mkwawa complex
Senior Member
- Dec 15, 2016
- 183
- 150
NIMESHAKUGUNDUA.KUMBE WEWE NI MJUKUU WA "KINGUNGE NGOMBALE MWIRUU".MNAMKASHIFU MUNGU,HALAFU MKIONA MNAKARIBIA kufa,MNAMRUDIA HARAKA-HARAKA.
Mungu ni mwema sana ,anajua yote yaliyopita ya sasa na yajayo. Kimsingi Mungu ameruhusu yote yanayotokea kutokea ili apime upendo wako kwake,je unampenda ,uko tayari kumtetea ,ikitokea unatakiwa uchague utamchagua nani yeye au shetani.hakuna kingine ni hicho tu haya yote yanayotokea ni kipimo tu.Kwa hiyo umepewa choice, Inasikitisha sana kwamba humpendi kwa sababu umeingia kwenye mtego wa shetani anayetaka wafuasi wa kuchomwa naye!Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.
1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)
2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?
3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?
4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.
5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.
6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.
Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Kiboya boya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Inaonekana uko stressed muda huu (point yako ya sita) as if kuna jambo baya umefanya,linakuumiza,unalijutia
Kama iko hivyo kweli ni heri ukatubu kwa imani yako na kuamini sisi binadamu hakuna mkamilifu,wote tunamkosea Mungu
Kwa imani yangu nafahamu Mungu ni pendo na huwa hakusudii baya lolote litutokee
Sasa kama humpendi yeye manake hata ndani yako hakuna upendo
USHAURI
Usipende kumuongelea Mungu kiboya boya kama unawongelea wachumba zako huko
Hayo maswali # 1,2&3 nimeshindwa kuyajibu kwasababu sipo into dini kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23]Nendeni kazini hizi dini haziwafikishi popote.
Kichwa weweUna mawazo yasiyo na majibu yaliyozidi uwezo wa ubongo wako. Hali hii itakupelekea kuwa kichaa.
Sasa rafiki fanya hivi kabla ubongo wako haujafyatuka fyuzi. Kama una pesa, andaa safari (ni vema ukawa na mtu mnayependana/kuelewana) nenda mahali pazuriiii fanya utalii pumzika, kula na kunywa vizuri, jichanganye usiwaze kabisaaaa futa maswali kichwani mwako. Tafuta mwalimu mwenye uelewa uanze kusoma/kujifunza vitabu kuhusu maswali yako. Kama huna pesa ..... lala muda mwingi na achana kabisa na mawazo uliyonayo. Jione unastahili kuishi upendavyo, fanya kazi kwa bidiii kutafuta chakula na mahitaji yako. Maisha lazima yaendelee bila kujali unakubali uwepo wa Mungu au la.
Pole sana nduguMoyo umefanya PAAAAAH!!!!!.
hii threadddddd.
Cc:aluwatan
Ni kweli kabsa....but inawezekana sifa tunazomvika zingine hana. Au pengine mahala kwenye maandika waandishi waliongeza yao...!KUTAMBUA UWEPO WA MUNGU NI MOJA YA SIFA YA MTU MWENYE AKILI.
Mi siamini kama ipo jehanamu au siku ya mwisho. Ni uongo tu wa wazungu, ukifa utazaliwa tena
Mimi naamini tofauti kabisa na hii ni scientific. Kuwa utazaliwa, utaishi na mwishowe utakufa na ndiyo mwisho wako kwa kila kitu. Hakuna maisha baada ya kifo!! Hii ya kutegemea uzima wa milele, ni huruma ya kutenganishwa na wapendwa kwa sababu tu ya kifo.Mm pia mara nyingi nimekuwa nikiamini kuwa ukifa unazaliwa tena kwa mtu mwingne japo utakuwa hujitambui kuwa uliwahi ishi duniani,, ila hayo ni mawazo yangu naamini kuwa MUNGU anajua nisiyojua maana yeye ndo muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo
Swali ka msingi, shetani ndio mwanzo wa dhambi na maovu, hapo kabla ya shetani ilikuaje mpaka akatokea. Huyo malaika lucifer, aliongozwa na nani kua shetani?1....jehanamu iliumbwa kwa ajili ya ibilisi na malaika wake, ila wewe binadamu unapofanya matendo ya ibilisi yaani kuungana na ibilisi nawe unakuwa sehemu yake ibilisi....kumbuka hao malaika hata huyo ibilisi mwenyewe walikuwa malaika wa Mungu
Mungu huamua analolitaka alafu katika hayo huwa akosei..Ni kweli kabsa....but inawezekana sifa tunazomvika zingine hana. Au pengine mahala kwenye maandika waandishi waliongeza yao...!
Haileti maana pale tunaposema kwamba mungu atatuchoma wenye dhambi milele na milele....!
Yaan unaishi dunia miaka 80. Unafanya dhambi say kwa miaka 70...then unakuja kuchomwa kwa a billion years plus....I dont get it!
Labda si kwa moto huu tunaoujua....and by the way...wakati tunachomeka huko...yeye Mungu atakuwa anapata faida gan!? Naamin kwa kuwa ni Mungu wa upendo atakuwa anaumia sana.
Nimeipenda hii, unaonaje mkuu ukatenga muda na kufafanua zaidi,.Ninafurahi kuona watu wanahoji kuhusu Mungu. Kwa ufupi, Mungu ni dhana tu. Hivyo kukesha kuiomba dhana ikusaidie ni kichekesho. Ikiwa unaamini kuwa Mungu ni wazo, basi tambua kuwa kila kitu
kipo ndani ya uwezo wako. Na utagundua kuwa
Mungu pekee ni wewe mwenyewe na ikiwa wewe
ndiye Mungu basi na jirani yako naye ni Mungu.
Kwa nini? binadamu ni binadamu tu, labda tutofautiane
tabia tu, ila binadamu ni binadamu tu.
Wewe ndio mwanzo na mwisho wa kila kitu. Rejea
mjadalawangu wa "Usipokuwepo,Hakuna
Kilichopo". Inahitaji utulivu kidogo kuelewa.