Safari za Kikwete zazaa matunda...

Zomba,

..utaratibu wa waalimu toka USA ulikuwepo tangu zamani.

..tulitakiwa kuboresha mafao na mazingira ya ufundishaji ya waalimu wetu.

..mnajisifia kuleta waalimu 47 wakati kuna maelfu ya waalimu wazalendo waliokata tamaa.

Naona mnakurupuka, kwa kuwa tu yanatajwa mafanikio ya Kikwete ambayo hamuyapendi, waliokuwa wanakuja wengi wao wanakuja kufundisha Kiingereza, hawa wameletwa rasmi kufundisha SCIENCE kama alivyo ahidi Kikwete kuliboresha hilo somo.

Vipi kanuni za IMO zimekuingia au bado?
 
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.

Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,

Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.

Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.

peace corps hawa wanajitolea ili baadae waweze pata kazi kwao au kusoma kirahisi hawa hata jk asingewaomba wamekuwa wakija huku kwetu miaka yote kutimiza adhima yao ya kujenga CV ya kuombea kazi au kusoma huko kwao.
 
Zomba usipende kusifia kila kitu anacho fanya JK Tafakali kwanza Isije siku moja ukasikia hawa walimu ni watafiti wa madini au wanazalisha mikanda ya Ngono na Dada zetu maana tumeshuhudia wazungu wengi walikuja kama viongozi wa dini lakini mwisho wa siku wamefanya kinyume na walicho ijia,

Mbona mikanda ya ngono inazalishwa kila siku? na haingoji wazungu, hujui hilo? washatuletea video mpaka kwenye simu, hayo mambo yamezagaa sana.

Madini watu wanachimba wewe unaongelea kutafiti> umelala.

Hawa ni Waalimu wa sayansi wakifanya mengine itakuwa wamevunja miadi, na hapo watalaumiwa. Kwa sasa tunawakaribisha watupe elimu inayotupiga chenga.
 
peace corps hawa wanajitolea ili baadae waweze pata kazi kwao au kusoma kirahisi hawa hata jk asingewaomba wamekuwa wakija huku kwetu miaka yote kutimiza adhima yao ya kujenga CV ya kuombea kazi au kusoma huko kwao.

Hapana, hawa ni waalimu wa sayansi waliokwisha staafu na wameombwa kuja kusaidia kutupa ujuzi wao hapa.
 
Hao waalimu wamekuja kufindisha sayansi, somo ambalo tuko nyuma kulinganisha na nchi zingine. Na hizi ni jitihada za Kikwete kuimarisha hilo somo alizozitoa bungeni Dodoma, pitia juu kuna link.

Soma vizuri swali langu zomba, waalim toka Marekani wanakuja kwa sababu hatuna waalim (wa sayansi) au hatulipi waalim watu vizuri na hivyo watu wanaikimbia hiyo taaluma? Be honest!
 
Ubora wa mgogoni uliopo sasa hauhitaji mzungu. Nyerere alikuwa na mzungu anamfundisha kazi miaka yote pale Ikulu, alileta ubora upi? hata shule zilimshinda kujenga. Wakati wake wote shule za sekondari hazizidi 100 mpya. Kikwete ni shule zaidi ya 4000 kwa miaka 7 tu. Upo hapo ulipo?

katumia macho ya aina gani kuwatazama waalimu wa kitanzania ya kuwa hawawezi kufundisha masomo ya sayansi, halafu sisi tusiwe na macho ya kuona kuwa naye ha-fit kukaa pale magogoni?
Wazungu tulishawaondoa kitambo, ametumia mwongozo wa sera ipi kutuletea wapelelezi wa kizungu?
 
Naona mnakurupuka, kwa kuwa tu yanatajwa mafanikio ya Kikwete ambayo hamuyapendi, waliokuwa wanakuja wengi wao wanakuja kufundisha Kiingereza, hawa wameletwa rasmi kufundisha SCIENCE kama alivyo ahidi Kikwete kuliboresha hilo somo.

Vipi kanuni za IMO zimekuingia au bado?

Zomba,

..walionifundisha mimi walikuwa waalimu wa masomo ya Science na hisabati.

