A
Anonymous
Guest
Ratiba ya mabasi hayo yanaanza kutoka Rombo saa 9 usiku na basi la mwisho saa 11 alfajiri. Jambo hili licha ya kuleta usumbufu kwa abiria lakini pia linahatarisha usalama wa abiria kutokana na mazingira ya eneo husika.
Maeneo mengi ya Rombo yametawaliwa na uoto uliofungamana (miti, vichaka na migomba) na pia watu hutegemea usafiri wa bodaboda ili kufika kwenye barabara kuu au stendi ili kupanda magari. Kutokana na maeneo mengi kuwepo pembezoni sana watu hulazimika kuanza safari mapema (kuanzia saa nane usiku) jambo ambalo ni hatari na pia ni vigumu kupata msaada wa haraka pindi watakapovamiwa na wahalifu au wanyama wakali.
Hili limepelekea baadhi ya abiria kwenda kuanzia safari zao njia panda ya Himo pindi kunapopambazuka ili kuepuka hayo.
Kutoka Rombo mpaka Dar gari hutumia takribani masaa nane mpaka kumi, jambo ambalo hakuna ulazima wa kuanza safari usiku hivyo. Lakini pia hakuna sababu ya msingi iliyotolewa ya kubadilisha ratiba ya mwanzo ambayo mabasi yalikua yanaanza safari zake saa 11 na nusu alfajiri mpaka saa 1 kasoro asubuhi.