Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

Idd Simba ni tapeli, Magamba Robert Kisena kaingizwa chaka. Ndio maana anahaha kusingizia kuwa eti ni sehemu ya malipo ya UDA bali ni dili ambalo walielewana kuwa nipigie pande ninunue share za UDA nitakupa mshiko. Simba alifanya hivyo na kufanikiwa. Robert alipogundua deal ni batili ndo akaanza kuhaha. Hii ni Bongo

Tena hii ni bongo Darisalamu. Abiria chunga mzigo wako
 
ya ununuzi huo ktk account ya mtu?.
2. Nataka kuuliza hivi kweli UDA ipo ktk soko la DSE na kama haipo hawa simon walipata wapi wazo la kwamba UDA iinauza hisa zake na kwa kupitia gazeti gani la serikali.. Na hata kama ikiwa kweli ununuzi wa hisa unafanyika vipi kwa mnunuzi wa hisa ktk shirika ambalo lipo DSE. Unanunua shares kwa kupitia account ya Idd Simba kweli?.. hii kweli inaingia akilini mwenu jamani..

Hapa kuna jambo limefanyika na kwa sababu jipu limepasuka na wananchi tumelijua hili mbele ya kile kilichotaka kutokea. Kuna mchezo mchafu sana unafanyika hapa na harufu ya rushwa inaendelea kujionyesha kwani binafsi naamini kabisa kwamba Simon group walitoa fedha hizo kama hongo RUSHWA ( Hearsay and circumstantial) ili tender yao ya ununuzi wa UDA ipite, sasa ilipokuja gundulika njama nzima za Uuzaji wa UDA kila mtu anaruka na Simon group wanashindwa kuzi account milioni 285 (just under Usd 200,000) ambazo walitoa kama rushwa ktk ununuzi wa UDA..Haiwezekani 285m/- kuwa sehemu ya malipo ya ununuzi wa mali zote za UDA ikiwa leo kiwanja cha nyumba ya vyumba sita Kinondoni au Migomigo kinauzwa kwa bei hiyo hiyo..[/QUOTE]


ACHA MASWALI FINYU
Usipoteze network, sio maneno yote ya Kihasibu au ya kihesabu yanatumika kama yalivyo,
Neno Share kwa kiswahili ni nini?
Define the following
Partnership?
Sharing?
Share?
Earning per share?
Sole propriator?
Mengine mengi
kama vile
Ubia?
Ushirikiano?
Kuchangia Uendeshaji?
Na uendeshaji kamili
bila kusahau Mugawo kwa kutumia KKS KDS
Think kwa mapana
mwweeeee
 
Wakuu zangu,
Pamoja na kutompenda Idd Simba lakini tujaribu kutumia akili japo kidogo ktk kutazama sakata hili..
1. Hivi kweli inawaingia akilini nyie kwamba shirika au mtu anaweza kutaka kununua hisa za UDA (shirika la Umma) akalipa sehemu ya ununuzi huo ktk account ya mtu?.
2. Nataka kuuliza hivi kweli UDA ipo ktk soko la DSE na kama haipo hawa simon walipata wapi wazo la kwamba UDA iinauza hisa zake na kwa kupitia gazeti gani la serikali.. Na hata kama ikiwa kweli ununuzi wa hisa unafanyika vipi kwa mnunuzi wa hisa ktk shirika ambalo lipo DSE. Unanunua shares kwa kupitia account ya Idd Simba kweli?.. hii kweli inaingia akilini mwenu jamani..

Hapa kuna jambo limefanyika na kwa sababu jipu limepasuka na wananchi tumelijua hili mbele ya kile kilichotaka kutokea. Kuna mchezo mchafu sana unafanyika hapa na harufu ya rushwa inaendelea kujionyesha kwani binafsi naamini kabisa kwamba Simon group walitoa fedha hizo kama hongo RUSHWA ( Hearsay and circumstantial) ili tender yao ya ununuzi wa UDA ipite, sasa ilipokuja gundulika njama nzima za Uuzaji wa UDA kila mtu anaruka na Simon group wanashindwa kuzi account milioni 285 (just under Usd 200,000) ambazo walitoa kama rushwa ktk ununuzi wa UDA..Haiwezekani 285m/- kuwa sehemu ya malipo ya ununuzi wa mali zote za UDA ikiwa leo kiwanja cha nyumba ya vyumba sita Kinondoni au Migomigo kinauzwa kwa bei hiyo hiyo..

Mkandara, alibi waliyopanga kutumia kutokea imesha pishana kwenye mainstream media. Ni bahati mbaya tu kwani haijatolewa under oath, else ambacho kingelifanyika hapa ni prosecution tu wala si kutupozea muda na kamati za uchunguzi!!
 
Idd Simba alifilisi kampuni ya EAST AFRICAN MEAT CO.kampuni hii ndio iliyokuwa imeanzishwa na Keenja kujenga machinjio ya kisasa katika kiwanja KILTEX GONGO LA MBOTO baada ya kuvunjwa Tume kampuni hii ilirithiwa na manispaa 3 za Dsm na Jiji na kila halmashauri ilichangia zaidi ya million200 Yeye kwa kutumia kampuni yake ya NICO na nafasi yake ya ubunge aliukwaa UENYEKITI wa kampuni hii na kumtafuta meneja kutoka zimbabwe na hatimaye kuifilsi kabisa kampuni hii pamoja na michango iliyotolewa na Halmashauri za DSM na mradi wa machinjio kuamuliwa ufutwe kabisa na KILTEX kubaki magofu.
 
Gazeti la majira la leo linaripoti kuwa Idd Simba anadai ile pesa aliyoingiziwa kwenye akaunt yake na mnunuzi (Simon) haihusiani na mauzo ya UDA bali ni consultancy fees (yaani malipo ya ushauri wa kitalaam) alioutoa kwa SImon Group. SImon yeye anadai hajawahi kupata ushauri wa kitaalam kutoka Idd SImba bali pesa hiyo ni malipo ya ununuzi wa UDA. Yaani ni full utata....

Habari yenyewe hii hapa

[h=3]Kashfa UDA - Idd Simba azungumzia kilichotokea[/h]


Iddi Simba ajibu tuhuma dhidi yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd.

Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela.

"Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza;

"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;

"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.

Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.



ILa sifikirii kama Kissena atakuwa na uwezo mdogo sana asijue alichokuwa anakifanya kwamba hawezi kutofautisha bei ya ununuzi wa hisa na consultancy fee,hapa lazima Idd Simba atuambie vizuri.Na ni vipi Idd Simba yeye mwenyewe awe Mwenyekiti wa bodi halafu pia anatoa ushauri kwa kampuni ambayo baadae atakuja kuijadili??????????this is a serious conlict of interest and gross violation of the principles of natural justice " in nemo judex in causa sua"
 
Mkuu, point yake ya tatu nadhani inamweka kwenye upande wa mwangaza!!

Mkuu maswali aliyouliza sidhani kama ndio yanatakiwa kuwa ya kwanza. Hapo kama nimemwelewa (correct me if I am wrong) kama vile anajaribu ku deviate from the main issue. Issue hapa ni kwamba kulikuwa na umuhimu wowote kwa UDA kuuzwa wakati ingeshirikishwa moja kwa moja kwenye project ya DART? Hata kama kulikuwa na huo umuhimu, uuzwaji umefuata sheria? Wapi uliona serikali imetangaza tenda ya kuuza shares zake UDA?
 
mmmm maskini Tanzania yangu,hvi mpaka lini tutafanywa majuha???kweli we need changes as soon as possible
 
ILa sifikirii kama Kissena atakuwa na uwezo mdogo sana asijue alichokuwa anakifanya kwamba hawezi kutofautisha bei ya ununuzi wa hisa na consultancy fee,hapa lazima Idd Simba atuambie vizuri.Na ni vipi Idd Simba yeye mwenyewe awe Mwenyekiti wa bodi halafu pia anatoa ushauri kwa kampuni ambayo baadae atakuja kuijadili??????????this is a serious conlict of interest and gross violation of the principles of natural justice " in nemo judex in causa sua"

