Matunda ya safari za Kikwete nje ya nchi

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,031
1,603
Mwenyekiti Mwenza Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, ameibuka na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa akisafiri zaidi na kutumia muda mwingi akiwa nje ya nchi kuliko nchini katika kipindi chake cha takriban miaka 10.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NLD na Chama cha Wananchi (CUF).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mbatia alidai kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10 chenye wastani wa siku 3,650, Rais Kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya Tanzania kwa wastani wa siku tano katika kila safari, hivyo jumla kuwa siku 2,045. Alisema siku hizo ni sawa na asilimia 56 ya muda wake wote akiwa madarakani hadi kufikia sasa.

Akifafanua zaidi, Mbatia alisema wastani wa gharama ambazo taifa imezibeba kutokana na safari hizo ni Sh. trilioni 4.5.

Alisema kiasi hicho cha fedha alichotumia Rais katika safari zake kingetosha kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kujenga hospitali na pia vyuo vya ufundi.

Alitaja idadi ya vyuo vya ufundi vinavyoweza kujengwa kuwa ni 200, vyuo vikuu 80 na pia kiasi kingine kingeweza kujenga hospitali za rufaa.

Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya idadi ya watu na wapigakura kilichotolewa Machi, 2015 kwa ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, Tanzania itakuwa na watu 48,522,228 kufikia mwezi ujao. Hivyo, kwa kiasi alichokitaja Mbatia kuwa kimetumika kwa safari za nje za Rais Kikwete, maana yake ni kuwa kila Mtanzania angeweza kupata wastani wa Sh. 92,741 ikiwa zingegawiwa kwa kila mmoja. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti ya NBS ya Machi mwaka huu, wastani wa pato la kila Mtanzania kwa siku ni Sh. 4,724.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu kuhusu madai hayo ya Mbatia, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, hakupokea na badala yake akajibu kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) 'I'm busy and i can't take your phone'. Ujumbe mwingine aliojibu kupitia simu yake ulisema 'siwezi kujibu naendesha kikao'.

MBATIA AKOSOA ZAIDI
Katika mkutano wake, Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mgombea ubunge katika Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, alisema safari nyingi za Rais hazikuwa za lazima yeye kwenda na kwamba angeweza kumtuma Waziri wa Mambo ya Nje ama Balozi wa Tanzania katika nchi husika.

Alisema nchi maskini kama Tanzania kutumia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari za Rais hakuwezi kulisaidia taifa badala yake kunazidi kulirudisha nyuma.

MAPATO YA SERIKALI
Katika hatua nyingine, Mbatia alizungumzia uwezekano wa kutolewa kwa elimu bure na serikali kwa kudai kuwa vipo vyanzo vingi vya fedha vinavyowezesha jambo hilo.

Alitolea mfano mapato yatokanayo na uvuvi, kodi za nyumba, ardhi na maeneo mengine aliyodai yanafikia Sh. trilioni 23.55 na kwamba gharam za elimu ni Sh. trilioni 1.55 kiasi ambacho ni kidogo.

KODI YA WAFANYAKAZI

Mbatia alitoa mfano nchi ya Kenya wafanyakazi wanakatwa kodi ya asilimi sita katika mishahara, Rwanda asilimia tano, Burundi asilimia 10.3, Uganda asilimia 11 na Tanzania kodi inayokatwa kwa wafanyakazi wa mishahara ya juu ni asilimia 18.

Alisema Ukawa wakiingia madarakani watapunguza kodi kwa wafanyakazi wa Tanzania hadi kufikia asilimia tisa na kwamba kiasi kingine cha mapato kitapatikana katika sekta zingine zikiwamo za utalii na ardhi.

Akizungumza katika mkutano huo, mshauri wa masuala ya ufundi wa Ukawa, Prof. Mwesiga Baregu, alisema Rais Kikwete amejulikana kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kutokana na kutumia muda mwingi kwa safari za nje.

Alisema ni aibu kutolewa visingizio vyovyote kuhusu safari hizo vikiwamo vya kuwaambia Watanzania kwamba Rais Kikwete alikuwa anakwenda nje mara nyingi kwa ajili ya kuomba misaada.

Alisema Rais angeweza kubakia nchini na kutumia rasilimali chache zilizopo kuboresha maisha ya Watanzania badala ya kutumia kidogo kilichopo kwa ajili ya safari za kwenda kuomba.

Aidha, Mbatia alitoa tuhuma kwa kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa ambazo zinaongozwa na wakuu wa wilaya na mikoa akidai kwamba zinafanya vikao vya siri ili kuhakikisha CCM inashinda hata kwa kutumia mbinu chafu.

"Kila kinachopangwa gizani lazima kitajulikana katika nuru na sisi tumebaini vikao mbalimbali kama hivyo ambavyo vimefanyika katika hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha na vingine jijini Dar es Salaam," alisema.

Kuhusu amani ya Tanzania, Mbatia alisema vyama vyote vya siasa vikutane na kufanya midahalo kwani amani ikitoweka kila mmoja ataumia.

Alirudia kauli ya Ukawa kwamba elimu ya Tanzania kutolewa bure mpaka chuo kikuu inawezekana, huku akisema sekta ya utalii, ardhi na kodi za majengo zinatosha kufanya kazi hiyo na kila Mtanzania akanufaika.

Aidha, Mbatia alikitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuachana na siasa za kuhubiri ukabila na ukanda, badala yake wawaeleze wananchi katika kipindi cha miaka 10 wamewafanya nini na kwa sasa wakiwachagua tena watafanya nini.

Alikitaka chama hicho kizungumzie matatizo ya wananchi badala ya kujikita kumsema mgombea wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

CHANZO: NIPASHE
 
Chanzo: Gazeti NIPASHE

CHANZO:NIPASHE

Yaan mim mtu ambaye atatoa ahad ya single digit kwenye salary ndo ntampa kura yangu..ile kod inauma hatari et PAYE
 
Good analysis,kuna mikutano Kikwete hua anaenda mpaka unashangaa kweli anaubongo kwani nyingine ni kama hazina tija kwa taifa hata kidogo.Saa nyingine unajiuliza wasaidizi wake wanafanya nini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom