Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu
tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. huu ni sawa na uuaji kwani kwa kufanya hivyo maslahi na maisha ya watanzania wengi yako hatarini.
eee mwenyezi mungu wape moyo wa uoga wote wenye moyo wa namna hii!
kweli inaudhi, lakini TIME WILL TELL!
"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.
"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."
Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;
"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.
Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.
Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.
Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.
Uuzwaji wa UDA kwa Simon Group ni kwa faida ya walalahoi wa Dar es Salaam, watanzania ni watu wa ajabu sana, angekuwa ameuziwa mgeni msingekuwa na tatizo lolote lakini leo kauziwa mtanzania mwenzenu basi maneno kibao,lipi jema kwenu, acheni wivu,*
Mkuu,
Katika makubaliono ya mauzo ya UDA (ambayo hata hivyo hayatambuliwi kisheria), Simon Group Limited ilitakiwa kulipa Sh1.4 billion kwa shares 51. Hata hivyo Simon Group Ltd imelipa Sh285 million (asilimia 12 tuu ya malipo yote) na kukabidhiwa UDA. Unaona hili ni sasa sawa kabisa? Kwa vile basi ameuziwa mzawa basi unaona hilo ni sawa? Walalahoi wamepata faida gani hapo? Yaani wewe ni mtu wa ajabu sana. Hakuna cha wivu hapa. Tumewashika pabaya. Na bado mtasemana, tena sana.
Serikali inasubiri nini kuwakamata wote na kuwanyonga?ushaidi upo wazi so wanachunguza nini?
Idd Simba mwizi na Robert Kisena mwizi sijui kwanini hawakamatwi na kuwekwa lupango haraka sana ili kuanza kuwahoji kwa wizi waliotaka kuufanya.