Mkuu uko right kabisa. Hawezi kusema kuwa kwa vile yeye si mwajiriwa, then the fundamental principles of natural justice hazi- apply kwake. Hapo atakuwa amekosea. Conflict of interest inatokea kwa mtu yoyote, whether or not ni mwajiriwa, anapojihusisha kwenye multiple interests, one of which could possibly corrupt the motivation for an act in the other. That is exactly what happened to Idd Simba. Kitendo chake cha kutoa ushauri kwa Simon Group kununua UDA wakati anajua wazi kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ime corrupt motivation yake ya kulitetea UDA. Nashangaa hata mwanasheria wake aliyenda nae kwenye vyombo vya habari hakuliona hili?
 
Mkuu maswali aliyouliza sidhani kama ndio yanatakiwa kuwa ya kwanza. Hapo kama nimemwelewa (correct me if I am wrong) kama vile anajaribu ku deviate from the main issue. Issue hapa ni kwamba kulikuwa na umuhimu wowote kwa UDA kuuzwa wakati ingeshirikishwa moja kwa moja kwenye project ya DART? Hata kama kulikuwa na huo umuhimu, uuzwaji umefuata sheria? Wapi uliona serikali imetangaza tenda ya kuuza shares zake UDA?

Yeah, maelezo yake ni yale ya funika kombe mwanaharamu aselebuke!!!

Anakubali kuwa malipo ya 51% shares ni 1.2 billion, hapo hapo anasema mali ya UDA ni kwenye tune ya 13 billion...
 
Iddi Simba jaman tumekukosea nini wana wa nchi hii mpaka ututendee hivyo?

.....Wakati mwingine watu wanajuta kuwa Watanzania, sababu ndo Kama hizi!
Hivi huyu jamaa ni Mtz kwani? just curious
 
Mkuu uko right kabisa. Hawezi kusema kuwa kwa vile yeye si mwajiriwa, then the fundamental principles of natural justice hazi- apply kwake. Hapo atakuwa amekosea. Conflict of interest inatokea kwa mtu yoyote, whether or not ni mwajiriwa, anapojihusisha kwenye multiple interests, one of which could possibly corrupt the motivation for an act in the other. That is exactly what happened to Idd Simba. Kitendo chake cha kutoa ushauri kwa Simon Group kununua UDA wakati anajua wazi kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ime corrupt motivation yake ya kulitetea UDA. Nashangaa hata mwanasheria wake aliyenda nae kwenye vyombo vya habari hakuliona hili?

Dude, these klepto mofxx gotten used to eazy money to the extent that can't even think to cover up their sickening trails!!!
 
Hivi Idd Simba alichaguliwa na nani huko UDA? Na ninani alimchagua kuongoza PRIDE? Kama ni board members then ingekuwa vizuri tuwajuwe kwa majina hao board members wa hizi kampuni mbili. Tusaidiane kwenye hili.
 
Service by za UDA zimegeuzwa kuwa maghala?


attachment.php




attachment.php


attachment.php



attachment.php
 
Mkuu maswali aliyouliza sidhani kama ndio yanatakiwa kuwa ya kwanza. Hapo kama nimemwelewa (correct me if I am wrong) kama vile anajaribu ku deviate from the main issue. Issue hapa ni kwamba kulikuwa na umuhimu wowote kwa UDA kuuzwa wakati ingeshirikishwa moja kwa moja kwenye project ya DART? Hata kama kulikuwa na huo umuhimu, uuzwaji umefuata sheria? Wapi uliona serikali imetangaza tenda ya kuuza shares zake UDA?
EMT, umemwelewa vizuri huyu mtu wa magamba, yeye kwa akili yake anajaribu kufanya watu waache kujadili issue mzizi na kujidai eti ni wivu kwamba UDA imeuzwa kwa mzawa. Hebu aonyeshe ni wapi ambapo mtu hata mmoja amelalamikia kuwa UDA imeuzwa kwa mzawa na ndio tatizo.

