Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

[h=2][/h]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) anatarajiwa kuwasili mjini Kuala Lumpur, Malaysia kesho, Jumapili, Juni 19, 2011, asubuhi, kuungana na viongozi wenzake kutoka nchi mbali mbali katika mkutano wa mwaka huu wa Smart Patrnership Dialogue.
Mkutano huo ambao umekuwa unafanyika kila mwaka kwa miaka 16 sasa tokea mwaka 1995 unatokana na maamuzi ya wakuu wa nchi za Jumuia ya Madola uliofanyika Cyprus mwaka 1993 na kuzinduliwa rasmi katika mkutano wa wakuu hao uliofanyika Auckland, New Zealand mwaka 1995.
Mkutano huo huzungumzia masuala mbali mbali ya maendeleo na hasa umuhimu wa uhusiano mzuri kati ya Serikali, sekta ya umma na sekta binafsi katika kuleta maendeleo.
Mkutano wa mwaka huu umepangwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Putrajaya (PICC) kilichoko katika mji mpya wa shughuli za Serikali ya Malaysia ulioko Patrajaya, nje kidogo ya mji wa asili wa
Kuala Lumpur.

Nchi ya Malaysia imewaalika wakuu 25 wa nchi mbali mbali duniani kushiriki katika mkutano huo hata
kama haitarajiwi kuwa wote watashirki mkutano huo. Kutoka Afrika wamealikwa Rais Kikwete, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Omar El Bashir wa Sudan na Waziri Mkuu wa
Lesotho.

Rais Kikwete atawasili
Malaysia kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu akitokea Shelisheli ambako usiku wa leo, Jumamosi, Juni 18, 2011, atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Taifa ya Shelisheli.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo ambako atazungumza kwenye kikao cha ufunguzi na pia kwenye kikao kitakachozungumzia namna mbadala na za ubunifu zaidi za kupata fedha kwa ajili ya maendeleo, Rais Kikwete pia atakuwa na shughuli nyingine muhimu za kikazi.
Miongoni mwa shughuli hizo ni Rais Kikwete kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Sri Mohammed Tun Abdul Razak, kukutana kwa mazungumzo na aliyekuwa waziri mkuu wa
Malaysia, Mheshimiwa Tun Dkt. Mahathir Mohamad, Rais wa Heshima wa Taasisi ya Uongozi ya Perdana Leadership Foundation.

Rais Kikwete pia atakutana na kula chakula cha usiku na wenyeviti, marais na watendaji wakuu wa makampuni makubwa ya
Malaysia wakiongozwa na Mheshimiwa Mahathir Mohamed.


TANZANIA: OPEN LETTER TO PRESIDENT KIKWETE « Jaluo
 
Cha kusikitisha ni kuwa ameunganisha saafairi katika nchi nne kwa kipindi cha wiki mbili bila kutulia nyumbani licha ya matatizo kibao tuliyonayo. tarehe 10-13 alikuwa nchini Afrika ya Kusini na alirudi nyumbani na kuunganisha kwenda Uswizi. alitoka uswizi akaruka Tanzania akaenda shelisheli na kutoka shelisheli akaruka tena anga la Tanzania na kwenda malyasia. huyu jamaa ana addiction ya safari hasa.
 
Si dhani kama kuna umuhimu wa kuwa na ikulu ya aridhini kwa sasa hivi. Na kilicho sahaulika kwenye bajeti ya mwaka huu ni fedha za kuhamishia ikulu kwenye ndege, na hakukuwa na haja ya kutenga bilioni 10 kupaka langi ikulu ilihali mkuu wa nchi muda mwingi anakua angani.
- hata katibu mkuu kiongozi na wafanya kazi wengine wa ikulu inabidi wahamie hukohuko angani hii itapendeza sana
 
kula maisha, piga suit za kifaransa, kupanda bembea etc.

Haya ndio madhara ya kuwa na rais mwenye ndoto mtaa...a president with street dreams.
Ndoto zake zilikua na kupendeza kwa designer suits and shoes...kuendeshwa kwenye BMW...kusafiri kila kona ya dunia n.k.

Hakuwa ameota namna gani atasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo la TZ!
 
Huyu Jk Jamani ni Rais wangu lakini tabia yake ya kuzurura nje inaboa sana. Nchi inateketea kwa matatizo lukuki nja, mfumko wa kutisha wa bei, migomo na migogoro kila kukicha, Ufisadi, mipasho kila kukicha katika serikali yake, magonjwa na huduma mbovu za afya, n.k n.k n.k.

Sasa sijui anatukomoa au vipi kwani nahisi hata matatizo haya hayaoni jamani? Rais wa nchi ni kama baba nyumbani ambaye anatakiwa kusimamia kwa karibu sana maswala muhimu yanayoikabili nyumba yake. Huyu mzee anajitetea kuomba msaada mpaka lini jamani haoni aibu???? Tukikazana wenyewe kwani hatuwezi jamani mpaka atufanye matonya wa kimataifa kiasi hiki??? Mtu anapenda kuomba sana ana matatizo haiwezekani kila kukicha ni bakuli la mchango tu unapitisha kwa mataifa mengine aibu gani hii jamani. Alikuwa South juzi, Then Geneva, Malysia, akirudi atahudhuria misiba miwili mitatu au sherehe fulani amemaliza mwezi natoka tena. Jamani inaumaaaaaaaaaaa sana wadau
 
ina maana hakujua lengo la kuwekwa waziri wa mambo ya nchi za nje kwa miaka 10 na MKAPA?tulitegemea ameshajifunza kwa uwaziri ule kumbe hakuna kitu
 
Mbora angekua ana safiri sana na matunda ya hizo safari tungekua tuna ziona. Tunaambiwa kila siku anaenda kuomba misaada ila hali inazidi kuwa mbaya zaidi siku hadi siku.
 
tumtishie kumfanyia mapinduzi ataogopa atajua akienda zurura nyuma watu watachukua nchi
 
Mloge tena ugonjwa wa stroke au miguu,atakaa tu kwani alivyo hatapenda kuonekana na wheelchair,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom