Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

Safari ya Dongobesh Wilayani Mbulu

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,272
Reaction score
1,923
Wakuu habari za mapumziko ya mwisho wa juma? Na kwaresima na Ramadhan zenu natumai zinakwenda swadakta.

Kwa uweza wa Mungu kesho nitakuwa safarini kuelekea Dongobesh wilayani Mbulu. Kwa yeyote mwenye uzoefu na mahali hapo anaweza shea humu mazuri na mabaya ya hapo.

Nitakuwa hapo kwa mwezi mmoja kikazi. Nawasilisha na ahsanteni sana.
 
Wakuu habari za mapumziko ya mwisho wa juma? Na kwaresima na Ramadhan zenu natumai zinakwenda swadakta.
Kwa uweza wa Mungu kesho nitakuwa safarini kuelekea Dongobesh wilayani Mbulu.
Kwa yeyote mwenye uzoefu na mahali hapo anaweza shea humu mazuri na mabaya ya hapo. Nitakuwa hapo kwa mwezi mmoja kikazi.
Nawasilisha na ahsanteni sana.
Mweee, nilitoka huko mwaka 1998, enzi hizo no lami, no umeme
 
Wakuu habari za mapumziko ya mwisho wa juma? Na kwaresima na Ramadhan zenu natumai zinakwenda swadakta.
Kwa uweza wa Mungu kesho nitakuwa safarini kuelekea Dongobesh wilayani Mbulu.
Kwa yeyote mwenye uzoefu na mahali hapo anaweza shea humu mazuri na mabaya ya hapo. Nitakuwa hapo kwa mwezi mmoja kikazi.
Nawasilisha na ahsanteni sana.
Unatokea wapi kwenda huko? Naomba ufike Dongobesh sec uwasalimie waambie NGUVU amewamisi sana bila kusahau picha za mjini kati hapo uturushie humu
 
Hali ya hewa nzuri, kuna kaubaridi kidogo, kama umetoka sehemu ya joto andaa nguo nzito kidogo

Kuna matope mvua ikinyesha

Kimbulu ndio lugha kuu hata hospitali ukifika au masokoni, unaweza ukawa discussion wakidiscus kwa kimbulu

Wanapenda sana kusoma ,hasa biology na chemistry

Kwakipindi hiki asilimia kubwa watu wapo mashambani , wanalima sana mahindi na maharage,

Pale kwa upande wa siasa HATA WATOTO NA WANAWAKE wanafuatilia sana siasa ukifika kutana na mzee yeyote piga nae story za siasa utajua kweli kuna watu wanajua mambo

Muda wote hata mchana wanaume wanavaa shuka, huo ni mtoko kabisa, pia mara nyingi huvaa bukta zile za shule ya msingi zikiwa na viraka( SIO UMASIKINI) ila ni tamaduni ya jamii hiyo. Tena hivyo viraka vinashonwa na uzi kwakutumia mkono na vinabandikwa kwa nje ( INGAWA SIO WOTE WAPO HIVYO) Na huenda wakawa wanabadilika kutokana na majira

Nguruwe zinafugwa kwa wingi mno

Sio wapenda usafi. Kula yao ,vaa yao, sio watu wakujipenda sana

Miswaki mara nyingi huwa niya miti(SIO KWAMBA MADUKANI HAKUNA ILA NI MAZOEA) ingawa sio wote

Rangi ya udongo ni udongo mwekundu.

Usafiri upo ila mtapangwa kama magunia ya mchele, kama kuna watu wanajua kupanga watu kama viroba vya mizigo utawakuta huko, labda kama unausafiri wako binafsi

Kila mahali utasikia neno SAITA,SAYUU,BARAGAHE,DERO, SHIDIKAH kariri hayo maneno ni comon kwa dongobesh

Ahsante
 
Back
Top Bottom