Watu wengine kweli wanatia maudhi, yaani jitu limefaidika na visenti sasa lina haha kutetea hata sehemu ambapo ukweli uko wazi. Iko mingi sana mijitu ya aina hii, yote ingekula shaba tu na mabwana zao.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Baada ya miaka 5 .. wanapewa kanga .. wanapigia kula CCM!... sometimes inabidi tujilaumu wenywe wa tanzania... CCM ndio chanzo cha mambo yote haya
 
ACHA MASWALI FINYU
Usipoteze network, sio maneno yote ya Kihasibu au ya kihesabu yanatumika kama yalivyo,
Neno Share kwa kiswahili ni nini?
Define the following
Partnership?
Sharing?
Share?
Earning per share?
Sole propriator?
Mengine mengi
kama vile
Ubia?
Ushirikiano?
Kuchangia Uendeshaji?
Na uendeshaji kamili
bila kusahau Mugawo kwa kutumia KKS KDS
Think kwa mapana
mwweeeee
Mkuu hata sielewi unachozungumza hapa...Kwanza isome habari kamili iliyotangulia kisha yasome majibu yangu. Na matumizi ya neno share yanatokana na madai ya Simon group kununua hisa unataka niseme kipi zaidi ya ku question kila sehemu ya Ubia huu. Hata hivyo, hiyo share kwa kiswahili maana yake ni hisa...si ndivyo unataka?..
Kama ungesoma maelezo YOTE ya mwanzo wa mada hii ya Kaburunye, kusingelikuwa na sababu ya kuvamia tafsiri ya maelezo yangu kwa jinsi unavyofikiria wewe iwe kwa kiingereza au kiswahili hoja kubwa ni ununuzi huu wa hjisa hauna kichwa wala miguu, haijalishi ni ushirika wa aina gani.

Kifupi mkuu wangu - UDA bado ni shirika la Umma. Hivyo haiwezekani kuwepo mkataba wowote wa Ubia iwe ktk ngazi yeyote ya ushirika bila kwanza hiyo UDA kubinafsishwa. Kwa hiyo ndio maana nimeweka sehemu mbili ya maswali ya kujiuliza, hata kama UDA imefikia kuuza hisa. Moja ni ile ya kununua ubia kwa kuweka fedha account ya Idd Simba ambaye sii mmiliki wa shirika hilo ila mwajiriwa. Pili sehemu nyingine ya kununua hisa ni DSE (Idd Simba nako yuko), nimeuliza vile vile na bado nimeshuku mpango mzima kwa sababu haiwezekani ujinga huu kufanywa na watu wenye kuelewa Hisa..

Mwisho mkuu wangu umeniomba nitoe definition ya maneno hayo mbona wewe mwenyewe hukutoa maelezo yoyote kisha wanitaka mimi niseme ili iweje? Samahani mkuu kama mawazo yangu yamekukwaza lakini ukweli unajionyesha hii ni RUSHWA ilojamba sasa mnatafuta pa kutokea...
 
Hawa wana ccm wanawachezea watanzania wala sioni haja ya uchunguzi maana haya ni mambo ya pwagu na pwaguzi watasindikizana mpaka panakucha mwenyekiti wa bodi anatoa consultancy kwa mnununuzi wa kampuni yake ambayo ni mali ya umma!hii danganya toto kwa akili timamu malipo yaliyokwanda kwa idd simba ni facilitation fee bt simon alijifanya mjanja kwa kulipa kwa akaunti ili awe na guarantee but imekula kwake
 
Hii kwangu naona ilikuwa deal kati ya Robert Kisena & co na Idd Simba & Co lakini wakashindwa kuelewana na sasa mambo yote hadharani. Pande zote mbili maelezo yao haya make sense; wanajichanganya, wanatoa maelezo tofauti tofauti etc. Kama walivyosema wengine hawa wote ni wezi tu. Hata kama shirika lingekuwa linauzwa kiuhalali transaction yenyewe imefanyika kihuni sana. Hivi kulikuwa hamna mwanasheria aliyekuwa anasimamia? au kwamaana nyingine UDA ina mwanasheria wake?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom