Saikolojia: Jinsi mnunuzi anavyoshindwa kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kazi ya kununua nyumba ni kazi rahisi sana ukilinganisha na kazi ya kuuza nyumba hasa kwa wanunuzi wa nyumba wasio wawekezaji.

Ni vigumu kupata wanunuzi wa nyumba kuliko kupata nyumba unayotaka endapo una fedha tayari za kununulia nyumba unayoitaka.

Kwa lugha nyingine, utatumia muda mrefu kupata wanunuzi wazuri wa nyumba kuliko muda utakaotumia kununua nyumba.

Dalali wa viwanja na nyumba hupata matangazo mengi ya watu wanaouza nyumba kuliko matangazo ya watu wanaonunua nyumba kwa sababu kuna ugumu kwenye kuuza nyumba.

Wakati wa kununua nyumba huwezi kufahamu hasara ya moja kwa moja, hii hupelekea uzembe wa kununua nyumba bila uangalifu.

Lakini wakati wa kuuza nyumba hasara inajulikana wazi kwa mmiliki wa nyumba husika na timu yake ya uwekezaji kwa ujumla.

Maumivu wa kupata hasara kubwa ya kifedha wakati wa kuuza nyumba huwafanya wawekezaji wengi kuendelea kupambana mpaka wauze kwa faida nzuri.

Wakati wa kununua unaongozwa zaidi na hisia ya kupata sio kupoteza. Wawekezaji ambao hushindwa kuona faida za kifedha kwa uwazi kwenye akili zao hushindwa kuweka umakini wakati wa kununua nyumba.

Mfano; mwekezaji akijenga nyumba na kuamua kuuza. Mwekezaji huyo atakuwa anatoa shuhuda kwa anayemuuzia kuwa ujenzi unagharimu fedha nyingi sana hawezi kupunguza chini ya kiwango fulani.

Wakati huohuo mwekezaji huyo hana ripoti ya jumla ya gharama za ujenzi wa nyumba yake. Mbaya zaidi hakuandaa ripoti ya makadirio ya mapato na matumizi wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba yake.

Kusukumwa na hisia ya kupata fedha inawapoteza wengi wakati wa kununua nyumba ukilinganisha na kusukumwa na hisia ya kupoteza mtaji fedha wakati wa kununua nyumba.

Mwekezaji anajenga nyumba kwa shilingi milioni hamsini (50) nyumba ambayo ataiuza kwa milioni arobaini (40).

Kwa kuwa hakufanya tathimini vizuri, huchanganyikiwa na kujihisi amepoteza wakati wa kuuza nyumba. Kwa maneno haya machache, ndiyo sababu kununua nyumba ni rahisi kuliko kuuza nyumba.

Saikolojia Ya Mnunuzi Wa Nyumba.

1. Jicho la mnunuzi wa nyumba huona kasoro ni tatizo

Mnunuzi wa nyumba huona kasoro kama kikwazo na hivyo kuogopa kununua nyumba zenye kasoro.

Kasoro zinazohitaji ukarabati na maboresho huwa kero kubwa kwa wanunuzi wengi wa nyumba.

Wakati huohuo mwekezaji kwenye nyumba huona kasoro zilizo kwenye nyumba ni fursa ya kuongezea thamani nyumba husika.

Nyumba inapokuwa na choo chenye kasoro mwekezaji hutumia kasoro hiyo kuomba punguzo la bei ya nyumba. Wakati huohuo mnunuzi huiona nyumba hiyo haina thamani kabisa na kuachana nayo.

2. Mnunuzi wa nyumba huona kile kinachoonekana

Mnunuzi wa nyumba hana muda wa kufikiria kuhusu matumizi ya nyumba kabla ya kuwa vile ilivyo.

Nyumba ambayo haijapkwa rangi hukosa mvuto kwa wanunuzi wengi na kuonekana haitaweza kutumika vizuri kwa malengo yake.

Nyumba ambayo ina bustani mbaya na haijafanyiwa matengenezo hukosa mvuto kwa wanunuzi waliowengi. Hii hupelekea kuchelewa kuuza nyumba au kukosa wanunuzi kabisa.

