Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

Hali ya hewa nzuri, kuna kaubaridi kidogo, kama umetoka sehemu ya joto andaa nguo nzito kidogo

Kuna matope mvua ikinyesha

Kimbulu ndio lugha kuu hata hospitali ukifika au masokoni, unaweza ukawa discussion wakidiscus kwa kimbulu

Wanapenda sana kusoma ,hasa biology na chemistry

Kwakipindi hiki asilimia kubwa watu wapo mashambani , wanalima sana mahindi na maharage,

Pale kwa upande wa siasa HATA WATOTO NA WANAWAKE wanafuatilia sana siasa ukifika kutana na mzee yeyote piga nae story za siasa utajua kweli kuna watu wanajua mambo

Muda wote hata mchana wanaume wanavaa shuka, huo ni mtoko kabisa, pia mara nyingi huvaa bukta zile za shule ya msingi zikiwa na viraka( SIO UMASIKINI) ila ni tamaduni ya jamii hiyo. Tena hivyo viraka vinashonwa na uzi kwakutumia mkono na vinabandikwa kwa nje ( INGAWA SIO WOTE WAPO HIVYO) Na huenda wakawa wanabadilika kutokana na majira

Nguruwe zinafugwa kwa wingi mno

Sio wapenda usafi. Kula yao ,vaa yao, sio watu wakujipenda sana

Miswaki mara nyingi huwa niya miti(SIO KWAMBA MADUKANI HAKUNA ILA NI MAZOEA) ingawa sio wote

Rangi ya udongo ni udongo mwekundu.

Usafiri upo ila mtapangwa kama magunia ya mchele, kama kuna watu wanajua kupanga watu kama viroba vya mizigo utawakuta huko, labda kama unausafiri wako binafsi

Kila mahali utasikia neno SAITA,SAYUU,BARAGAHE,DERO, SHIDIKAH kariri hayo maneno ni comon kwa dongobesh

Ahsante
Wow so amazing umetisha mwamba 🙏🙏🙏🙏
 
Habari za jioni wakuu?
Nimefika salama Babati kwa usafiri bora kabisa wa shabiby line. Nitalala hapa leo. Nimewasoma vya kutosha sasa wacha nikajionee mwenyewe.
Thnx members
Hiyo shabibi ofisi zao zipo upande wa kulia hapo kama unaenda Arusha,Karibu sana,misosi mizuri ipo hapo ofisi za shabibi kwa chuma,wanajua kuchoma nyama usipime
 
Hakika mkuu unawajua hao watu kipindi cha mbaazi imefunga ni uzinzi kwa kwenda mbele, mabomba ya maji ni ya ku pump , nguruwe wanachungwa kama mbuzi, kipindi cha mahindi mabichi ni mwendo wa mahindi ya kuchemsha , ukikuta mtu kajisaidia shamban choo chake ni mahindi matupu, watoto wadogo wanavalishwa mashati marefu bila bukta , kila boma limefuga mbwa uchwara, kuna pombe ya asili ya mtama inaitwa mangure, usafiri ni cruser na one 10 , kipnd cha ukame vumbi jekundu utalinywa , ukiomba utamu kwa watoto wa kimbulu utasikia daaah ww chukua tu ni sambi sako mwenyewe , mtu wa kuja wanakuita omooo, ata kama una umri mdgo utasalimiwa shkamoo na mtu wa miaka 60 cha msingi uwe umependeza tu , Watu wa huko ni wakarimu mno ukiishi nao vizuri mahindi na vyakula vingne utavipata bure kabsa .
Aiseee 🤣🤣🤣🤣🤣 kama script
 
Sijajua kwa sasa ila 2015 lami ilikua inaishia babati kwingine vumbi tu
Ukipita njia ya mbuyu wa mjerumani kuelekea mbulu kule milimani kuna zege wameweka kama lami sehemu chache na wakati huo mbulu lami ilikua kdg tu tena kama msalaba katikati ya mji
Barabara ya kupita katesh, hydom,kutokea babati kwenda mpaka singida ni lami...ndio gari za kutokea moshi, tanga, arusha, manyara kwenda mwanza, zinapitia hapo
 
Tupeni na fursa za biashara na sio stories za dudu tu ..vp fursa za huko zikoje kwa wageni ambao tunaweza kuja na kuwekeza au kuleta Mali za misumu
Huko kuna umaskini tu mkubwa hakuna hela huko, wanalima mazao madogo madogo tu ya chakula, hata alizeti imewagomea....hali ni mbaya tu huko, tofauti na merelani huko machimboni
 
Hapa babati kwa kabila nakula kuku kienyeji choma kwa buku 8 tu. Mkoani kutamu sana
20230326_185225.jpg
 
Back
Top Bottom