Afisa Ustawi wa Jamii Ubungo: Watu kutoka kanda ya ziwa wanaongoza kutelekezwa na ndugu zao Stendi ya Magufuli

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Taarifa ni kwamba watu wengi wanaotoka mikoani kuja Dar es Salaam wamekuwa wakitelekezwa na ndugu zao stendi ya mabasi ya Magufuli, mamlaka za kituo hicho zimeamua kutangaza kwa kutumia Spika kuhusu ndugu ambao wanatelekezwa au wamekosa mwenyeji.

MIKOA INAYOONGOZA KUTELEKEZA NDUGU ZAO STENDI YA BASI
"Mikoa ya Kanda ya Ziwa yote tukianzia na Mara, Mwanza, Kagera (Bukoba), Geita (inaongoza (ndugu zao kuwatelekeza kituo cha Mabasi Magufuli wanapofika Jijini Dar es Salaam).

Pia kuna Mikoa ya Kigoma, Mbeya, Iringa, Morogoro na Dodoma na hatuna kitu cha kufanya zaidi ya kuelimisha jamii lakini pia tutaomba jamii iweze kuelewa kile ambacho tutakachokifundisha, elimu zinatolewa na tatizo lipo palepale" Naamini Nguve, Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Ubungo.

Naamini Nguve.JPG

Chanzo: Clouds TV

Pia soma - Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi
 
Mtu anakusanya Viroba na ndala zake anakimbilia stendi anapanda Bus mpaka anafika Mlandizi ndio anakupigia sasa.

"Aloo? Ehh Ulimora Baba? Mwangaruka! eeh mimi Mjomba wako mtoto wa Bibi wa Simiyu, Kaka yake Baba Mkubwa, niko hapa MURANDIZI nakuja DAA, Nawomba unipokee hapo Sitendi Magufuri"

Hapo yupo na kitochi na elfu 1 mfukoni, simu yenyewe haina bundle wala chaji.

Hizi ni LAWAMA tunatafutiana.
 
Ndugu zangu Wasukuma punguzeni kula sana, mjini hakuna mashamba vinginevyo sio tuu mtatelekezwa Bali mtafukuzwa pia 😂😂😂😂

My Take
Nyie wa Katoro,Kolomoje,Buselesele na Vijiji vingine kama hivyo Nenda Mjini Ukiwa umebeba unga na dagaa msijifanye hamkufindishwa mgeni karibu mwenyeji apone.

=========

Clouds TV
 
Yeye amewahi kutelekezwa na nani?
 
pokeeni ndugu zenu, waafrika tunasaidiana na hiyo ndo dini inataka hivyo . acheni ulimbukeni wa mjini
 
Taarifa ni kwamba watu wengi wanaotoka mikoani kuja Dar es Salaam wamekuwa wakitelekezwa na ndugu zao stendi ya mabasi ya Magufuli, mamlaka za kituo hicho zimeamua kutangaza kwa kutumia Spika kuhusu ndugu ambao wanatelekezwa au wamekosa mwenyeji.

MIKOA INAYOONGOZA KUTELEKEZA NDUGU ZAO STENDI YA BASI
"Mikoa ya Kanda ya Ziwa yote tukianzia na Mara, Mwanza, Kagera (Bukoba), Geita (inaongoza (ndugu zao kuwatelekeza kituo cha Mabasi Magufuli wanapofika Jijini Dar es Salaam).

Pia kuna Mikoa ya Kigoma, Mbeya, Iringa, Morogoro na Dodoma na hatuna kitu cha kufanya zaidi ya kuelimisha jamii lakini pia tutaomba jamii iweze kuelewa kile ambacho tutakachokifundisha, elimu zinatolewa na tatizo lipo palepale" Naamini Nguve, Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Ubungo.

Chanzo: Clouds TV

Pia soma - Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi
Sasa kama hao ndugu wanakimbilia mjini kishamba kwanini wasitelekezwe? Ndugu wa kijijini wana kawaida ya kuja mjini kwa kukurupuka. Mtu anasafiri kutoka kijijini bila kumtaarifu mwenyeji wake akifika Bus Terminal ndipo anakupigia simu umfuate wakati wewe hujajipanga kumlisha wala kumwandalia mahali pa kulala.

Tatizo mpaka sasa hivi watu wa mikoani wana ile mentality ya kizamani ya kusema: "Kaka yangu anafanya kazi TRA ngoja niende akanitafutie kazi hata ya kufagia hawezi kukosa". Wanadhani utaratibu wa kupeana kazi kizamani na kiholela bado upo. Hili ni tatizo.

Ipo haja kwa serikali kuwaelimisha watu wa kijijini namna nzuri ya kutembelea ndugu zao wa mjini Dar badala ya kukurupuka. Unakuta mtu anaishi na familia yake yote kwenye chumba kimoja cha kupanga, halafu mtu anakurupuka kimyakimya kutoka kijijini akifika Mbezi ndipo anakupigia umfuate. Umfuate uje kumlaza wapi na kumlisha nini?

Jamani tusiwatetee tu hawa jamaa bila kujua jinsi wanavyokurupuka kutoka huko kijijini bila mpango. Mimi hili tatizo liliwahi kunitokea. Nimekaa room sina hili wala lile napokea simu ngeni kutoka kwa ndugu yangu kwamba yupo Ubungo terminal nikamfuate. Kumbe alitumia simu ya abiria mwenzake hana hata simu. Ngoja nipate shida ya kuaga kazini na kumfuata huko Ubungo sasa! Nilikoma.

Baada ya kufika kwangu akakaa tu bila mpangokazi wowote. Fikiria wakati huo nakaa kwenye chumba kimoja kule Kinondoni mtaa wa Mgobanya. Na chumba hichohicho ndicho nakitumia mimi na demu wangu. Ilibidi sasa nianze kuingia gharama za kwenda kulipia pesa loji wakati nina room yangu. Na ghafla gharama za maisha zikapanda na kumbuka sikuwa nimejipanga kuwa na bajeti ya ziada ya kumlisha mtu wa ziada wala sikuwa na chumba cha ziada cha kumlaza.

Kwa hali kama hii unadhani kwanini wageni wasiendelee kutelekezwa? Tumechoka bhana, kama mbwai iwe mbwai!
 
Mtu anakusanya Viroba na ndala zake anakimbilia stendi anapanda Bus mpaka anafika Mlandizi ndio anakupigia sasa.

"Aloo? Ehh Ulimora Baba? Mwangaruka! eeh mimi Mjomba wako mtoto wa Bibi wa Simiyu, Kaka yake Baba Mkubwa, niko hapa MURANDIZI nakuja DAA, Nawomba unipokee hapo Sitendi Magufuri"

Hapo yupo na kitochi na elfu 1 mfukoni, simu yenyewe haina bundle wala chaji.

Hizi ni LAWAMA tunatafutiana.
Mkuu umeandika kwa hisia sana. Yamewahi kukukuta nini? :D :D :D :D :D :D
 
Taarifa ni muhimu popote unapoenda ili sehemu husika wajipange Kwa budget na vinginevyo,,ila kama anakuja bila taarifa hpo lazima utatelekezwa mjini watu wanaishi Kwa mipango
 
Back
Top Bottom