..tena kuna kwa miaka tofauti walikuwepo wanatokea Australia, Ujerumani, India, Marekani, na Uingereza.

..waalimu 47 wont make much difference kama waalimu wenzao wazalendo wataendelea kukatishwa tamaa kama inavyotokea sasa hivi.
 
Waalimu wazalendo hawakatishwi tamaa, hakuna wakati migogoro yao iliposhughulikiwa kama huu wa Kikwete, hakuna wakati mishahara imeongezeka kama huu wa Kikwete, hakuna wakati wanaosikilizwa na kuthaminiwa kama huu wa Kikwete, hakuna wakati vyuo vya Ualimu na wanaosomea Uwalim wamekuwa wengi kama wakati huu wa Kikwete. Na waliambiwa wakae mezani waongee, wanajidai kugoma.

Hao wanafata wajinga wachache wanaowadanganya, wasikurupuke.
 
..there r go.

..kama mishahara haikidhi mahitaji, na haihimili mfumuko wa bei, basi malalamiko ya watumishi/waalimu yataendelea kuwepo. serikali nayo itaendelea kushangaa kwamba wanapandisha mishahara lakini watumishi hawaridhiki au wanakosa "shukurani."

..mimi nadhani mfumo mzima wa elimu ya Tanzania unakatisha tamaa. inatia aibu kuona watoto wanasoma kwenye madarasa yaliyoezekwa kwa makuti. Mind you, Tanzania ni kati ya nchi 5 wachimbaji wakubwa wa dhahabu ktk bara la Afrika.
 
Unless wametoka MIT ,na vyuo vingine vya calibre yake,hawa jamaa wanaweza kuwa shallow sana naaibu kwa taifa,pengine US waamue tuletea FBI na CIA kuja checki vizuri ni kwa kiasi gani tunalea maadui wao uatamaduni wao,na jinsi watakavyokuj piga kambi hapa.Hawa jamaa mbona huwa wanaomba wenyewe kuja tena amombi huenda kwa taasisi,shule, kanisa, NGO husika?

Sijui kama presidaa anajua kuwa nchi nzima kumejaa wazungu wanaokujwa tafuta uzoefu, ili wakirudi kwao wate kazi, huku wengine wakija enjoy bia za bwereree na safari za kutosha +kuonja mitulinga ya kibongo.Halfu wakifuta computers na kufundisha watu kuchat wanarudi kwa kupokea sifa kuwa wamekuja wapa watu elimu ya computers ambayo haijafika kabisa kwa watu weusi.
 
Mwaka huu wakati wa Kikwete kwa mara ya kwanza tunaona kampuni za uchimbaji dhahabu zikianza kulipa kodi, au hujui hilo?

Unafikiri wawekezaji wajinga? waje, wawekeze mali zao, mitambo na muhimu zaidi ni ujuzi wao halafu wakuwachie wewe kila kitu? NO. Kwanza wanahakikisha wanarudisha wanachowekeza, halafu wanapata faida halafu ndio mgawane faida sio kabla. Kama hutaki, kachimbe na kucha.

Mishahara kama haiwatoshi waende wakafanye nchi zitakazowapa mishahara ya kuwatosha au wasubiri tunaenda kwa kuongezana hivyo hivyo kidogo kidogo. Huwezi kulazimisha kitu hakiwezekani kwa mara moja.

Wameshaambiwa kaeni, msiwe na shaka tutaongezana kidogo kidogo na kila muda unavyokwenda tutaongezana, hutaki wacha. Wewe ukisema ya nini wenzako wanauliza ntaipata lini.
 
Hivi tuna shule ngapi TZ za sekondari?
NWY, wakija waje na vitabu, madaftari, vifaa vya maabara, bila ya kusahau ubao na chaki.
Ah! Wasisahau mievuli kwa kipindi cha mvua, madarasa yanavuja.
 
Wameshakuja na wapo Tanzania kwa sasa na hiyo ni first batch na wengine wako njiani.
 
