Safarini Dar: Msaada wa hoteli nzuri bei ya wastani

Haahaa,,Hotel za ninii we sema tu nije nikupokee,,ila jitahidi uwe unanizidi umri,,ni kikuta kasichana na zima simu,,Ni Pm,,,nitakuwa mwenyeji wakoo
 
ukifika Ubungo chukua bajaj buku mbili njoo shekilango rombo green view.
ni hoteli safi iko karibu na Huduma nyingi unapata usafiri wa kwenda popote kwa kutumia daladala moja bila kuunganisha.
pia kuna Huduma zote muhimu jirani. bei ni kuanzia 35000.
ukifika ni pm.
 
Wana MMU, hasa wa Dar na Dom. Ninasafari ya Dar, Naombeni kujua hotel/lodge nzuri jirani na Stendi ya mabasi ya mikoani. Iwe ya bei ya wastani kama shilingi 20,000 hadi 30,000 kwa siku. Iwe jirani na chakula kinapopatikana na pia isiwe vichochoroni.

Pia Lodge yenye sifa hizo hizo kwa Dodoma.

Msaada wenu, marafiki
Tafuta couch surfing
 
Mimi nadhani nimeathiriwa na tabia nchi, nitakwenda kinondoni lakini siyo Manzese, huu ndio ukweli wangu.

Mimi hata Magomeni nimeanza kwenda juzijuzi tu baada mchizi wangu mmoja kupata mjengo wa bei nafuu pande hizo.

Unaweza usinielewe, hata kariakoo mimi ndio tofauti kabisa siku nikipita kariakoo basi kuna kitu muhimu sana siwezi kukipata sehemu nyingine zaidi ya Kariakoo.
haujaathiriwa na tabia nchi, sema ushua wako tu mkuu. Hoteli zipo nyingi nzuri.
 
Nenda Kagame hotel iko nyuma ya ubungo stand karibu na ubungo Plaza utapata room ya 30,000 nzur kbsa kitanda kikubwa half ni wasafi sana


"Iko nyuma ya Ubungo stand, alafu karibu na Ubungo plaza"?!!!!

Mkuu unaielewa hiyo sehemu vizuri? au ulihadithiwa tu?

-Kaveli-
 
Beauty Eva, usihangaike Mkuu. Kwa hotel nzuri ambazo zipo karibu zaidi na Ubungo Stand, yaani kutembea kwa mguu dakika 8, ni MIC HOTEL au KIBADAMO HOTEL.

MIC hotel, vyumba vipo vya kuanzia Tsh 35,000 kwa siku.

KIBADAMO hotel, vyumba vipo kuanzia Tsh 25,000 kwa siku. Restaurant nzuri ya kula ipo jirani tu hapo inaitwa Pazuri Garden. Pia waweza amua kunyoosha miguu na kwenda kula sehemu zingine za jirani hapo.

Hizo hotel zipo karibu kabisa na Ubungo Bus Terminal. Ukipata vyumba vya juu ghorofani, stand unaiona ileee. Ni friendly zaidi kwa mgeni mwenye mishe zake downtown, coz dakika 8 tu unafika road na stendi ya daladala ipo hapo hapo, mwendo-kasi pia unapandia/unashukia hapo hapo.

Ukishuka Stand, wala usipate tabu, njoo nje ya stand pale getini utaona Taxi na bodaboda nyingi tu, kwa Taxi bei haizidi Tsh 3,00 kwenda pale.

Kama umefika mapema (sio usiku), basi ulizia tu uende kwa mguu, dakika 8 maximum kufika. Ila angalia na mtu wa kumuuliza, sio unamuuliza teja mpiga debe eti MIC hotel iko wapi, ataona fursa hii then utakaribishwa DarSlum kwa kusomeshwa namba za kirumi.

Kwa vile ni mgeni, to be on safe side chukua tu taxi, bei haizidi sh. elfu 3. Au bajaji or bodaboda sh elfu moja tu.

Mic na Kibadamo zipo jirani. Inaanza Mic, then kwa mbele zaidi ni Kibadamo.

Wish you an enjoyable stay in DarSlum jiji la Makonda. Take maximum care and be risk-conscious.

Endapo utaamua kufanya utalii wa ndani ya jiji, usiishie kwenda kucheck mnara wa askari tu, au daraja la kigamboni tu, bali karibu pia huku kwetu Mbagala kwenye hewa safi.

-Kaveli-
 
Golden Palm hotel tsh 20,000 tu..ukishuka stendi ya mkoa unavuka barabara unafuata road ya ubungo maziwa mbele kama kilometa 1 tu utaikuta...ni ya gorofa ina rangi nyeupe...ipo njiani kabisa.
Asee itabid nije hapo niulete mchepuko wangu
 
Kwa Dar sehemu jirani na stendi ya ubungo ni Sinza, Sinza kuna hotel kibao good quality ila bajeti weka kuanzia 40,000/=
Sinza kijiweni kuna Golden park na pacha yake iko jirani nimeisahau jina.

Hiyo 20,000/= au 30,000/= waweza ishia nyumba za ngono tu ambazo ni maalum kwa watu kulana mauloda.

Hotel zina raha na status yake, si kila anayelala hotel yupo kwenye malengo ya ngono na ndio maana hazina short time.

Mimi nimekoma kulala kwenye Guest house maana yale mashuka yananukia janaba muda wote tena waweza jitia nuksi tu.
Nimecheka sanaaaa!!
 
Aende best point ubungo riverside...wanaprovide breakfast...ni kuanzia 45000 hadi 80000, Pako vizuri. Kama una nia ya kukaa karibu na stend ya mabasi ya mikoa pale patakufaa.
 
NENDA MANZESE NDO KILA KITU KWASASA HAPA DAR ES SALAAM WAKINGA WAMEJENGA MAHOTELI YA KUFA MTU TENA JIRANI ROADS KWA BEI HIYO TAJWA
 
Kumbe kuna breakfast pale, duuuuh mi nililala tena chumba chenye AC halafu asubuhi nikasepa tu.....
Wana breakfast ambayo ukila kila kitu huhitaji kula lunch, na ni varieties ya vyakula halafu vimeandaliwa vizuri mno pamoja na fresh juice
 
Hahhahahaaaa ngoja tusibishane bure tafuta siku nikuchukue ziara
Serious speaking mambo yanapinduka siku hizi huku kunakuwa kule na kule kunakuwa huku
Hizi zote nilizotaja ziko pembeni ya morogoro Rd na zinafikika kwa urahisi sana lakini hebu niambie kule Sinza mfano ukitaka kwenda Namnani
Msipigwe roba tu...hahaha
 
Wana MMU, hasa wa Dar na Dom. Ninasafari ya Dar, Naombeni kujua hotel/lodge nzuri jirani na Stendi ya mabasi ya mikoani. Iwe ya bei ya wastani kama shilingi 20,000 hadi 30,000 kwa siku. Iwe jirani na chakula kinapopatikana na pia isiwe vichochoroni.

Pia Lodge yenye sifa hizo hizo kwa Dodoma.

Msaada wenu, marafiki
Mkuu zipo nyingi tu, kuna Kagame hotel, pia Whitemark zote hizo zipo Ubungo karibu tu na ubungo.
 
Back
Top Bottom