCM.
Halafu panaponiacha hoi zaidi ni pale Kisena alipodai ati walitaka kuingia kushika Uongozi wa UDA (shirika la Umma) inaonyesha huyu Kisena hajui kabisa utaratibu..Mawili, aidha huyo Kisena ni kati ya watu waliojaliwa utajiri kupitia waganga wa kienyeji au ndio kutofahamu utaratibu wa ununuzi wa hisa ktk mashirika..
 
Kama shirika la UDA lilikuwa linabinafsishwa kwa kuuzwa hisa za serikali whether ni serikali kuu au local government; utaratibu uko wazi kuwa CHC ndio wanakuwa wasimamizi wa transactions zote. Kama asemavyo Idd Simba kuwa serikali ilihusishwa katika kila hatua ya uuzaji wa shirika hilo hivyo basi tungetegemea kuwa malipo ya hisa hizo toka Simon group wala yasingepelekwa kwenye account ya UDA ambayo inasemekana ilikuwa na overdraft huko benki bali malipo kwa kawaida yangepelekwa kwenye accont ya CHC na sio accont ya Idd Simba!! Hizo zilizowekwa kwenye account ya Simba ni hongo alilopewa ili kufanikisha uuzaji wa hizo hisa kwa bei poa!!
Mkuu wangu mbona nawe unachanganya vitu.. Account ya UDA imetoka wapi tena? Mkuu tunazungumza kitu kimoja isipokuwa kwa mtazamo tofauti. Labda nambie kitu kimoja hao CHC walikuwa wanauza hisa za UDA? na uuzaji huo upo ktk gazeti gani la serikali au hata hao CHC wako DSE?..iweje Simon group wawalipe CHC ktk ununuzi wa hisa wa shirika ambalo bado halija binafsishwa..
 
Nchi hii nayo imezidi kuwa kama shamba la bibi! Si wageni,si wazawa....wote wanavuna tu ata wasichopanda!
 
Idd Simba ni tapeli, Magamba Robert Kisena kaingizwa chaka. Ndio maana anahaha kusingizia kuwa eti ni sehemu ya malipo ya UDA bali ni dili ambalo walielewana kuwa nipigie pande ninunue share za UDA nitakupa mshiko. Simba alifanya hivyo na kufanikiwa. Robert alipogundua deal ni batili ndo akaanza kuhaha. Hii ni Bongo

hahahahahu ndio ushauri anao ongelea IDDI SIMBA kuuza maneno
sasa huko tayari kufukuzwa hapo kwenye bodi kwa kugonganisha maslahi lakini ROBERT kaliwa
unacheza na vibabu vya mjini wewe
 
unafiki aliowafanyia wachungaji wa dECCI utamtafuna iddi simba mpaka ajute:kev:
 
huwezi lipa consultancy fees karibia sawa na capital bandugu! Anyway mjomba Simba ,kama una consultancy co.haina akaunti mpaka atumie personal? Any consultancy agreement stating the chargeable fees? Huo mwezi ilipolipwa hiyo fees Vat return zenye hiyo amount zilipelekwa tra?
 
Back
Top Bottom