Vita ya kwanza ya kijana si biashara, ni chakula

Vita ya kwanza ya kijana si biashara, ni chakula

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,009
Reaction score
61,260
kipindi cha nyuma tukiwa tunarudi safari za kikazi wilayani namuona boss wangu anajaza viroba vya vyakula mpaka cruiser inajaa ananishauri ninunue debe za mahindi me bishoo hapo naona huo ni ushamba nanunuaje mavyakula wilayani wakati mkoani masoko yapo na kibunda nitakuwa nacho.. nadharau mpaka ninapokuja kushtuka hela zimeisha na chakula sina ndani..oyaaa hamna kitu muhimu kama msosi. Ukiwa na njaa kali hata atokee pisi mbele yako, akili haitakuwa huko chini unachofikiria ni ugali au wali.

Ukiwa na njaa huwezi kukaa umsikilize mtu kwa makini. Anaweza akawa anakupa michongo ya kutengeneza hela, lakini wewe kichwani unasikia tu wali maharage... wali maharage...kama huamini mtafute mtu mwenye njaa kali muonyeshe videos youtube kuhusu miradi mizuri hata ya ufugaji bata bukini uone kama anaweza kuangalia hio video mpaka mwisho halafu mtafute akiwa kashiba mpe videos anasikiliza mpaka mwisho..

hata mashuleni me nawaonea huruma wanafunzi najua ikifika mchana saa 6 kuelekea 7 tumbo linaanza kupiga kelele tumbo lipogi kama ubongo, kile kipindi cha mwisho kinakuwa ni formalities tu. Mwalimu anafundisha mbele, wanafunzi nyuma wanahesabu saa zilizobaki waende kula.Ukiona mwanaume anakuja kukulilia anakwambia hajala muagizie msosi usimpe hela.. ubao ni mbaya sana ..mtu hawezi kukaza akiwa na njaa anaweza kudhalilishwa asipokuwa makin anauza utu wake.

vijana tusikosee hatua. tusianze kufikiria biashara , uwekezaji, mafanikio wakati hata suala la chakula halina uhakika. Kaka yangu, ukilala leo hujui kesho utakula nini, ni ngumu sana kufikiria maendeleo ya muda mrefu.

Step ya kwanza kwa kijana ni kuhakikisha suala la msosi halikupi stress kila siku. Uwe na uhakika wa kula. Uwe na stock ya vyakula au kipato kinachokupa amani ya tumbo. Ukishamaliza vita ya chakula, akili inaanza kufunguka kufikiria mambo mengine.

Kuna muda niliwahi kubanwa na njaa nikaingia hotelini nikaagiza msosi nikala hela ya kulipa sina nikawaambia kaeni na hii smartphone yangu nitakuja kuichukua nikaweka bondi.. vipi we mdau umewahi kufanya tukio gani lisilo la kawaida kwa sababu tu kujinusuru na njaa?
 
Back
Top Bottom