Safari za Reli ya SGR Dar Moro zanukia Kuanza Julai 2023

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

NAIBU WAZIRI ATUPELE MWAKIBETE ASEMA SAFARI ZA DAR - MORO KUPITIA RELI YA SGR KUANZA JULAI, 2023

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imepokea mabehewa sita ya reli ya kisasa ya (SGR) ambayo yamewasili kutoka nchini Ujerumani tayari kwa kuanza majaribio mwezi ujao. Naibu Waziri Mhe. Atupele Mwakibete awataka watanzania kuyatunza.

Mabehewa haya ni kati ya 30 ambayo yalitumika na kufanyiwa maboresho nchini Ujerumani, imeelezwa kuwasili kwake ni kiashiria cha kuanza kwa safari za reli kati ya Dar hadi Morogoro.

Akipokea mabehewa hayo Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete amesema ameridhishwa na hali ya mabehewa hayo ambayo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya reli yameonekana nchini.

Naibu Waziri Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete amesema kinachosubiriwa sasa ni kuwasili kwa kichwa kitachovuta mabahewa hayo ambacho kinatarajiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu.

Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Ameeleza kuwa mabehewa hayo ambayo ni ya ghorofa, manne kati yake yana uwezo wa kubeba abiria 120 kila moja na mengine mawili yakibeba abiria 140 kila moja.

“Haya mabehewa yalinunuliwa yakiwa yametumika ila yamefanyiwa marekebisho kwa zaidi ya asilimia 80 na yamekuwa bora pengine sawa na mapya" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi

"Tunatarajia kuanza majaribio mara baada ya kichwa kuwasili mwezi ujao na hilo likikamilika tutaanza rasmi safari za kipande cha kwanza cha Dar- Moro" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Amina Lumuli amesema mabehewa mengine 24 yatawasili nchini Agosti huku kichwa cha pili cha umeme kinatarajiwa kuwasili Novemba.
 

Attachments

  • mabehewa-pic.jpg
    mabehewa-pic.jpg
    114.2 KB · Views: 16
  • WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.53.jpeg
    61.2 KB · Views: 15
  • WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.53(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.53(1).jpeg
    58.6 KB · Views: 15
  • FyG9J74acAUUCE-.jpg
    FyG9J74acAUUCE-.jpg
    33.8 KB · Views: 16
  • WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.54.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-09 at 17.41.54.jpeg
    52.6 KB · Views: 16
  • FyG9J7PaUAUjSpU.jpg
    FyG9J7PaUAUjSpU.jpg
    72.3 KB · Views: 24
  • FyG9J7ZaUAEfaLu.jpg
    FyG9J7ZaUAEfaLu.jpg
    58.9 KB · Views: 22
  • FyG9J7YaEAAjkgO.jpg
    FyG9J7YaEAAjkgO.jpg
    52.8 KB · Views: 19
Kila siku tunapewa kalenda.
Kuna jamaa humu alitupia ahadi za uongo za kuanza kazi SGR. Hii leo ni kama mara ya saba tunadanganywa
 
Dar Dom elfu 60
Sasa kulikuwa kuna sababu gani ya kununua mabehewa used, halafu na kuyafanyia maboreshwa kwa 80%!! Akili za Waafrika bhana!! Sasa si yatachakaa mapema kabla ya wakati wake!

Cha kushangaza kwenye magari ya serikali na bidhaa nyingine, sheria ya manunuzi inataka bidhaa iwe mpya!!

Anyway, mimi nasubiri hiyo treni ianze. Maana imewatesa sana watumishi wa umma enzi huo mradi wake ulipoanza.
Sasa kulikuwa kuna sababu gani ya kununua mabehewa used, halafu na kuyafanyia maboreshwa kwa 80%!! Akili za Waafrika bhana!! Sasa si yatachakaa mapema kabla ya wakati wake!

Cha kushangaza kwenye magari ya serikali na bidhaa nyingine, sheria ya manunuzi inataka bidhaa iwe mpya!!

Anyway, mimi nasubiri hiyo treni ianze. Maana imewatesa sana watumishi wa umma enzi huo mradi wake ulipoanza.
 
Ngonjela tushazizoea.huo ni mkakati wa uchaguzi.uchaguzi ukikaribia ndio wataaanza ili kutuhadaa wananchi.
 
Back
Top Bottom