Naibu Waziri Mwakibete: Lazima Tutafute Utafiti Wenye Tija Ili Wamiliki wa Meli Wasione Gharama Kuleta Meli Bahari ya Hindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945
"Katika Mkoa wa Tanga tumebarikiwa kuwa na Bandari ambayo ilianza kufanya kazi tangu miaka ya 1880 enzi za Utawala wa Mkoloni (Ujerumani) ikijulikana kama Marines Gent. Mwaka 1914 wakajenga geti la kwanza (Gati) ambapo Meli zinatua (Kusimama). Gati lilikuwa na urefu wa mita 221" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Mwaka 1954 lilijengwa Gati lenye urefu wa mita 229 na kukawa na jumla ya mita 450. Umbali wa kushusha mizigo kutoka Nangani mpaka Meli inaposimama ilikuwa na umbali wa kilomita 1.7, kwenye Nanga palikuwa na kina cha maji kilikuwa ni kifupi (Mita 3), Meli kubwa na ndogo zilishindwa kuja kwasababu ya tope" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Mita 450 zilizoanza kujengwa mwaka 1954 katika bandari ya Tanga zilikuwa hazileti ufanisi wala tija. Serikali ya CCM mwaka 2019 - 2020 kukawa na mradi mkubwa wa kuboresha bandari ya Tanga kuongeza kina cha Maji kutoka Meli zinaposhusha ndani ya Maji Kilomita 1.7 na kuongeza kina kwa mita 13 na kuongeza upana wa mita 73" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Mradi wa Bandari ya Tanga mwaka 2019-2020 uligharimu Shilingi Bilioni 172.3. Awamu ya pili ilikuwa ni kujenga magati yenye mita 450 ambayo yamekamilika kwa asilimia 99.85 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 226.8. Jumla ya miradi Miwili kwenye bandari ya Tanga zilizoletwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni Shilingi Bilioni 429.1" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Tanga ya zamani ni tofauti na Tanga ya sasa. Tanga ya zamani Meli kubwa zilikuwa haziwezi kufika. Sasa hivi ni zaidi ya Meli 7 zimeshaanza kutua katika bandari ya Tanga baada ya maboresho makubwa kufanyika. Ilani ya CCM 2020-2025 suala la kuboresha bandari, neno bandari limejitokeza zaidi ya mara 116" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Tunavyobadirisha na kuanza kuboresha na Kutafuta wanaoweza kuendesha vizuri bandari siyo jambo geni kwa kuwa tumeelekezwa na Ilani ya CCM 2020-2025. Ilani ya CCM ni Mkataba kati ya wananchi na Serikali iliyopo Madarakani kwenye ukurasa wa 80 mpaka 90 yenye kurasa 308" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Kumekuwa na maneno mengi kuwa bandari zote nchini zimeuzwa, Nataka niwahakikishie, Mimi Atupele Fred Mwakibete ambaye niliaminiwa na Mheshimiwa Rais nimsaidie kazi kama Naibu Waziri, niwatoe hofu na mashaka, Hakuna Bandari yoyote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyouzwa. Bandari ya Tanga tutaendesha Serikali wenyewe. Bandari zote kwenye Maziwa hazijaguswa kwa uwekezaji wa DP World" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"DP World ni miongoni mwa Makampuni makubwa Duniani, inamiliki Meli zisizopungua 400, Inafanya kazi Duniani zaidi ya nchi 30. Katika Bara la Afrika anafanya kazi kwenye nchi 6. Tanga tupo karibu na Kenya ambao wana bandari ya Mombasa na Ramu ambao ni washindani wetu" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Ili mizigo ije kwenye bandari zetu za Tanga na Dar es Salaam lazima tutafute ufanisi wenye tija na Wamiliki wa Meli wasione gharama kuleta Meli zao ndani ya Bahari ya Hindi kwa bandari zetu za Tanzania" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Ukienda Dar es Salaam, ukiangalia ng'ambo ya Bahari ya Hindi utakuta kuna Meli nyingi kama Meli 10, 15, 20 zinasubiri kushusha mzigo itie Nangani Dar es Salaam ila zinashindwa kushusha mizigo kwasababu Gati za Dar es Salaam ni chache. Sisi tuna Magati 12 tu katika bandari ya Dar es Salaam, Kenya Mombasa wana Magati 22" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Meli nyingi Dar es Salaam zinakuwa kwenye kina Kirefu kwasababu Magati yetu ni machache; Hatuna vifaa vya Teknolojia vya kushusha mizigo kwa wakati; Hatuna mifumo inayosomana ili iwe rahisi watu kulipa kodi na Meli ikifika inashusha mizigo kwa wakati mmoja. Kuna mfumo mmoja tunaita Electronic Single Windows System" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Meli inavyokaa Nangani kwa muda mrefu wanaanza kulipa gharama ya Meli. Meli moja kwa siku moja ni Dollars za Marekani 25,000 sawa ma Shilingi Milioni 58 kwa siku moja. Meli ikikaa siku 10 ni sawa na Shilingi Milioni 580. Anayelipa (Shipping Line) gharama yake itaenda kwa wenye mashehena, madhara yatakuja kwa wananchi wa kawaida kwa kupanda bei ya bidhaa zilizopo ndani ya Meli" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Serikali ya CCM tukaona umuhimu wa kutafuta mwekezaji mwingine ambaye muda wa kusubirisha Meli Nangani utakuwa mufupi na gharama zitakuwa ndogo" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

"Kazi kubwa ya mwekezaji wa bandari itakuwa ni Kuendeleza, Kuendesha na Kusimamia. Mwaka 2021-2022 bandari zote Tanzania tulikusanya Shilingi Bilioni 795.226 na matumizi yake ilikuwa ni Shilingi Bilioni 791.862. Zilibaki Shilingi Bilioni 3.364. Gharama zote zinaenda katika uendeshaji" - Mhe. Atupele Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
 
Back
Top Bottom