Mnunuzi huamini kuwa nyumba ambayo haijapkwa rangi ni kiashiria kikubwa cha uwepo wa matatizo mengine ambayo hayatambui kwa macho yake.

3. Mnunuzi huweka umakini mkubwa kwenye vitu visivyokuwa na umuhimu

Wanunuzi wengi wa nyumba hawana vigezo vinavyo waongoza kufanya maamuzi ya kuchagua aina fulani ya nyumba.

Kwakuwa huona aina nyingi za nyumba, huwafanya kuvutiwa na sifa nyingi tofauti tofauti.

Wasipoiona sifa ambayo waliiona kwenye nyumba nyingine husita kununua nyumba. Huweka vipaumbele kwenye sifa ambazo hazina umuhimu wowote kwenye nyumba husika.

Mfano A: mnunuzi anahitaji nyumba ya kupangisha lakini anaanza kutafuta nyumba ya paa iliyoinuka sana. Paa iliyoinuka haina umuhimu wowote kwa wapangaji bora.

Mfano B; mnunuzi anataka kununua nyumba ya kuuza lakini hataki kuona kasoro yoyote ya kumfanya afanye ukarabati. Kitu ambacho kitamzuia yeye kuongeza thamani ya nyumba anayonunua.

Mnunuzi anaanza kutafuta umbo la nyumba zuri ambalo hata haiongezi thamani yoyote kwenye nyumba kulingana na mahitaji ya wapangaji wake.

Kwa namna hii ya kutafuta sifa za nyumba zisizo na thamani mnunuzi hushindwa kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba husika.

4. Huchagua nyumba kamilifu au nyumba ya kuhitaji ukarabati rahisi sana

Wakati wa kuuza nyumba, ukiwa na nyumba ambayo ina kila kitu ni kivutio kikubwa kwa wanunuzi wa nyumba.

Wanunuzi hawapendi usumbufu wa kufanya ukarabati wa nyumba na kuwasimamia mafundi ujenzi.

Hupenda kununua na kuanza kuitumia hata kama itawagharimu kiasi kikubwa cha fedha kuliko wangefanya wao wenyewe ukarabati wa nyumba.

Nyumba ambayo haitaji ukarabati na maboresho hupata wanunuzi haraka zaidi ukilinganisha na nyumba inayohitaji ukarabati zaidi ya kasoro moja.

Hakikisha nyumba yako haina kasoro ikiwa unahitaji kuuza kwa haraka na kwa faida nzuri.

Wanunuzi kutopenda kununua nyumba zenye kasoro ndiyo sababu mojawapo ya kushindwa kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba.

5. Dalali wa viwanja na nyumba hulenga hisia za wanunuzi wa nyumba

Dalali wa viwanja na nyumba hulenga hisia za wanunuzi wa nyumba kwa sababu dalali hulipwa kwa kufanikisha mauzo ya nyumba.

Ili aweze kuuza nyumba kwa haraka zaidi anahitaji kuweka shabaha kwenye hisia za mnunuzi wa nyumba. Hisia mojawapo ya mnunuzi wa nyumba ni kupenda kinachoonekana kwa wakati huo.

Hivyo dalali atahakikisha nyumba ipo safi, imepangiliwa vizuri, imepandwa bustani nzuri, nyumba imepakwa rangi nzuri na kadhalika.

Kama kuna sifa ambazo zinawavutia sana wanunuzi wa nyumba kwenye halmshauri husika, dalali atamshauri muuzaji wa nyumba kuweka sifa hizo kwenye nyumba.

Kitendo cha kuongeza sifa kwenye nyumba kwa ushauri wa dalali kinaweza kumfanya muuzaji kupata hasara au kutengeneza kiasi kikubwa cha faida baada ya kuuza.

Muuzaji atatengeneza kiasi kikubwa cha faida baada ya kuuza ikiwa atakarabati na kuboresha nyumba kwa makadirio mazuri.

Ni muhimu sana kujifunza kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba badala ya kupambana kutengeneza fedha wakati wa kuuza nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom