Safarini Dar: Msaada wa hoteli nzuri bei ya wastani

Safarini Dar: Msaada wa hoteli nzuri bei ya wastani

Wana MMU, hasa wa Dar na Dom. Ninasafari ya Dar, Naombeni kujua hotel/lodge nzuri jirani na Stendi ya mabasi ya mikoani. Iwe ya bei ya wastani kama shilingi 20,000 hadi 30,000 kwa siku. Iwe jirani na chakula kinapopatikana na pia isiwe vichochoroni.

Pia Lodge yenye sifa hizo hizo kwa Dodoma.

Msaada wenu, marafiki
karibu kabisa na stendi ya ubungo kuna hoteli ya 30,000/= na ni ya kiwango kizuri. nafikiri inaitwa kidamo hotel. ukiwa ubungo bus stand unaiona.
 
Tip tipo kweli vilodge vipo vingi lakini mazingira sio mazuri mkuu
Kweli kabisaa tiptop vingi saana mazingira Yake ndani sinashaka nayo ila wakat Wa kwenda na kurudi mmmmmh
 
Ukishuka ubungo elekea moja kwa moja mpaka sinza kisha tafuta lodge au hotel nzuri kwani zipo karibu na stand.

Kuanzia elfu 30 unaweza kupata chumba kizuri.

Ukikosa njoo mpaka mwenge ulale kwangu bure na breakfast asubuhi, maisha kusaidiana.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mkuu mimi ni mzawa wa Dar, nimeshindwa kumuelewa Mshana Jr ni Manzese ipi hiyo nisiyoijuwa mimi mpaka uniconvice kwenda?
Matola,wewe unasema hujakanyaga Manzese kwa zaidi ya miaka kumi. Sasa kwa kkipindi hicho chote kuna mabadiliko makubwa sana ya miundombinu especially kwa mkoa wa Dar tena ktk awamu mbili zilizopita. So Manzese unayoijua wewe siyo ya sasa!
Mkuu mimi ni mzawa wa Dar, nimeshindwa kumuelewa Mshana Jr ni Manzese ipi hiyo nisiyoijuwa mimi mpaka uniconvice kwenda?
 
Mkuu usihangaike sana kuzunguka wala kuchukua tax,ukifika hapo stendi ya ubungo kwa nje utaona hotel moja inaitwa MIC hotel ni nzuri sana inaanzia 45,000/-mpaka 150,000/=
 
Matola,wewe unasema hujakanyaga Manzese kwa zaidi ya miaka kumi. Sasa kwa kkipindi hicho chote kuna mabadiliko makubwa sana ya miundombinu especially kwa mkoa wa Dar tena ktk awamu mbili zilizopita. So Manzese unayoijua wewe siyo ya sasa!
Hata buguruni na vingunguti kuna mabadiriko makubwa ya miundombinu baada ya kunufaika na mradi wa World bank wa DMP, but/lakini buguruni itabaki kuwa buguruni na uswahili wake halikadhalika na Vingunguti pia.

Same applies to Manzese.
 
Matola hapana umeshafika JM hotel? Eraldo Natron je? Silver? Mahanju Inn? Nk nk hizi zote zipo Tiptop ni nzuri zina viwango na bei imepoa
Erado natron hadhi yake sinza nzima hamna yaani huduma bora kwa Tsh 35,000 na breakfast juu huwezi ifananisha na zile taka taka, za sinza
 
Mkuu samahani kama nitakukwaza mimi naishi uswahilini lakini ukishanitajia tu Manzese au Tandale kwakweli mimi hapana.

Sinza ina ustaarabu wake mkuu, ndio maana hizo hotel ni nzuri lakini haziwezi kuwika kwa sababu ya location zilipojengwa.

Sinza itabaki kuwa Sinza tu.
Madhara ya kukariri, sinza ya sasa ni uswahilini kuliko tip top
 
Nakushauri nenda Jm hotel manzese pazuri kuna vyumba vya kuanzia 20 25 30 bed and breakfast restaurant ipo ukitaka msosi unatwanga tu simu pia kila siku kwa wale wasafiri wana gari ya kupeleka wateja stand ya mabasi
Asante sana
 
Erado natron hadhi yake sinza nzima hamna yaani huduma bora kwa Tsh 35,000 na breakfast juu huwezi ifananisha na zile taka taka, za sinza
Hapa unachanganya madesa, hata porini kuna lodge nzuri tu, ili tusibishane sana weka kiwanja tip top na weka kiwanja Sinza kwa ukubwa uleule na bei ileile utapata jibu sahihi.

Yaonekana wewe ni mdau wa Manzese, usipanick Manzese hata siku moja haiwezi kuwa na thamani ya Sinza.
 
Mimi sikai sinza wala manzese hapa mjini ila kwa ukweli sinza ya miaka hii inaboa sana wizi nje nje. Sinza ina vijana wengi ambao hawafanyi kazi wanategemea udokozi, ukipak gar tuu wanakomba spare zotee. Hata ukitoka usiku ukienda kwenye mziki hakikisha haurudi usiku jirudie asubuhi
 
Wizi wa vifaa vya magari ni tatizo la jiji zima, kama matukio hayo yanatokea sana Sinza itakuwa ni kwa sababu Sinza ni sehemu ya matumizi na wale wanyori watakuwa wanatoka maeneo mbalimbali kwenye kupiga timing zao Sinza.
 
Back
Top Bottom