DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 8,586
- 17,696
Zifuatazo ni Failed Mission ya Majaribio au Kuanza Kwa Kutumika SGR..
Kipi Kifanyike..
Kipi Kifanyike..
- Februari 2019 - Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alisema safari ya kwanza ya SGR itaanza Novemba, 2019.
- Januari 2021 - Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alisema huduma za SGR zitaanza ndani ya mwaka 2021.
- Machi 2021 - Aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandishi Leonard Chamuriho alisema safari zitaanza rasmi Agosti, 2021.
- Aprili 2021 - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema safari za majaribio zitaanza Julai/Agosti 2021.
- Mei 2021 - Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari za majaribio zitaanza Agosti 2021.
- Septemba 2021- Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema safari zitaanza rasmi kati ya Disemba 2021 & Januari 2022
- Machi 2022 - Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC), Masanja Kadogosa amesema safari zitaanza rasmi Aprili 2022.
- Septemba 2022 - Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchakuzi, Atupele Mwakibete alisema safari zitaanza rasmi Februari 2023.
- Januari 2023- Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa alisema safari za majaribio zitaanza Februari 2023.
- Februari 2023- Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema safari za SGR zitaanza rasmi Mei 2023
- June 2023- Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa alisema safari za majaribio zitaanza Julai 2023.
- Disemba 2023- Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema safari zitaanza rasmi mwishoni mwa Januari
2024. - Disemba 2023- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo safari zianze kabla ya mwezi Julai 2024.