Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

Karibu sana

Kuna guests nzuri Sunshine na nyingine jirani na Torokauje bei 20000Tsh safi kabisa .Kuku choma Torokauje watam balaa.ITM 1 km from mjini bank NMB na CRDB ..Mpesa ulizia kwa Maziku hapo pia kuna Min supermarket
Vi grosari vya kutosha utakutana na Waarabu wa Dubai na WaEthiopia(wairaqw)...ni kamji katulivu hakuna Kufuatana fuatana bia 24hrs ....wenyeji Wachangamfu sana....pombe kali jamii ya Viroba kwa wingi usishangae kukuta warembo wakipiga hayo makitu...
Mayai ya kienyeji sh 300 moko...kuku wa kienyeji kibao bei nafuu kabisa...mahindi ya kuchoma maharage mabichi msimu mzima.....karoti bora barani Afrika kutoka Tumati

Nenda Mkuu hutajutia.....kuna mrembo anaittwa Pasikii ana kigrosari mtaa wa Mchagaa mchoma nyama maarufu....ukimwona mpe salamu
Ukifika huko usikose kutembelea mnada wa DIRIMU
Pasikii
 
Wakuu habari za mapumziko ya mwisho wa juma? Na kwaresima na Ramadhan zenu natumai zinakwenda swadakta.

Kwa uweza wa Mungu kesho nitakuwa safarini kuelekea Dongobesh wilayani Mbulu. Kwa yeyote mwenye uzoefu na mahali hapo anaweza shea humu mazuri na mabaya ya hapo.

Nitakuwa hapo kwa mwezi mmoja kikazi. Nawasilisha na ahsanteni sana.
Kama wewe ni mpenzi wa masikio ya mbuzi na marefu andika umeumia, wanayafyeka!
 
Pitia njia ya Katesh, Mogitu mpaka Sechet (mashamba ya ngano) halafu uende Dongobesh. Madunga, Mang'ola, Dareda Mission, Basodesh, Mbulu, Karatu ni maeneo ya karibu. Unaweza kupitia pia Magugu-Mbuyu wa Mjerumani, Ziwa Manyara-Ukingo, mlima Magara mpaka Mbulu, Basodesh then Dongobesh. Unaweza kupitia Makuyuni Mto wa Mbu, Rotia, Karatu, Mbulu, Basodesh, Madunga then Dongobesh.

Karatu pia ipo karibu sana kwa bata za kiaina.

Maeneo yangu origin pendwa hayo ingawa kwa sasa napambana kimaisha katika mitaa ya Skid Row karibu na West Holiwoody (kambi popote).

Halafu usisahau kutembelea mashamba ya ngano ya Mulbadaw, Murijanda, Gidagamowd, Gawali,Basuto nk.








Sent from my CPH2127 using JamiiForums mobile app
Dah....umenikumbusha mbali sana ..MULBADAW ... nlienda mwaka wa 2000 .... sikupita tena ile njia cjui Leo pakoje
 
Chukua koti kwa sababu ni baridi.
Kama unatoka mbali na utafika babati jioni nashauri ulale babati asubuhi panda gari za kwenda huko zamani kama 2014 hivi kulikua na basi linaitwa manday sijui kama bado lipo
-Jiandae kupita milimani
-Jaindae kusalimiwa kiirak kila upitapo kwa sababu wanajua kila mtu ni muirak
-kua makini na mabinti manake wakiona mgeni watakuchekea lengo ni pesa zako
-ukiwa kiboeo dinda utarudi na kaswende na kisonono kwa mkeo


Kila la heri mkuu
Baridi ni kali huko jo inatandika
 
Hali ya hewa nzuri, kuna kaubaridi kidogo, kama umetoka sehemu ya joto andaa nguo nzito kidogo

Kuna matope mvua ikinyesha

Kimbulu ndio lugha kuu hata hospitali ukifika au masokoni, unaweza ukawa discussion wakidiscus kwa kimbulu

Wanapenda sana kusoma ,hasa biology na chemistry

Kwakipindi hiki asilimia kubwa watu wapo mashambani , wanalima sana mahindi na maharage,

Pale kwa upande wa siasa HATA WATOTO NA WANAWAKE wanafuatilia sana siasa ukifika kutana na mzee yeyote piga nae story za siasa utajua kweli kuna watu wanajua mambo

Muda wote hata mchana wanaume wanavaa shuka, huo ni mtoko kabisa, pia mara nyingi huvaa bukta zile za shule ya msingi zikiwa na viraka( SIO UMASIKINI) ila ni tamaduni ya jamii hiyo. Tena hivyo viraka vinashonwa na uzi kwakutumia mkono na vinabandikwa kwa nje ( INGAWA SIO WOTE WAPO HIVYO) Na huenda wakawa wanabadilika kutokana na majira

Nguruwe zinafugwa kwa wingi mno

Sio wapenda usafi. Kula yao ,vaa yao, sio watu wakujipenda sana

Miswaki mara nyingi huwa niya miti(SIO KWAMBA MADUKANI HAKUNA ILA NI MAZOEA) ingawa sio wote

Rangi ya udongo ni udongo mwekundu.

Usafiri upo ila mtapangwa kama magunia ya mchele, kama kuna watu wanajua kupanga watu kama viroba vya mizigo utawakuta huko, labda kama unausafiri wako binafsi

Kila mahali utasikia neno SAITA,SAYUU,BARAGAHE,DERO, SHIDIKAH kariri hayo maneno ni comon kwa dongobesh

Ahsante

Shidi idero[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom