Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Wakati kukiwa na mitazamo mbalimbali juu ya Rais Samia Suluhu Hassan na utendaji wake kazi, Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete anasema imekuwa ni miaka mitatu ya kutengeneza utulivu wa nchi ambao umefanikisha kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali. Mzee kikwete anasema:
Hata wafanyabiashara sasa hivi wanafanya kazi zao kwa utulivu, mazingira yale yaliyopo ndani ya nchi kuna utulivu hili ni jambo kubwa. Mazingira hayo ndilo jambo linalochochea uchumi kukua.
Mazingira yetu ya leo hapa hayamfanyi mtu kufikiria kuhamisha mtaji wake, kuhamisha shughuli zake kwenda nchi nyingine. Haya ni mambo makubwa yanayopambanua Urais wa Samia Suluhu Hassan.
Huko nje watu wanataka kuwekeza wanaifikiria Tanzania, ameibeba ile shughuli vizuri. Halafu kingine ni mtulivu she is the President that dont panic.