Beauty Eva, usihangaike Mkuu. Kwa hotel nzuri ambazo zipo karibu zaidi na Ubungo Stand, yaani kutembea kwa mguu dakika 8, ni MIC HOTEL au KIBADAMO HOTEL.
MIC hotel, vyumba vipo vya kuanzia Tsh 35,000 kwa siku.
KIBADAMO hotel, vyumba vipo kuanzia Tsh 25,000 kwa siku. Restaurant nzuri ya kula ipo jirani tu hapo inaitwa Pazuri Garden. Pia waweza amua kunyoosha miguu na kwenda kula sehemu zingine za jirani hapo.
Hizo hotel zipo karibu kabisa na Ubungo Bus Terminal. Ukipata vyumba vya juu ghorofani, stand unaiona ileee. Ni friendly zaidi kwa mgeni mwenye mishe zake downtown, coz dakika 8 tu unafika road na stendi ya daladala ipo hapo hapo, mwendo-kasi pia unapandia/unashukia hapo hapo.
Ukishuka Stand, wala usipate tabu, njoo nje ya stand pale getini utaona Taxi na bodaboda nyingi tu, kwa Taxi bei haizidi Tsh 3,00 kwenda pale.
Kama umefika mapema (sio usiku), basi ulizia tu uende kwa mguu, dakika 8 maximum kufika. Ila angalia na mtu wa kumuuliza, sio unamuuliza teja mpiga debe eti MIC hotel iko wapi, ataona fursa hii then utakaribishwa DarSlum kwa kusomeshwa namba za kirumi.
Kwa vile ni mgeni, to be on safe side chukua tu taxi, bei haizidi sh. elfu 3. Au bajaji or bodaboda sh elfu moja tu.
Mic na Kibadamo zipo jirani. Inaanza Mic, then kwa mbele zaidi ni Kibadamo.
Wish you an enjoyable stay in DarSlum jiji la Makonda. Take maximum care and be risk-conscious.
Endapo utaamua kufanya utalii wa ndani ya jiji, usiishie kwenda kucheck mnara wa askari tu, au daraja la kigamboni tu, bali karibu pia huku kwetu Mbagala kwenye hewa safi.
-Kaveli-