Unless wametoka MIT ,na vyuo vingine vya calibre yake,hawa jamaa wanaweza kuwa shallow sana naaibu kwa taifa,pengine US waamue tuletea FBI na CIA kuja checki vizuri ni kwa kiasi gani tunalea maadui wao uatamaduni wao,na jinsi watakavyokuj piga kambi hapa.Hawa jamaa mbona huwa wanaomba wenyewe kuja tena amombi huenda kwa taasisi,shule, kanisa, NGO husika?

Sijui kama presidaa anajua kuwa nchi nzima kumejaa wazungu wanaokujwa tafuta uzoefu, ili wakirudi kwao wate kazi, huku wengine wakija enjoy bia za bwereree na safari za kutosha +kuonja mitulinga ya kibongo.Halfu wakifuta computers na kufundisha watu kuchat wanarudi kwa kupokea sifa kuwa wamekuja wapa watu elimu ya computers ambayo haijafika kabisa kwa watu weusi.

Hayo yote unayosema ni sawa, lakini hawa waliombwa mahsusi kuja kusaidia kusomesha sayansi.

Labda uniambie wanakuja kutazama (scout) vijana wanaofaa kuwa wana sayansi wazuri baadae ili wawahi kabisa kwani wenzetu wanafikiri mbali sana, unafikiri scholarship wanatupa huwa za bure? wakita scholarship mia wanaorudi huku ni wale ambao hawakufanya vizuri sana wanaofanya vizuri huwa wanawahiwa hukohuko kwa ma offer ya makampuni na taasisi za huko. Uliyajuwa hayo?
 
Waalimu wazalendo hawakatishwi tamaa, hakuna wakati migogoro yao iliposhughulikiwa kama huu wa Kikwete, hakuna wakati mishahara imeongezeka kama huu wa Kikwete, hakuna wakati wanaosikilizwa na kuthaminiwa kama huu wa Kikwete, hakuna wakati vyuo vya Ualimu na wanaosomea Uwalim wamekuwa wengi kama wakati huu wa Kikwete. Na waliambiwa wakae mezani waongee, wanajidai kugoma.

Hao wanafata wajinga wachache wanaowadanganya, wasikurupuke.
Itoshe tu kukita mpumbavu kwa ghalama yoyote!
 
Gahrama ya UVasco Nusu ya bajeti ya serikali,

Matokeo walimu 47 wa kujitolea toka Marekani?

Haya wa Uk wako wapi?

Akili ndogo inaongoza akili kubwa.

Kuna watu hapa jamvini,
hawawezi kutofautisha,
kati ya hekima na kiwango cha fedha mfukoni.
waTanzania kadhaa wanadhani Fedha nyingi ni mbadala wa hekima.
 
Mwaka huu wakati wa Kikwete kwa mara ya kwanza tunaona kampuni za uchimbaji dhahabu zikianza kulipa kodi, au hujui hilo?

Unafikiri wawekezaji wajinga? waje, wawekeze mali zao, mitambo na muhimu zaidi ni ujuzi wao halafu wakuwachie wewe kila kitu? NO. Kwanza wanahakikisha wanarudisha wanachowekeza, halafu wanapata faida halafu ndio mgawane faida sio kabla. Kama hutaki, kachimbe na kucha.

Mishahara kama haiwatoshi waende wakafanye nchi zitakazowapa mishahara ya kuwatosha au wasubiri tunaenda kwa kuongezana hivyo hivyo kidogo kidogo. Huwezi kulazimisha kitu hakiwezekani kwa mara moja.

Wameshaambiwa kaeni, msiwe na shaka tutaongezana kidogo kidogo na kila muda unavyokwenda tutaongezana, hutaki wacha. Wewe ukisema ya nini wenzako wanauliza ntaipata lini.

Zomba,

..kuhusu migodi ya dhahabu, tatizo ni kila Raisi na Waziri anataka asaini mkataba wa kuchimba dhahabu.

..tulitakiwa tuanze na migodi isiyozidi 3 kama maandalizi ya kujenga uwezo na kupata mikataba mizuri zaidi ktk migodi mingine.

..kuhusu elimu, pamoja na mafao ya waalimu, I hope ulichoandika does not reflect the attitude ya wakubwa huko serikalini na ktk CCM kuhusu sekta ya elimu.
 
Back
Top Bottom